10 March 2011

Waliokufa Loliondo wamsikitisha mchungaji

*Asema wametoroshwa hospitali wakiwa hoi

Na Said Njuki, Loliondo

IDADI kubwa ya wagonjwa wanaokufa kabla na baada ya kupata tiba ya Mchungaji Ambilikile Mwaisapile katika Kijiji cha Samunge Loliondo, Arusha
wameelezwa ni wale waliotoroshwa hospitali mbalimbali wakiwa mahututi na kukimbizwa kwa mchungaji huyo wakitaraji kupatiwa tiba ya haraka.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari juzi nyumbani kwake alipoulizwa na waandishi hao juu ya vifo vinavyowakuta wagonjwa hao wakiwa katika msururu wa kupatiwa tiba hiyo au baada ya kutibiwa.

“Nimesikia baadhi ya wagonjwa kufariki dunia wakiwa bado hawajapata tiba au baada ya kupatiwa tiba hii, lakini idadi kubwa ya wagonjwa hao naamini ni wale wanaotolewa katika hospitali mbalimbali wakiwa wamekata tamaa ya kupona na badala yake kukimbizwa kwetu.

"Hakuna anayefurahia kifo chake wala cha ndugu yake, lakini ni wazi hakuna binadamu yeyote atakayezuia kifo cha mtu isipokuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe. Na kwa idadi kubwa ya wagonjwa waliofurika hapa kijijini vifo kutokea si jambo la ajabu," alisema Mchungaji huyo akionyeshwa kusikitishwa na taarifa hizo.

Habari zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa wagonjwa wengi wa magonjwa sugu kama sukari, saratani, kifua kikuu na UKIMWI wameombewa ruhusu katika hospitali hizo na kuruhusiwa kwa lengo la kukimbizwa kwa mchungaji huyo, huku wengine wakitoroshwa kujaribu bahati yao ya uponyaji.

9 comments:

  1. hivi hapo Tanzania mpo zama gani ? na hapo mko na serikali au ndo siasa za kuogopana kama muna amini fortune teller si mngempatia ward hapo Kcmc au hospital yoyote ya taifa,au hamjui thamani ya roho za watu,
    Na hao watu wakianza na magonjwa ya tumbo huyo mganga atawamudu

    ReplyDelete
  2. Naona ndugu hujaumwa bado,alafu fanya uchunguzi kabala hujasema au kubeza,huduma ni ya hiyari na wanokwenda kule ni wenye kuhitaji msaada ambao wewe huwezi kuutoa.

    cha msingi ni kumsaidia kuwenka mazingira yatakayo mwezesha kutoa huduma kwa haraka.anahitaji wahudumu zaidi,vikombe nk,kaomba huo msaada.

    watanzania Tubadilike!!!

    ReplyDelete
  3. Kimsingi nafikiria kama ingekuwa ni nchi za wenzetu zilizoendelea huyu mzee angepewa ushirikiano mkubwa sana, sasa sijui matamko ya viongozi wetu wakuu yanasubiri nini. Pili, pia tahadhari zinatakiwa zichukuliwe endapo kama hiyo dawa itakuwa na madhara kwa binaadamu. ili baadae Serikali isianze kuwalaumu watu waliopewa huduma hiyo. Mimi nionavyo huyu mzee ni kama 'LULU' kwa Tanzania ila sielewi kwa nini bado hatujatambua hili. na inakuwaje tunadharau swala kubwa kama hili.

    ReplyDelete
  4. Ukitaka uthaminiwe kwa kazi yako basi kuwa msanii au mwanamichezo aah utaona jinsi gani viongozi wa nchi wanavyokupapatikia,leo hii mara kempisk kesho ikulu na kwengineko.lakini serikali bado haijajua umuhimu wa huyu mzee kwa jinsi anavyoisaidia hii jamii yetu.laiti huyu mzee angelikuwa yupo katika nchi za magharibi aah sijui angekuwa na thamani gani...MUNGU ndio anayejua.leo hii MUNGU ametupa huyu mzee lakini hatuoni umuhimu wake,badala ya kuimarisha huduma ile sehemu wao wanataka kumfungia kwa kuwa wao wameshapata hio tiba hio sio sahihi kabisa.namshauri waziri asijishuhulishe na hii dawa kwa kutaka kuifanyia vipimo ni bure tu kwani haitatoa majibu yoyote yale.cha msingi awapime hao waliokunywa hio dawa....wapo maaskofu,wakuu wa mikoa na mawaziri wameshakiri kama dawa inafanya kazi kwa hio anaweza kuwatumia hao katika kupata vipimo vyao.

    ReplyDelete
  5. Anselm,Biluganyuma GervaseMarch 10, 2011 at 3:33 PM

    Kwakeli haya ni maajabu ya Mungu kama watu wmethibitisha kupona kwa dawa ya mzee Amblikile basi naona kuna umhimu wa serikali yetu kutoa support kwake na kmfanyia alivyoomba kufanyiwa kama kurekebisha miundo mbinu nk ya kutolea huduma hiyo

    ReplyDelete
  6. Haya mambo ni ya kiimani tu. Hakuna tiba hapo, usanii mtupu. Mbona kuona wizara ya afya wanataka kuichunguza hiyo dawa, weshaanza kutoa sababu kwamba "hata wakichunguza hawatoona chochote, tiba hii ni ya kiimani, kama mtu anaamini atapona na kama haamini haponi". Sasa hili si changa la macho. Huu ni mchezo wa kuigiza wa kawaida unaowavuta watu wajiunge na dini yao tu. Itakuwaje hiyo dawa itibu maradhi kibao ambayo vyanzo vyake ni tafauti?

    ReplyDelete
  7. hakuna swala la kuvutwa kujiunga na dini,wala mchezo wa kisanii..kilichopo ni huduma ya afya,watu wanabarikiwa na wanagundua mambo. embu kuwa uwe na akili

    ReplyDelete
  8. Imani ya mtu haipimiki maabara.Kazi ya Mungu inazidi akili za mwanadamu. Achani wanaoona inawasidia wakatibiwe. Wewe ambaye unaona haitakusidia hulazimishwi kwenda. Acheni kabisa kumjaribu Mungu.

    ReplyDelete
  9. Mimi Naona Pamoja na swala la imani bado kuna usainii na kwamtazamo uliopo kinachotibu sio dawa ila ni MKONO wa babu sababu kama ni dawa na umati mkubwa namna hiyo kwanini hao wasaidizi wasimsaidie kuigawa mpaka achote na mkono wake tu?inamana yeye babu anakula saa ngapi? haendi msalani wala halali?

    ReplyDelete