04 March 2011

Mrema, Wassira waivaa CHADEMA

Na Waandishi Wetu

VYAMA vya upinzani vimetakiwa kuangalia njia wanazotumia katika kupata madaraka kwa kuwa baadhi yake hasa malumbano zinaitumbukiza nchi kwenye
maafa na maangamizi kama ilivyowahi kutokea kwenye nchi nyingine duniani.

Akizunguma na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbunge wa Vunjo, Bw. Agustino Mrema alisema malumbano yanayojumuisha maandamano pamoja na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupinga ufisadi serikalini ni hatari kwa usalama wa nchi.

Kwa mujibu wa CHADEMA maandamano hayo ni kupinga hali ngumu ya maisha, iliyosababishwa na kupanda kwa bei ya vyakula, bei ya umeme na kupinga malipo kwa kampuni ya Dowans.

Bw. Mrema alisema serikali iondolewe kwa kutumia njia ya katiba na si njia za mkato, kama maandamano kwa kuwa njia hizo zinaleta matatizo makubwa zaidi na kusababisha maasi na uvunjaji wa amani nchini na kuliangamiza taifa kama Somalia ilivyoangamia.

"Wapinzani wamepewa kazi ya kupambana na ufisadi kwa kutumia bunge  na kama wakishindwa ni udhaifu wao wenyewe na sio serikali. Ufisadi hauwezi kumalizwa kwa maandamano bali ni kubuni sera mbadala  na mikakati endelevu ya kuleta maendeleo," alisema Bw. Mrema.

Kauli ya Bw. Mrema inashabihiana na ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Bw. Stephen Wassira aliyoitoa kwenye Kipindi Maalumu kilichorushwa juzi usiku na Televiesheni ya Taifa na krudiwa jana mchana, akisema chama hicho kimekuwa kikiwachochea wananchi kuindoa serikali kwa maandamano, jambo ambalo ni kinyume cha katiba.

Hata hivyo, alisema CHADEMA haina uwezo wa kuiondoa serikali madarakani kwa njia hiyo, lakini kwa kutamshi yake tayari wamevunja katiba na sheria za vyama vya siasa na ile ya usalama wa taifa.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi, Bw. John Cheyo alionya hali yoyote ya kuhatarisha amani nchini akisema hata CHADEMA wanafanya maandamano yao na mikutano kwa sababu Tanzania kuna amani, hivyo hawana budi kutoa hotuba ambazo zinalenga kuhimiza amani.

"Wanasiasa tuache hisia za ushabiki na kupenda kuzungumzia vitu ambavyo ni hatari kwa taifa, alisema Bw. Cheyo.

Aliongeza matatizo ya wananchi yasichukuliwe kama njia ya kukaa na kuanzisha mijadala isiyo ya msingi isipokuwa jibu lake ni kufanya kazi kwa bidii na kama mijadala ikiendelea inaweza kutokea hali mbaya ya siasa kama ilinayoendelea nchini Libya.

Mbali na hilo, Bw. Cheyo alitaka Rais Kikwete kutimiza ahadi yake ya  kuchukua maamuzi magumu kwa mambo yanayolalamikiwa katika serikali yake bila kujali kama yatawaudhi wanasiasa marafiki waliomo katika serikali yake.

Alimtaka Rais Kikwete kuwahakikishia Watanzania amani, kuwaondoa katika hofu inayojitokeza na hali ngumu ya maisha ikiwemo gharama za kupanda kwa maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Cheyo alisema Serikali ya Rais Kikwete imepoteza matumaini na kuleta hofu kwa wananchi na ikiwa ataendelea kukaa kimya bila kuwahakikishia amani nchi inaweza kuelekea kubaya.

"Rais Kikwete anatakiwa kufanya maamuzi ambayo yatawaridhisha Watanzania, anatakiwa kufanya maamuzi, hata yasipowapendeza marafiki zake, ili kulihakikishia taifa amani," alisema.

Alisema amani Tanzania imeanza kutoweka na ikiwa Rais Kikwete ataendelea kukaa kimya bila kuchukua uamuzi wananchi watatakiwa kufanya maandamano kudai amani kwa sababu ni haki yao.

Katika hatua nyingine Cheyo alisema kuhusu suala la umeme la mkataba kati ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na kampuni ya DOWANS wanasiasa wanatakiwa kuiunga mkono mahakama na kuiacha ilishugulikie kisheria kuliepusha taifa katika malumbano yasiyokuwa ya msingi.

Bw. Cheyo pia amemtaka Mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Rostam Aziz kuchagua moja la kufanya kati ya biashara au siasa kumsaidia rais na serikali yake kufanya kazi.

"Rais anatakiwa kujua hali ya hewa ni chafu, hali ya hewa kwa Rostam sio nzuri, achague moja la kufanya kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ameisaidia serikali na taifa na kama angekuwa kwenye chama changu ningeshamtimua," alisema Cheyo.

Imeandikwa na Nassra Abdulla, Amina Athumani na Addolph Bruno

32 comments:

  1. Cheyo na Mrema waache kujipendekeza kwa chama tawawla, wameona wamezeeka ndiyo maana wanaona wajipendekeze ili serikali iwafikirie baaadae.Kweli CHADEMA wanaweza kutumia bunge lakini ni wachache na hoja yao haiwezi kusikilizwa sana watazomewa na wana CCM pamoja na CUF. Tusiogope yanayotokea LIBYA kwani kwetu hapa hayawezi kutokea kulingana na misingi ya taifa letu iliyoundwa na Mwl. kama yakitokea si sasa hivi, iaweza kutokea labda baada ya miaka mingi ijayo kama kuna wasiwasi basi CCM na CHADEMA wakae pamoja wajadiliane ili kutafuta namna gani kero hizi za CHADEMA zinzvyoweza kutatuliwa kwa masilahi ya taifa.

    ReplyDelete
  2. Cmm acheni kutesa wananchi, sera zenu mbovu hamna cha kujitetea. Hao akina Mrema ni wachovu tu nao wanaangalia maslahi yao.

    ReplyDelete
  3. Wasira ni rafiki wa mafisadi.Watanzania tumechoshwa na ukandamizaji unaofanywa na CCM.CCM sasa hatuitaki.Serikali ikianzisha vurugu au kuwakamata viongozi wa CHADEMA huo ndio utakuwa mwanzo wa vita.Wananchi tutatumia marungu na mapanga na mikuki kama Mkwawa, nyie CCM mtumie mabomu yenu hayo ya Mbagala na Gongolamboto. Tuko tayari kufa kwa kuondoa ufisadi walau kizazi kijacho kiishi vema kwenye nchi yenye asali na maziwa tuliyojaaliwa.Hahaaaaaa!

    ReplyDelete
  4. CCM acheni kupeana uongozi katika ngazi mbalimbali kirafiki.Sasa wananchi wamefungua macho hata mkiwatisha hamuwezi,mbona mabomu sasa tumeyazoea.Hatuogopi hivyo vibomu vyenu mlivyonunua kwa pesa nyingi wakati watu hawana dawa hospitalini.Ushauri wa bure,Rostam ajihuzuru ubunge,Lowasa ajihuzuru ubunge,Ngeleja ajihuzuru uwaziri.Mkifanya hilo tu umma wa watanzania watarudisha imani kwa CCM kwa asilimia fulani.Vinginevyo acheni CHADEMA wachape kazi.

    ReplyDelete
  5. Maandamano ya CHADEMA kuandamana kulalamikia hali ngumu ya maisha hayako specific,kwa sababu hali ya maisha kuwa ngumu ni tatizo la miaka mingi.And it is not something that is gonna change tommorrow. Tatizo hapa ni sera ziboreshwe hasa zinazolenga watu wenye maisha ya chini kabisa ambao ndio wengi.
    Rais Kikwete katoka na "Kilimo kwanza".Jengeni hoja kwenye hili kwa sababu ndio hapa pekee tutakapomaliza tatizo la mfumuko wa bei ya vyakula.Jengeni hoja bungeni kwenye bajeti,na vikao vingine vya bunge,badala ya maandamano nchi nzima.
    Isitoshe,baada ya maandamano haya,hali ngumu ya maisha ndio itaisha?Na je isipoisha,kwa muda mfupi kama CHADEMA wanavyotaka,then what,ndio wataiondoa serikali madarakani kama wanavyosema "mpaka kieleweke"??.
    CHADEMA kuweni realistic,you folk should put forward the targets which are achievable.!!

    ReplyDelete
  6. Hawa wanalipa fadhila. Kupewa uenyekiti wa kamati za bunge ingewezekanaje kwa vyama vyenye mbunge mmoja? Hii inawezekana? Walipewa support na CCM, lazima waitetee CCM.

    ReplyDelete
  7. Wewe Mallya Saidi,unajua pesa wanazoiba viongozi walioko madarakani zingesaidia kupunguza makali ya maisha kwa kutoa ruzuku kwenye vitu kama vile: gharama za umeme,vyakula toka nje,viwanda vidogovidogo,kilimo n.k. Kwa kuwa CCM inagawa madaraka kiurafiki basi kila kiongozi anaiba kwa kwenda mbele.Hivyo wananchi wakielimishwa watasimamia haki zao.Mishahara inakatwa kodi kubwa lakini inaishia kwa wachache.Naomba Mallya Saidi ubadilike.Hapa hatuna ushabiki wa chama bali ukweli.

    ReplyDelete
  8. kaka Mallya said,hongera kwa kuwa na upevu wa mawazo.japo sikufahamu naamini ww ni mmoja wa watanzania wenye busara.ugumu wa maisha ya watanzania usitumiwe na wanasiasa kujitafutia umaarufu then tuushabikie ila tuchape kazi ili tuutokomeze umaskini huu wa kutisa.lakini kama amani na mshikamano vikitoweka pia hatutakuwa na nafasi ya kuutokomeza bali tutauzidisha zaidi ,maana pengine tutakuwa wakimbizi ktkt nchi jirani.tukemee mabaya kwa busara na tuikosoe serikali kwa hekima bila kutukana viongozi wetu au kuwalaani.maana wapo wazuri na wabaya,wale mafisadi tutumie sheria zaidi kuwahukumu,maana sheria ipo kwa ajili ya wahalifu.pia tujue siasa ni propaganda jamani tusiishabikie kupindukia.

    ReplyDelete
  9. Hivi huyu jamaa Rostam anahusishwa vipi na ugumu wa maisha ya watanzania? ina maana Rostam ndiye aliyeshika akili za viongozi ,watendaji na wanachi wa tanzania yote kiasi cha kushindwa kufikiri jinsi ya kujindoa katika matatizo tuliyonayo? tatizo siyo Rostam bali ni sisi wananchi na viongozi tulio nao. hivi Rostam ndiye anayepanga na kupitisha matumizi makubwa ya kifahari kwa viongozi na watendaji wetu katika serikali, posho kubwa,magari ya kifahari wakati wananchi wa kawaida hata mlo mmoja shida,tofauti kubwa ya kipato,huduma za jamii wakati nchi ni yetu sote, ni lazima tubadilike na kukubari kuwa hawa wenzetu pia watu na wanastaili kupata huduma bora, hakuna mwananchi atakaye kubari kuandamana na kuiondoa serikali madarakani kama atakuwa anapata huduma bora za jamii kama shule,tiba usafiri na mlo wake wa kila siku.lakini kwa stahili hii ya kufanyana wajinga hakutakuwa na amani ya kudumu, maana itafika wakati inakubidi mwananchi uchague kufa kwa njaa na kwa kukosa huduma muhimu au kufa kwa kudai haki yake.tusimgeuze Rostam mbuzi wa kafala wakati hata nyinyi wanasiasa wengine mnasababisha nchi hii kwenda pabaya kwa kujari zaidi maslahi yenu,

    ReplyDelete
  10. maisha magumu ya Watanzania yasiwe mtaji wa wanasiasa,kaeni bungeni mjadili namna ya kuboresha huduma za jamii. chadema, CCM na vyama vingine vya upinzani zungumzeni mstakabali wa taifa letu wanaotaka kuchochea maandamano kuing'oa serikali madarakani wanadanganyika hiyo vita wanaisikia tu kwa majirani, haijawapigia hodi haya endeleeni, mtoto akililia wembe hupewa! ujinga wetu ulituongoza kuichagua CCM licha ya sera nzuri zilizosemwa na chadema wakati wa kampeni, mbona kwenye masanduku ya kura hatukujitokeza kama kwenye mikutano ya chadema, halafu tunasingizia eti kura zilichakachuliwa na sasa tumechoka na ufisadi tuwaondoe kwa maandamano wakati ni miezi michache tu imepita tangu uchaguzi umalizike? nani aniambie ni kipi kipya sasa ambacho chadema hakikusema wakati wa kampeni? kwa nini hamkutumia nguvu hiyo kuindoa CCM kwa kura, mbona maeneo waliofanya hivyo chadema ilishinda? acheni kutudanganya subirini uchaguzi 2015, watu wafanye kazi kwa sasa.acheni kuchochea vita ikitokea hata huo mlo mmoja ya watoto wako hautaupata na utajenga visasi visivyoisha ndani ya nchi hii kwa vizazi vyote.'akili ya kuambiwa changanya na yako'tusiwe remote control watanzania wenzangu.

    ReplyDelete
  11. Mrema na Cheyo ni makuadi wa CCM kwa sasa. Mrema anasahau alipokuwa NCCR jinsi wananchi wa kawaida walivyosumbuliwa wakati akipinga ufisadi? Sasa amejumuika nao!
    CUF, CHADEMA, NCCCR na wengine msikubali 'mihadhara' kutoka kwa viongozi wa CCM kana kwamba wao ndiyo wana akili zaidi ya wengine!
    Wasio wana-CCM ni Watanzania /Wazalendo vile vile ni wapembuzi yakinifu pia, kwa hiyo wasikilizwe.

    ReplyDelete
  12. Hoja ya msingi ni kwamba CHADEMA wamevunja katiba ya Jamhuri?

    Je, mikutano ya hadhara, maandamano inaweza kuwa njia ya chama cha siasa kujiimarisha? Na je mikutamo, maandamano inaruhusiwa kwenye katiba?

    Lengo la Chama chochote cha upinzani duniani ni kukitoa madarakani chama tawala na kuchukua dola.

    Hivi kweli kwa Chama kama CCM wanataka watolewe madarakani kwa njia gani kama si kuwajengea wananchi uelewa wa mambo yanayoendelea katika nchi na kuonesha dhahiri kwamba utawala wa nchi sasa unahitaji chama mbadala?

    Halafu Raisi anapoonesha ku-panic kwa sababu tu chama cha upinzani kinafanya maandamano na mikutano ya hadhara then inaonesha plainly kwamba there is something wrong kwenye administration yake. Mimi sikumbuki hata siku moja kwamba mzee Mkapa alishawahi hata kuwa disturburted kwamba kuna wapinzani ndani ya nchi hii- alikuwa anasema mara kwa mara - "wadharauni"!!

    Panic ya serikali inawapa CHADEMA momentum kubwa zaidi kwa sababu inaonekana kweli wameguswa na mambo wanayotuhumiwa nayo.

    ReplyDelete
  13. Ndg CCM sisi vijana tunawapenda CHADEMA, elewa hilo kwa kifupi wala usipoteze muda. Kwa speed hii yenu ya kobe ya kuwaletea wananchi maendeleo mtatoka kwa People Power tu!

    ReplyDelete
  14. DOminic
    Sreven wasira ni mfisadi.Ubunge kaununua,Wananchi wa Bunda ni mshahidi.Walitoa siri hiyo katika mkutano wa hadhara ndiyo maana anahasira

    ReplyDelete
  15. Tusichanganye mambo,you might have a right in anything,but the way you exercise it matters. Issue sio rais ku-panic,lets talk on what he addressed! Kwa wale waliomsikiliza Rais Kikwete alisema kuandamana ni haki ya kila mwananchi,lakini fursa hiyo isitumike vibaya kuchochea vurugu.
    To me,I think the President was wise and diplomatic kuwa hakutaka kuzungumza kwa undani yale yanayozungumzwa na kina Mbowe na Slaa kwenye mikutani hii inayoendelea.Tonasoma magazetini Mbowe na Slaa wanaongea kwa kujiamini na kutamba,Rais asipofanya this and that..tutamtoa madarakani kwa kuandamana kama Tunisia,Egypt na kwingineko..Sidhani kama ni sawa kutoa speech kama hizi na hasa unapoongea na wananchi wenye hali ngumu ya maisha.Do we need to be there?
    Mchangiaji wa kuwa Mkapa alikuwa hababaishwi na wapinzani,you er right bro,but kumbuka zama zimebadilika.Mwananchi wa miaka ya 80-90 aliyeamini upinzani ni vurugu,sio wa leo,fikra za watu zimebadilika,teknolojia na mambo mengine mengi..Besides,I believe sio sawa kuwapima viongozi waliopita na wa sasa katika rula moja.Tunamsoma Nyerere kama kiongozi wa kuigwa aliyechukia udini,ukabila,wizi n.k But who knows the other faces of Nyerere?How many scholars were demoted and assassinated by that old man?Do you remember kulikuwa na magazeti,redio,televisheni ngapi wakati ule?
    Leo tuna uhuru wa kumchambua kiongozi hata Rais aliyeko madarakani kivyovyote,how about wakati ule?
    Brothers,it is important that any movement threating our unity and peace must considered and addressed in a correct perspective..

    ReplyDelete
  16. Tusichanganye mambo,you might have a right in anything,but the way you exercise it matters. Issue sio rais ku-panic,lets talk on what he addressed! Kwa wale waliomsikiliza Rais Kikwete alisema kuandamana ni haki ya kila mwananchi,lakini fursa hiyo isitumike vibaya kuchochea vurugu.
    To me,I think the President was wise and diplomatic kuwa hakutaka kuzungumza kwa undani yale yanayozungumzwa na kina Mbowe na Slaa kwenye mikutani hii inayoendelea.Tonasoma magazetini Mbowe na Slaa wanaongea kwa kujiamini na kutamba,Rais asipofanya this and that..tutamtoa madarakani kwa kuandamana kama Tunisia,Egypt na kwingineko..Sidhani kama ni sawa kutoa speech kama hizi na hasa unapoongea na wananchi wenye hali ngumu ya maisha.Do we need to be there?
    Mchangiaji wa March 4, 2011 3:34 AM kuwa Mkapa alikuwa hababaishwi na wapinzani,you are right bro,but kumbuka zama zimebadilika.Mwananchi wa miaka ya 80-90 aliyeamini upinzani ni vurugu,sio wa leo,fikra za watu zimebadilika,teknolojia na mambo mengine mengi..Besides,I believe sio sawa kuwapima viongozi waliopita na wa sasa katika rula moja.Tunamsoma Nyerere kama kiongozi wa kuigwa aliyechukia udini,ukabila,wizi n.k But who knows the other faces of Nyerere?How many scholars were demoted and assassinated by that old man?Do you remember kulikuwa na magazeti,redio,televisheni ngapi wakati ule?
    Leo tuna uhuru wa kumchambua kiongozi hata Rais aliyeko madarakani kivyovyote,how about wakati ule?
    Brothers,it is important that any movement threatening our unity and peace must considered and addressed in a correct perspective..

    ReplyDelete
  17. Mimi si mwanasiasa bali ni Mtanzania aliyezaliwa kabla ya uhuru na kuishi na kuelimishwa wakati huo hadi tulipopata uhuru wetu kwa jitihada za viongozi waliojitoa wakati ule: Baba wa Taifa Hayati JK Nyerere, Simba Mzee Hayati K Mfaume, Mama Bibi Titi na wangine wengi hata wakina Fundikila hapa napenda kuwauliza wachangiaji baadhi wanaolaumu kila kukicha hali mbaya ya Watanzania na eti inasababishwa na mtu mmoja yaani Rais aliyeko madarakani; nyuma alilaumiwa Nyerere kwa Ujamaa, mwingine kwa Mzee Ruksa, na Mkapa kwa lile na sasa Kikwete kwa eti anataja kuhusu kudra za Mwenyezi Mungu; Je ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu hahitajiki leo katika maisha yetu? Ombi langu kwa vyama vyote vya siasa ni hili: Watuongoze, watushauri na watutie moyo katika utelezaji wa shughuli zetu binafsi kwa maendeleo ya Taifa letu. Maendeleo ya nchi hayaletwi na rais peke yake bali wote wenye moyo wa uzalendo. Ninayaona maendeleo yaliyopo nchini mwetu, leo usafiri wa anga nchini si kama miaka ya Ujamaa Dar- Bukoba Mwanza Mbeya nk ni kitu cha kawaida na wala si kwa matajiri peke yao, bali kwa Mtanzania wa kawaida ambaye anachakalika kuwajibika na kuona umuhimu wa kusafiri haraka kwa njia ya anga. Ukiangalia majumba ya fahari yanayojengwa na Watanzania Mbezi Beach, Moshi, Arusha Mwanza, Mbeya na hata Lushoto nk si sifa ya Watanzania. R. Mengi amezipata wapi fedha alizonazo, Billicans nao walizipata wapi, huyo wa Black Point naye je? Yapo mengi ya kujifunza kama vile JK alivyosema mwenye macho haambiwi tazama. AMANI YETU NI YA KUDUMISHA NA WALA TUFUATE MKUMBO WA MANENO YA MAJUKWAANI:

    ReplyDelete
  18. CCM imeshapoteza Mamlaka na haki ya utawala imeshawatoka. Madaraka imeshawatoka CCM. Wamebakia na Vitisho tu visivyotumia akili. Kama Gadaffi CCM waondoke waende wanakokujua watuachie nchi tulete maendeleo.

    CCM waende zao huko kwenye matawi yao nje ya nchi

    ReplyDelete
  19. Hivi watu wanapotoa maoni na kufika wakati mwingine wanaanza kuchanganya lugha nyingine badala ya lugha ya taifa ambayo ni kiswahili tatizo huwa ni nini haswa?Inamaana anapoamua kuweka kiingereza maana yake ni kwamba hajui kiswahili au vipi?,Tunatakiwa tujivunie lugha yetu.Sijawahi kuona mfaransa akielezea jambo halafu ikafika mahala akaweka kiingereza au mmarekani kazungumzia jambo fulani halafu a
    kaamua kuingiza kispanish ndani yake.Kunashida gani mtu akizungumza kiswahili peke yake ambayo ndio lugha yetu.

    ReplyDelete
  20. nguvu ya umma ni wakati wa ccm kwenda, tunajiaandaa kwenda iringa, mbeya, arusha, kilimanjaro, tabora dar, tafadhali shiriki kama uko katika mji hiyo. Zidumu fikra sahihi za baba wa taifa mwalimu julius k nyerere kwa kutupa amani na elimu bure.maadili yako yatatimia hata kama aupo hapa duniani.

    ReplyDelete
  21. Hata mie nashangaa kwa nini Kikwete siku aliposema lugha ya kuwacheka Chadema, au waziri mkuu Pinda, na Makinda walipounga mkono kuwazomea Chadema Bungeni mlinyamaza na kuona ni sawa. Mnasema watoe hoja zao Bungeni, lakini Bungeni wananyamazishwa na Makinda. Cheyo na Mrema kumbukeni hata ninyi siku za nyuma mlivyokuwa mnawachamba ccm. Chadema waendelee tu kuwaelimisha watu na huko siyo kuchochea vurugu, vingenevyo hata kuwazomea wabunge wa chadema ndani ya bunge na kuungwa mkono na Spika ni uchochezi wa vurugu. Mkuki mtamu kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Ccm mnanguvu bungeni kwa vile mpo wengi na pia mmenunua vibaraka Cuf, hivyo uwanja wa Chadema ni mikutano ya hadhara na maandamano. Msiwachagulie cha kusema, na wanaowasemea ni watu wazima na akili ya kujua uongo na ukweli. CCm tumieni maandandamano na mikutano ya Chadema kujikosoa na kujirekebisha hapo ndiyo mtakuwa mmejibu wanachodai maana siyo uongo wanachokisema juu ya ugumu wa maisha ya mtanzania wa kawaida.

    ReplyDelete
  22. Kama kuna mtu mwehu basi si mwingine isipokua huyu mzee wa kiraracha. Hivi amesahau kwamba alishapigwa mabomu ya machozi mpaka akawa haoni?? Tulishawaambia kwamba hili ni pandikizi la CCM hamkusikia. Kwanza anahistoria ya kuua vyama na kuvidhoofisha.
    Huo ubunge umepewa tu baada ya wana kiraracha kuona UMEFULIA upate angalao pesa kidogo za matibabu. Funga mdomo hutakiwi katika kizazi hiki cha vijana tunaotaka mageuzi ya kiuchumi.Tunaimani CEMENT kuuzwa Tsh 5000/= inawezekana kwani ni miamba tuliyonayo hapa. Wwe sera zako ni zakujisifu tu hunajipya.Umefulia shukuru Mungu CCM imekubeba .

    ReplyDelete
  23. CCM haijapoteza mwelekeo japo yapo matatizo ndani ya chama. Iwapo mtu anasema zidumu fikra za Baba wa Taifa Mwalimu JKN nakubaliana naye kwa moyo wote. Katika jamii yoyote duniani kuanzia familia, koo nk watu wake wana tofautiana- wapo wema na wabaya. Ndani ya CCM, CHADEMA CUF na vinginevyo watu wanatofautiana na matatizo hayakosekani. Zitto alishutumiwa na viongozi wake wakati fulani, na Shibuda naye mmm . Jambo la msingi kwa ajili ya matatizo ya hali ya uchumi nchini mwetu ni letu sote; na wala si la chama au mtu binafsi. Nawaomba viongozi wetu wawatumie wanauchumi wetu kushauri ni vipi tunaweza kukabiliana na matatizo yetu.

    ReplyDelete
  24. Ni jambo la kusikitisha kumsikia Mzee Cheo akizungumza hayo. Yeye na wazee kama Mrema wamepitwa na wakati. UDP ni Cheyo. Hakuna Chama pale. Mrema sijui ana sera gani na chama chake cha TLP.

    Mimi nawaomba wakae kando. Waiache CHADEMA ifanye siasa kama wao wameshindwa.

    CCM inapobadilisha kanuni za Bunge ili ziidhibiti Chadema ndani ya Bunge na Spika asiyeelewa maswali unategemea nini? CHADEMA watakwenda moja kwa moja kwa wananchi. CCM nao waende huko, nani kawazuia.

    CCM ilitumia pesa nyingi sana kuwazungusha mawaziri nchi nzima kuelezea walichokiita "bajeti" badala ya mikataba ya dhahabu. Wazunguke tena. Nchi hii imebadilika na hakuna cha kuzuia mageuzi yanayokuja, tena sio kwa vurugu bali kwa "ballot box".

    CHADEMA ni chama tawala mbadala, mkae mkijua.

    ReplyDelete
  25. Vitisho vina mwisho wake. Jifunzeni kwa waarabu. Mtu hawezi kutishiwa kuuawa kila siku. siku moja tutakuwa tayari mtuuwe lakini kieleweke. Mbona wa libya hawamuogopi Gaddaffi tena hata midege yake na majeshi yake watu hawayaogopi tena. Kwa nini CC< hawajifunzi. Vitisho havisaidii kitu tena!!!

    ReplyDelete
  26. Mhh kweli Ibilisi kasimama, Wairaqi waliposhangilia kuondoka kwa Saddam walifikiri watakuwa na maisha mazuri, lakini ya leo ni heri ya enzi ya Saddam walikuwa wanaweza hata kulala ingawa JK hafanainishwi na Sadam mana hawa kina Mbowe wangekuwa kwa Sadam saa hizi tushawasahau.

    Watunisia waliandama na leo hii bado hakuko shwari wala hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea. Misri Mubarrak kaondoka uchaguzi bado lakini haijulikani kama uchaguzi wenyewe utakuwa huru na wa haki maana washika sau kutoka nje wenye hisa kwenye serikali ya Misri ni wengi, mmoja kajipeleka eti kwenda kuandaa demokrasia, kenda na kundi la watu kutoka ughaibuni.

    Libya, wao pamoja na udikteta unaisemwa wa Ghaddafi lakini walikuwa better off, pato la chini lashinda masikini wa US, na lilikuwa dola 1500, na hawa walikuwa kwenye mfumo fulani wa kijamaa. Walibya ukiwa mtu mzima serikali inakupa makazi, pesa nyingi za mafuta zilirudi Libya, ndio maana pamoja na kuwekewa vikwazo muda mrefu Ghadafi hakutetereka. Propaganda za udikteta wa Ghadafi zinashangaza maana iweje dikteta au mjumbe wa tume za haki za binadamu za UN, amevuliwa juzi tu baada ya vurugu!

    Wazungu hao walikuwa wanatoka kwao kwenda mshauri namna ya kuinvest google LSE and Ghadafi. Sasa hao walioanzisha vita ya kwanza na ya pili ya dunia, na kumsupport Hitler ndio hao hao husababisha machafuko duniani hawana dini wala nini wanachokitaka wao ni kuitawala dunia na kuweka watu wao kwenye serikali. Tafuta kitabu cha mtu anaitwa Edmond Paris soma uelewe kinaendelea nini duniani. Leo hii ripoti ya UN imeshatoka inasema machafuko yaliyotokea nchi za waarabu na yanayoendelea Libya yamesababisha kupanda kwa maisha duniani kote kuanzia bei za mafuta, mbolea na vyakula. Tafuta hiyo ripoti mtandaoni. Kwa hiyo tusikae tunashabikia tu wakati hatuna pa kwenda!

    Na kinachoonekana wazi wazi shida kubwa wakiyonayo hao ni kumuondoa JK wala si kwa sababu za kisiasa hapana na wala si kuiondoa ccm subirini 2015, maana hili halikuanza leo kwa wanaofuatilia limeanza taratibu kwa matusi wee akasubiriwa awamu yake amalize ya kwanza lakini mikakati ikapangwa hata ndani ya ccm kuwa asipite awamu ya pili. Ndio maana nikasema si siasa kuna la ziada.

    ReplyDelete
  27. When people cross the barrier of fear, there is nothing you can do. Tafsiri ni hii, Watu wakishavuka ukuta wa woga, huwezi kutumia woga tena kuwadhibiti. CCM na Serikali waangalie namna ya kutatua shida za watu.

    Acheni ubishi tuleteeni UMEME na rudisheni pesa inayoibiwa ya watanzania. Tatueni kero za wananchi. hii itamaliza kelele zote

    ReplyDelete
  28. sokwe anasema nini? akili yake wasira ni kama ya sokwe ni mabaki ya ugunduzi wa Dr Leakey asituongopee maisha ni magumu kisa ccm alikuwa mageuzi amepozwa kwa uwaziri ndio kasahau watu wake akina mbowe wanahela bado wanateyea wanyonge viva chadema ikibidi tuwang'oeelee mbali mafisadi eti usalama wa taifa hakuna usalama na njaa maasikari wetu mazezeta mguu pande akili nyuma mbele tembea na chadema

    ReplyDelete
  29. Hasante kwa michapo ya maoni kila mmoja inambidi aseme mambo yanayomkera yakimzidi akilini. Pia mimi napenda kutoa maoni yangu kwa ndugu zangu Watanzania wote kwani kusema au kutoa maoni kwa jamaa unaowapenda na ulioishi nao kwa furaha na mapenzi,na hutaki yakawapata mabaya yakuwadhuru katika maisha yao. Watanzania wasifika Ulimwenguni kote kwa ubusara na mapenzi ya kupendana wao kwa wao na kwa wote wanaoishi nao katika nchi yao. Kwa kuwa kuna mwingiliano wa KISIASA uliovuma haraka nchi Tanzania katika miaka michache na inataka kusababisha kutokufahamiana kati ya wana SIASA basi ni bora sana kutumia akili na busara njema kutatua jambo hili kwa kukaa pamoja na kuelewana au kutumia kura za mashauriano na wananchi wote. Naomba muwe na imani kubwa ya kulinda nchi yenu na maendeleo yaliyopatikana tangu alipoanzisha BABA wa TAIFA MWALIMU MWEREVU Marehemu Julias K. Nyerere. Kumbukene kuwa Tanzania haijamwaga damu ya wananchi wake toka ipate UHURU kutoka kwa Waingereza. Hii ni neema kubwa sana kila Mtanzania inampasha ajivunie jambo hilo na azingatie Usalama na Amani ya nchi yake. Usikubali kung'owa jicho lako kwa vidole vyako, KUUWANA NA KUVUNJA NA KUTEKETEZA MAENDELEO yaliyojengwa nchini kwa manufaa ya Taifa zima ni sawa na mtu anayejidhuru nafsi yake.Maendeleo ya nchi ni manufaa kwa Umma wote wa Tanzania.

    ReplyDelete
  30. jamani wana wanchi tufunguke, tuache unazi wa chama kisicho wajali wananchi ila maslahi yao binafsi, Kama kwa kauli yake rais wa nchi kasema hawez kututoa katika shida tulizo nazo.
    anatakiwa kujua tanzania ina watu wana weza kutukwamu hapa tulipo. kama hawe he have to step down...

    ReplyDelete
  31. Wananchi mnalalamika nini? Mliichagua CCM ninyi wenyewe. Mlipewa kanga, kofia na fulana na mashati.

    Mimi naona tukubali kupokea zawadi zao nyingine walizo nazo: bei kupanda, rushwa kukuthiri, gharama za maisha kupanda, kukosekana kwa ajira, kukosa maji na umeme, ukatili wa polisi, kushuka kwa elimu(shule za kata), jamani zawadi ni nyingi sana walizonazo CCM na serikali yao.Mnikumbushe nyingine kama nimesahau.

    Kupanga ni kuchagua. Wa kumlaumu nani?

    Katika hali hii, siasa za CHADEMA zinanivutia. Naona kama ukombozi uko huko sijui wenzangu mnasemaje?

    ReplyDelete
  32. kiukweli CHADEMA inakubalika sana kwa sasa ndio maana hata wanasiasa wengine wa vyama vya upinzani wanajaribu kwa kila namna ili kuweza kutumia umaarufu na kukubalika kwa CHADEMA ili kuweza kujiletea maslahi binafsi.
    Wanachofanya ni kutaka kuiangusha CHADEMA kwa namna yoyote ile ili waweze kuwa pamoja na CCM kwa maslahi yao.
    Mrema amechoka sasa, ndio maana hata ameamus kuingia katika ubunge ili kuweza kujitengezea maisha yake ya uzee yaliyobaki na si kwa masslahi ya wananchi wa jimbo lake la Vunjo!!

    Cheyo akae pembeni awapishe wengine wakiendeleze chama alichopo kiukweli kimechoka na KIMEFULIA sana tu na sina hakika kama kitaweza kudumu hadi uchaguzi mkuu ujao. Anajilimmbikizia mali bila kuwajali wananchi wake!!
    Wazee wangu wakongwe wa siasa za "nji" hii hebu someni alama za wakti "NG'ATUKENI"

    ReplyDelete