11 January 2011

Ngoma CCM, CHADEMA Arusha bado mbichi

*Mbunge kutoka Tanga ashiriki tena uchaguzi
*CHADEMA waususia, wasema hawashiriki uhuni


Na Glory Mhiliwa, Arusha
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga kupitia CCM, Bi. Mary Chatanda jana alizidi kuleta mvutano wa
kisiasa baada ya kushiriki kwenye uchaguzi Jumuia ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Arusha na kusababisha wajumbe wa CHADEMA kuususia.

Hii ni mara pili kwa mbunge huyo kupitia Mkoa wa Tanga kuzua tafrani kama hiyo baada ya kushiriki uchaguzi wa meya na naibu wake katika Manipaa ya Arusha, hatua iliyopingwa na madiwani wa CHADEMA, huku CCM wakisisitiza kuwa ni halali kufanya hivyo.

Kutokana na kitendo cha Bi. Chatanda ambaye pia ni  Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, wajumbe wa CHADEMA waliondoka katika mkutano huo wakisema wasingewe kushiriki kuchakachua sheria kwa kuchagua wajumbe wa ALAT, huku akimshirikishwa mjumbe haramu.

Hata hivyo, vigogo wa CCM ambao ni wabunge mkoani Arusha na wajumbe wa kikao hicho, Bw. Edward Lowassa (Monduli), Lekule Laizer (Longido), Bw. Goodluck Ole Medeye (Arumeru Magharibi), Bw. Jeremiah Sumari (Arumeru Mashariki) pamoja na Meya anayelalamikiwa wa Manispaa ya Arusha, Bw. Gaudence Lyimo hawakuhudhuria.

Kikao hicho kiliendeshwa na mwenyekiti wa muda, Bw. Ismail Katamboi, ambaye ni diwani wa Kata ya Kisongo, ambaye alisema kukuwapo kwa wajumbe sita wa CHADEMA siyo sababu ya kuwazuia kuendelea na uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi, Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbles Lema alisema, "Sisi tumetoka ndani ya kikao hiki kwa sababu ya huyu Bi. Mary Chatanda ambaye ni mbunge wa Tanga, iweje leo apige kura za kuchagua wawakilishi wa mkoa Arusha,"  alisema Lema.

Alisema kuwa kinachofanyika sasa kwa Mkoa wa Arusha ni uhuni na siyo demokrasia, hivyo bora wawaachie wenye chama tawala wafanye kila wanachotaka, ila wao hawako
tayari kushiriki kuchakachua sheria kwa kuchagua wajumbe, huku wakimshirikisha mjumbe haramu.

Kikao hicho kilitakiwa kuchagua, mwakilishi ALAT Taifa, Mwenyekiti na makamu wake mkoa, katibu na Mweka hazina.

Pamoja na Bw. Lema wajumbe wengine wa CHADEMA waliosusa uchaguzi huo ni Bi. Cecilia Paleso, Diwani Viti Maalum- Karatu, Lazaro Maasai, Mwenyekiti Halmashauri ya Karatu, Joyce Mukya, Mbunge Viti maalumu Arusha, Winner Kitembe, Diwani wa Karatu na Mchungaji Israel Natse ambaye ni Mbunge Karatu.

Kikao hicho kilitakiwa kuwa na wajumbe halali 40, lakini baada ya wajumbe sita wa CHADEMA kutoka na wengine ambao hawakuhudhuria, walibaki 28 wa CCM ambao waliendelea, na kumchagua Bw. Godfrey Majola, mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru kuwa Mwenyekiti wa ALAT mkoa.

Msuguano huo umeendelea kutoka mkoani Arusha wakati vumbi lililotimka kutokana na polisi kuzima maandamano wa CHADEMA kupinga uchaguzi wa meya likiwa halitatua.

Katika tukio hilo, watu watatu waliripotiwa kuuawa na polisi kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, na chama hicho kimendaa mazishi ya 'kitaifa' yatakayofanyika katika viwanja vya NMC kesho.

Katika hatua nyingine, Anneth Kagenda anaripoti kuwa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, limewataka viongozi wa dini kukaa kimya na kutojiingiza kwenye siasa kwa kutoa msimamo kuhusu suala hilo la Arusha kwa madai kuwa kufanya hivyo kunaweza kuleta maafa makubwa nchini.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana, na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bw. Mohamed Mtulia wakati akitoa tamko la kukemea vurugu za Mkoani Arusha zilizotokea Januari 5, 2011.

Alisema kuwa wamesikitishwa na kauli hizo ambazo zinaashiria matakwa ya kidini katika masuala ya kisiasa, kwa kuwa jambo hilo likiachiwa litaitumbukiza nchi katika machafuko ya kidini.

"Sisi wazee tunawaomba maaskofu na viongozi wengine wote wa kidini kuiacha siasa kwa wanasiasa, kwani kitendo cha maaskofu wa Arusha kukataa kumtambua Meya wa Jiji hilo ambaye pia amekataliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaleta wasiwasi wa kujitokeza viongozi wengine wa kidini na kujipa mamlaka ya kutowatambua viongozi wasiowakubali kama walivyofanya maaskofu hao," alisema Katibu Mtulia.

Alisema kuwa wanaamini kwamba Dkt. Willibrod Slaa aligombea urais katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 na kama angekuwa 'chaguo la Mungu' basi angekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi, na bila shaka asingeridhia Mwenyekiti au Katibu wa chama chochote cha siasa apinge kwa maneno na vitendo, amri halali za mamlaka za kisheria zilizoundwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

"Pamoja na kusikitishwa na nguvu iliyotumika ni wajibu wetu kuitafakari nguvu hiyo na je, ilikuwa lazima itumike au haikuwa lazima, hivi kikundi cha raia kinachoelekea kituo cha polisi kwa ajili ya kuwatoa watuhumiwa kwa nguvu kimedhamilia nini, na je, jamii inafahamu nguvu waliyonayo raia hao na wanaowaunga mkono?" alihoji Bw. Mtulia.

Aidha alisema kuwa  wazee hao wanaamini kuwa endapo uvamizi wa kituo cha polisi ambacho kinawahifadhi watuhumiwa, pamoja na silaha na nyaraka muhimu ungefanikiwa na silaha zikaangukia mikononi mwa raia wa kawaida wasio na nia njema, kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kutumika vibaya na kuleta madhara makubwa.

"Ni dhahiri kuwa waliokusudia kuvamia kituo hicho wangefanikiwa na kupora silaha ili zisaidie kuwatoa watuhumiwa, hali ingekuwa mbaya sana na pia kama angalizo la Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) lingefuatwa, yaliyotokea yasingetokea," alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Athuman Mwinyimvua alisema kuwa wanatoa pole kwa wale wote walioathiriwa na vurugu zile kwa kupoteza mali huku wengine wakipoteza maisha na wale waliojeruhiwa.

53 comments:

  1. Mohamed Mtulia, acha kuongea upuuzi kama huu wakati raia wasio na hatia wameuawa kwa uroho wa madaraka ya viongozi wa CCM. Unaleta dhana y akufikirika kuwa eti CHADEMA walikwenda kuvamia kituo cha polisi ili wapore silaha? Hayo ni mawazo mgando. Halafu kumbuka wewe huna hadhi ya kuwaelekeza maaskofu na mapadre ni nini cha kufanya. Wewe na mashekh wenzako fanyeni yenu ya Koran misikitini, yanayowahusu wa Biblia waachieni wenyewe. Excuse me!

    ReplyDelete
  2. RIP nyie wazee njaa. Majina yote yanaja ulikana ni dini gani? Hivi kwa nini hatuna shule za maana au hospital za maana za kiislam? angalia vyuo vikuu vingapi, huduma ngapi zinazotolewa na waislam. Badala ya kujenga shule, hospital mnajenga misikiti tena barabani!!!! Ujinga muda wenu wa kufikiri umekwisha sanda zinawasubiri. Hivi da ndo kuna wazee?? kazi kunywa kahawa basi. Narudia RIP

    ReplyDelete
  3. hivi hawa niwazee au uchwala msome madarasa hayata wakomboa ukisikia tu jina limeanzia na mzee wa barakashee utajua nipumbu tu zinazo fuata ooo udini hivi hamna hoja wa kristu wangekuwa wadini wangewachagua hawa ndg zenu wanaolipeleke taifa kudidimia kiuchumi mjue kuongoza hamwezi ni jaziba ya udini tu kila kukicha.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli kwa hili serkali ya sisiemu haiwezi kukwepa lawama.wamaona kabisa kuwa kuna tatizo bado wanaendelea kuruhusu chaguzi za namna hiyo kufanyika,wanataka wao tu ndio wawe madarakani hata kama hawakuwekwa na nguvu ya wananchi.kwani uchaguzi ukirudiwa Arusha kwa uangalizi na kufuata sheria zote za uchaguzi na ikaonekana ccm wameshida chadema haiwezi lalamika.lakini kwa uroho wa madaraka wanapindisha sheria na kuonekana wameshinda,pia hembu liwekeni wazi nani anaestahili kupiga kura ktk kumchagua meya wa jiji???mtu mbaya sana anaeharibu amani nchini ni pamoja na Yusufu Makamba,pia hata jeshi la polisi,huyu mama pia mbunge wa tanga aangaliwe pia,

    ReplyDelete
  5. Hawa ndio wazee wanaomshauri Rais na kula mapochopocho ya Ikulu. Wanafikiri TZ ni mali yao. Au wanafikiri wangealikwa kwenda kula maharagwe. Kwa taarifa yenu hakuna maharagwe ni majonzi. Huo udini ni nyinyi mnao kama kawaida yenu, na ndio maana nchi zote zenye waislam ni matatizo matutpu. Kama sio kuwasaidia kwenye Elimu sijui mngefa je. Mnachukua kuvuli cha udini muanze kufunga mabomu kiunoni na kutumia makwanja yenu yaliyoko humo msikitini.

    ReplyDelete
  6. Chadema (Chama Cha Demokrasia na Maandamano) Nyie ndio wa kulaumiwa kwa nini hamkutii amri halali ya kutokuandamana iliyotolewa na IGP>. Nyie ndio mmesababisha mambo yote haya. Namsihi Hakimu awafunge wote walioshutakiwa kwa kutotii sheria miaka 10 kila Mmoja nyie ndio mlisababisha watu wakauawa kama mngeenda tu kwenye mkutano kistaarabu yote hayao yasingetokea lakaini mkaandamana kinyime cha sheria mnataka mfnaye mambo yenu manavyotaka nyinyi ili jumuia ya kimataifa iwaone CCm wabaya nyie ndio wabaya. Haya na hao maaskofu nduguze Slaa hawamtambui Meyawa Arusha ni maajabu wao ni kina nanai au walitaka Slaa awe rais ili nchi iwe ya kikirito hatukubali siye waislamu

    ReplyDelete
  7. pETRO eUSEBIUS mSELEWAJanuary 11, 2011 at 8:50 AM

    Chatandaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaeeeeeeeeeeeeeeee! Ondooooooooooooooooooookaaaaaaaa kwa jina la Yesu!

    ReplyDelete
  8. Huyo mama Chatanda damu iliomwagika imwangukie yeye,na akatubu makosa hayo vinginevyo dhamira itamshtaki,

    ReplyDelete
  9. Chatanda kaombe radhi watakunyang'anya ukristo wako. Kumbuka yaliowafika wakristo wa sumbawanga walioikataa Chadema Kanisa limewafanya nini? Umemsikia Malecela alivyokuita mtovu wa nidhamu.

    Hivi kwa nini chama cha CHADEMA kisifutwe kwa kuubeba udini. Kwa nini Mbowe na Padre Slaa wasijiuzulu kwa kushindwa kuwachunga kondoo zao na kuwasabibishia maafa ambayo yanaepukika.

    Balaa la umasikini la Nchi hii limeletwa na Nyerere. Tuwe w Kweli. Ilifikia watu wanakwenda uchi, wakalazimishwa kula sembe la Yanga, wakakosa hata sabuni ya kuogea na dawa ya meno,tukawa tutanunua chakula kwa kadi na kiwango alichoweka yeye.Maovu matupu. Watu kuwekwa ndani bila ya kufikishwa mahakamani. Ubabe mtupu. Lakini hatawasikia Maaskofu kulaani au kukosoa utawala huwo. Ni Unafiki wa kikatoliki na Udini tu ndio uliotawala nchi hii hivi sasa, Nayote kwa sababu CHADEMA chama cha Maaskofu kimeshindwa uchaguzi na kitaendelea kushindwa maisha. Kwa vile dhamira zao zinajuulikana sasa na kila mpenda amani

    ReplyDelete
  10. Nimependa maoni yoote leo ah. Ntalala kwa raha sana.

    ReplyDelete
  11. sasa nimeelewa kwa nini tunaambiwa viongozi wa dini wasijiingize kwenye siasa. Wakitaka wavue majoho waingie kwenye ulingo.

    Matoeo ni haya hapa.soma wachangiaji.Mgogoro wa Chadema na CCM umekiwa matusi baina ya wakristo na waislamu. Vitone vya matusi aina hii vinaweza kuleta mfarakano usiotegemewa kwenye jamii.

    Na hili limekuja baada ya viongozi wa dini kuanza kuleta chokochoko au kuegemea upande mmoja.

    hatari mti na macho

    ReplyDelete
  12. Hili limekuja baada ya CCM kutaka kwa nguvu kutawala bila kufuata kanuni. Ntu yeyote anao uhuru wa kuhimiza amani; na zaidi sana viongozi wa dini. Maoni ya kuleta amani yasichukuliwe kama maoni ya udini. Udini sasa unaletwa na Chatanda na mashekh wanaojibu maaskofu kana kwamba hawapaswi kukemea maovu ili kudumisha amani nchini. Tunapotoa maoni tufikirie kwa kichwa si kwa tumbo!

    ReplyDelete
  13. HIVI NYIE WAFUASI WA CHADEMA MMEKUWA WEHU? WENGINE WAKITOA MAONI MNAWATUKANA NA KUWAKEBEHI LAKINI MAASKOFU WAKISEMA SAWA,HUO NI UJINGA WA KUPINDUKIA,KAMA MAASKOFU WAKISEMA NI HAKI YAO KUTOA MAONI,KAMA WAISLAMU WA MKOA WA ARUSHA WALISEMA NI HAKI YAO YA KUTOA MAONI NA KAMA HAO WAZEE WA DAR-ES-SALAAM WALISEMA PIA NI HAKI YAO YA KUTOA MAONI,LEO KUNA GAZETI LINASEMA MWANZA KIKUNDI FULANI CHA WATU WANATAKA KIKWETE AJIUZULU NAO NI HAKI YAO KUTOA MAONI,NYIE MKISHA ONA JINA LA KIISLAMU TU TAYARI VICHAA VINAWAPANDA. KOMENI WAACHIENI WENYE MAONI YAO WATOE.

    ReplyDelete
  14. Wewe mbunge wa Arusha unaoongoza kihuni hapo,waeleze watu sheria za nchi zinasemaje kuhusu diwani wa kuteuliwa kutoka katika vyama na haki zake sio kila siku kuleta migongano isiyo na tija kwa jiji letu la Arusha. weka sheria wazi inasemaje? kutuambia tu huyu ni mtu wa Tanga wakati ni katibu wa CCM wa Arusha na anaishi Arusha haitoshi,wewe kwenu ni Moshi na sio Arusha basi nenda kwenu Moshi.

    ReplyDelete
  15. Mary Chatanda ni muislamu? Acha ujuha wewe, watu wanaotoa maoni yao, nao piani haki yao kufanya hivyo. Upo hapo!

    ReplyDelete
  16. MNALOLILETEA MZAHA LEO KWA KUANDIKA UTUMBO KWA KUTAKA MJIFURAHISHE, KESHO LITAWALIZA. NA MTALIA NYOTE BILA KUJALI KUWA WANA CCM AU CHADEMA. NG'ANG'ANIENI TU MADARAKA DAWA YA WOTE SASA IKOJIKONI. NA TUKANENI SANA WACHUNGAJI TENA KWANGUVU ZOTE, CHAMOTO KITAKUJA IKIWA TU NIDHAMU YA NNCHI HAITARUDISHWA NA VIONGOZI WA CCM WENYE UROHO WA MADARAKA. NANYI CHADEMA ACHENI MAMBO HAYA YA KUPIGANIA UKOMBOZI WA MTANZANIA, KWANI KWASASA SI WAKATI WAKE, MTAJICHOSHA BURE NA HAKUNA LITAKALOSAIDIA, MWAJUA FIKA KUWA SERIKALI YA TZ IMOMIKONONI MWA KIKWETE NA AMEMILIKI HATA JESHI LA POLISI NA KWAO SASA KUUWA WATANZANIA WA FUASI WA VYAMA VYA UPINZANI NI KUTAKA WAPANDISHWE VYEO KILA MTU ANAJUA KWA SERA SASA YA CCM NI KUUWA WATANZANIA WASIO WAFUASI WA CCM. CHADEMA TULIENI WAACHIENI CCM WAENDELEE KULA MPAKA WAPASUKE

    ReplyDelete
  17. Kwanini CCM wanaogopa maandano kuliko mahakama? Jibu ni rahisi, mahakama zetu sio huru, anayeteua majaji woooote nchini ni mwenyekiti wao wa CCM taifa, hivyo ni sawa na kesi ya nyani kula mahindi kumpelekea ngedere akaamue. Maandamano yanaogopewa na serikali zote kandamizi duniani, maana ni maandamano pekee nyenye nguvu ya kukusanya watu wanyonge ili waende wakakusanyike pahala ili wajulishwe ukweli halisi wa mambo, matukio na ubaya wa watawala na hatua za kuchukua.

    Kamwe msikimbilie mahakamani, hamtapata kitu huko, kimbilieni maandamano na mikutano ya hadhara sio mahakamani, ona kesi ya mgombea binafsi ya mch. Mtikila ilivyoamuliwa na mahakama ya juu, ona kesi ya Ditopile, ona kesi ya zombe, ona dowans, ona kesi ya mzee wa vijisenti ya kuua, ona, ona, ona,.........

    Ndiyo maana makamba na wenzake hawaishi kusema muende mahakamani ili mkakatwe shigo zenu kwa panga butu ya kijani ya mwenyekiti wao wa CCM.

    Maandamano ndiyo mwiba wa madhalimu, andamaneni hadi mfe wote, sio kwenda mahakamani mtavuliwa huko kwa nyavu zenye rangi ya kijani ndiyo maana wanawasakizia mahakamani. Tuchukue uwamuzi mgumu hata ikididi kupoteza maisha ili kuzikomboa njia kuu za demokrasia na utawala wa sheria ili watu tuishi kwa amani na utulivu wa kweli

    ReplyDelete
  18. Hawa wazee wa Dar siku zote tunawajua, wameshapungukiwa hekima!!! Mawazo yao ni yaleyale ya chama kimoja. Binafsi siwezi kuwashangaaa, ndio hao waliomshangilia Rais wakati anatishia wafanyakazi na kukataa kura zao!!! Sidhani kama leo wanaweza kubadilika na kuwakemea CCM na Serikali yake.

    ReplyDelete
  19. Basi tugawane nchi tupige kura sehemu ipi ya Tanzania iwe serikali ya kiislamu na sehemu gani serikali ya kikristo. Maana mnakazania udini udini kana kwama ni Mgawo wa umeme. ACHENi UPUZI Ninyi nyote mnaoingiza udini kwenye mijadala ni Wapumbavu kabisa.

    ReplyDelete
  20. Mtaji wa CCM ni Ujinga na umasisikini, jinsi ujinga unavyopungua na ndio mwisho wao unavyofika, sisi wenye akili hatuwezi kumisikiliza huyo mtulia mpuuzi atakuwa amepewa hela kidogo ili aongee agange njaa

    ReplyDelete
  21. Jamani sasa watanzania na ukiristo umevuka mpaka.matusi mpaka kwa raisi sasa yanavuka mpaka.ni bora mkawatukana maaskofu wanaoingilia mambo ya siasa badala ya kumtukana raisi.nyie wakiristu mnasema mmesoma kuliko nani?wacheni kujigamba wakati ujui ni chuo gani ambacho wewe umesoma na waislamu atujasoma.huo ni ulimbukeni wa karne tuu.wacheni kujigamba wakati magamba ujaona.

    ReplyDelete
  22. hakuna mwenye hati miliki ya siasa nchini. wnasiasa wanafiki hawapendi kukosolewa hata siku moja. mbona hao maaskofu wakiwasifia hamuiti kuingilia siasa na dini ; wakiwakosoa mnasema dini kuingilia siasa. what is your principle then? mbona mko selective? makamba akitumia biblia kutetea oppression hamusemi anachanganya dini na siasa. what is your principle then? what is dini what is siasa? zote ni platform za kumhudumia mwananchi; zote zina uhuru wa kutoa maoni kukosoa na kushauri; hakuna mwenye hati miliki zaidi ya mwingine. zote ni social tools kwa ajili ya mwanadamu. dhana ya kutochanganya Siasa na Dini inatumiwa kama silaha ya oppressive leaders kuendeleza kuwakandamiza wengine. Viongozi wadini msikubali kufungwa midomo wala kuwa maspika wa oppressive leaders. kwanza, askofu, mwalimu, polisi, mbunge, mwanachama cha siasa au NGO wote wana haki ya kikatiba kutetea maslahi ya mwananchi - hakuna wa kumtukana mwningine. kiongozi akiwa mfano wa kufuata sheria na utaratibu, hatalaumiwa na yeyote. kama sheria hazifai tuzibadilishe kwa demokrasia ya wazi. asijifanye mtu mmoja alizaliwa na label au hati miliki juu ya wengine!! Maskofu na mashehe endeleeni kukosoa wote wanaoleta ukorofi wa kisiasa na kijamii. yote hayo ni mauovu. mwanasiasa anayeona kukoselewa hakufai ajisafishe tu awe safi morally and ethically; no manipulation hapa. tukatae kucheza huo mpira wa kinafiki sasa. kiongozi mbovu akosolewe bila woga. na anayejiona mzuri asimame ajitetee mwenyewe. mtu asiwe laudspeaker ya mtuhumiwa. ukiwa na tuhuma zinakujia jibu, tena kama unajiona msafi jibu tu lakini weka wazi usafi wako, usitukane wanaokukosoa, wala kutumia mtu mwingine kukujibia.

    ReplyDelete
  23. WAKRISTO KUWENI MACHO YALITOKEA EGYPTI YATAWAKUTA. SIMLISIKIA WIKI MBILI ZILIZOPITA WAKRISTO ZAIDI YA ISHIRINI WALIUWAWA KANISANI. MAMBO HAYA MABOMU KIUNONI YANAKUJA. SASA WAMESHTUA IRINGA. HILO NI LA MGAMBO LIMESHALIA.

    ReplyDelete
  24. Namjibu ndugu wa pili juu. Kiongozi wa dini akikosoa taratibu za uchaguzi na maangamzi yalitokea; au ukitoa maoni yake kuhusu mwelekeo unaofaa - hajajiingiza katika siasa. Lakini akisema "hamtambui Meya" basi amejiingiza katika siasa kwa sababu he has taken a political stand. Amechukua msimamo wa kisiasa na hiyo ni kijiingiza katika siasa. Hapo atakuwa open kuhujumiwa kwamba alitumia criteria gani kutomtambua Meya. Ni wazi atakuwa amejitosa katika mgogoro wa siasa kinyume na maadili ya uongozi wa kidini.Narudia: wanahaki ya kusema kwamba chaguzi zifanyike kwa haki na uadilifu. Lakini hawana haki ya kusema fulani kashinda/kashindwa au fulani nina mtambua/simtambui. Their calling (as religious leaders) requires them to steer clear of partisan positions. Wako, Mwendapole

    ReplyDelete
  25. By the way, Maaskofu pia ni raia wa Tanzania, wanaposhiriki siasa ni kama raia wngine, tena wao wanaona mbele zaidi kuliko akina Makamba.

    Makamba anaona leo tu, hajui ya kesho na mtondo. Ndio maana anapofumbua kinywa chake haoni aibu wala hatari ya maneno yake. Hajui hayo maneno yatawaandama watoto wake na wajukuu zake hadi kaburini. Kama ambavyo leo mtu akijitambulisha kuwa yeye ni mjukuu wa Hitler wa ujerumani, wengi watastuka wakisikia ni mjukuu wa Makamba.
    Tusiwe wanafiki, CCM ina udini, na wanautumia kuwatishia wengine ili waogope kuitwa wadini. Hakuna mtanzania asiye na dini. Kama si muislam au mkristo atakuwa na imani ya kimila. Ila watu wanapokwepa kusema ukweli ili wasionekane wadini, wanakuwa waongo.

    Hawa wanaojiita wazee wa DSM hawajui kuwa CCM wamecheza rafu? Acheni unafiki. Hawa ni wazee wa CCM sio wa DSM.

    Viongozi wa serikali wanatakiwa wawatumikie wananchi wote, sio wanaCCM. Haki itendeke kwa watu wote. Hata CCM wangekuwa wanaonewa wangeandamana tu.

    ReplyDelete
  26. WOOOTE NYIE MNAOZUNGUMZIA UDINI NI WAPUMBAVU MSIO NA AKILI. NA NYIE WAKRISTO MNAOJITIA MMESOMA SANA,MBONA MNAJICHANGANYA? SAWA MMESOMA SANA NA MADARAKA YA JUU KWA SEHEMU KUBWA MLIKUWA NAYO NYIE TOKA UHURU,SASA NI NYIENYIE MNAOPIGA KELELE NCHI HAINA MAENDELEO TOKA UHURU,SASA TUWAELEWE VIPI? NI KWAMBA ELIMU YENU MLIOKUWA NAYO HAIKUSAIDIA CHOCHOTE NCHI HII ZAIDI YA KUIANGAMIZA KAMA MNAVYODAI,ACHENI UJINGA WA KUJADILI CCM NA CHADEMA,UCHAGUZI UMEISHA NA RAIS KESHA PATIKANA HAKUNA KURUDI NYUMA,MNADANGANYWA NA HAO WACHAGA,TOKA LINI MCHAGA AKAJALI UHAI WA MTU KWENYE PESA?

    ReplyDelete
  27. Hivi hii hija ya Udini inatoka wapi? Endeleeni kutukanana kuhusu dini zenu na sisi tusiokuwa na dini sijui mtatuweka kwenye kundi gani? Historia itatuhukumu ndugu zangu, DINI hizi tunazo gombania zina wenyewe siye tuliletewa tu ( Hata kama utabisha lakini ukweli ndio huo) toka Uarabuni, ulaya na Asia! Sasa kama unataka kuhakisha hili jaroibu kupekuwa kitabu chako kitakatifu kama utakuta jina lolote lile la kiafrika mfano mbonde, mkumba, shemweta, rweyembiza, mwagito, komba, matonya, mbawala, mwakipesile, sekwao nk, HAKUNA.
    Sasa wewe unayejivunia kuwa dini yangu au yetu kuna jina la baba yako mzazi kwenye hivyo vitabu? Chungeni midomo yenu nyinyi, tunawafundisha nini watoto wetu kuhusu asili yetu? Dini zote ni mapokeo toka kwa mababu zetu hivyo upaswi kutukana au kuisema dini ya mwenzi wako kwa maana babu yako hatujui kwa nini alichagua kuingia kwenye dini hiyo unaiita ya kwako (Labda kwa kuogopa bakora na vitu vingine kama hivyo)! Aaaaakh inakera sana ndugu zangu hamna hata staa? Hivi ina maaana tumekosa vitu vya kujali hata kufikia muafaka bila kuingiza haya masuala ya dini? jadilini hoja ya msingi, ila kwa mtu mvivu wa kufikiri ili kutetea hoja yake lazima ataingiza udini! (Mara ooh hii imesababishwa na dini fulanii.. ya nini yote haya jamani? Eh!)


    Moderator naomba hoja za watu wasioweza kufikiria bila kuingiza udini kwenye hoja kama hizi wasiruhusiwe kuzituma hapa! Hivi huoni kama nafsi yako inakusuta kwa kusema wewe Muafrika kuwa Dini yangu ni fulani tena mbele ya kadamnasi! Ifike mahali sasa tuseme inatosha sio lazima nikufahamu wewe ni dini gani nikishajua Ni MTANZANIA inatosha! DINI DINI UNA DINI WEWE?

    TUJADILI HOJA AMBAZO ZITAKAZO JENGA NA KUSTAWISHA JAMII YETU NA SIO KUTUGOMBANISHA NA KUSHINDWA KUFIKIA MAENDELEO KWA MANUFAA YETU NA VIZAZI VYETU!

    Akhsanteni sana! Nawakirisha!

    ReplyDelete
  28. Ni sawa wanahaki kama raia wengine, lakini waseme wazi kwamba wanazungumza kama raia wa kawaida wala si kama wakuu wa dini. Nadhani umeshawasikia wanasiasa hapa nchini au hata nje wakisema: " Mimi sikusema hayo kwa niaba ya serikali/au chama, ni maoni yangu ya kibinafsi". Ni bora viongozi wa kidini wawe mbali kidogo na siasa kwa sababu wanatusaidia kwani wanasiasa wanawahofu - na hofu hii inatokana na kwamba wanasiasa wanatambua kuwa raia wanawaamini wakuu wa dini kwa kuwa hawapendelei upande wowote. Nguvu yao inatokana na kujikinga na "uchafu" wa siasa. Kwa hivyo, licha ya kwamba wana haki ya kukosoa, lakini wanawajibu wa kujikinga na madai ya kuhusishwa na upande wowote au kuegemea msimamo ulio controversial. Wako, Mwendapole.

    ReplyDelete
  29. Mwendapole mimi ni yule rafiki yako tuliokuwa tunapingana kwa hoja na sio matusi,maadili ya malezi yamepotea,wengine kujifanya wamesoma zaidi ya wengine lakini hapohapo wanajichanganya kusoma kwao kwa kujicontradict wenyewe kwamba hatuna maendeleo leo kwa miaka hamsini ya uhuru,wakati wao wasomi ndio walioshika nchi kwenye madaraka yote ya juu. NAONA WANAJISUTA WENYEWE.Hapa suala la Arusha ni dogo sana lakini wanasiasa wababaishaji ndio wanataka kujipatia umaarufu hapo. SHERIA ZA NCHI ZINASEMAJE KUHUSU DIWANI MTEULE? HAKUNA MMOJA ANAYESEMA ILA WANASHIKILIA ANATOKA TANGA LAKINI WANAKIRI NI KATIBU WA CCM ARUSHA,SASA SISI TULIO MBALI TUNASHINDWA KUELEWA,HUYO MBUNGE WA ARUSHA INAWEZEKANA SI KIONGOZI BALI NI MHAMASISHAJI KWANI UONGOZI HUJA KWA NJIA MBILI ZA MUHIMU KWENYE MAISHA YA BINAADAMU UKIACHILIA MBALI KUPEWA UONGOZI KAMA ZAWADI. 1. KIPAJI CHA KUWA KIONGOZI 2. NI KUSOMEA UONGOZI (bila kununua mitihani au vyeti kama walivyo vijana wengi wa sasa hivi)

    Kingine viongozi wa dini hawana budi kuchunga kauli zao,hatuna budi kukumbuka yaliyotokea Ruanda,hawa viongozi walijikita kutetea uovu na hata baadaye wakashiriki kuua watu juu ya kwamba walikuwa na majoho ya upadre,mimi husomasoma sana matukio,kuna tukio moja lilitokea Rwanda la kusikitisha mno,watu walikimbilia kanisani wakiamini kabisa kuwa ni mahali salama,lakini Padri yule baada ya kuwakaribisha vizuri akaenda akawaita wauwaji wakawateketeza mlemle kanisani,kwa maana hiyo nasema kuwa viongozi wa dini wasjione wako sawa kwa kuona wamevaa majoho au kanzu wakiamini kila wanachotamka ni sawa kumbe ndani ya nyoyo zao wako vingine.

    ReplyDelete
  30. Asante. Yote uliyosema ni ya ukweli. Ingawaje sijui jina lako lakini hufarahia kusoma unayoandika kwa sababu unajadili ukiwa na heshima zako - hata ikiwa wanipinga. Kweli hayo yalitokea Rwanda na pia yalijiri wakati wa vurugu za uchaguzi mkuu mjini Eldoret,Kenya. Wako, Mwendapole

    ReplyDelete
  31. Nani kasema Maaskofu wako mbele? hao ni binaadamu kama binaadamu wengine,na mifano hai ni yale ya kashfa ya kulawiti watoto wadogo huko majuu,mauaji ya Rwanda,sasa huyu utasemaje yuko mbele? hawa ni binaadamu na wana mapungufu yao kama watu wengine na hata hapa Tanzania tunayaona,hapa suala si askofu wala sheikh ila kwa ufinyu wenu wa akili ndio mnayaingiza haya kama vile ni mipango maalum fulani ilyoandaliwa ili malengo yafikiwe.

    ReplyDelete
  32. its better uchaguzi ukarudiwa sheria zote zifuatwe ili apatikane kiongozi atakae leta maendeleo arusha. jaman sio muda wa malumbano arusha is one of the biggest cities in Africa.

    ReplyDelete
  33. Jamani waandishi naomba mnipe msimamo wa kisheria hapa huyu mama chatanda kwa hiari yake alikwenda kugombea ubunge wa viti maalum Tanga ili awawakilishe wanaTanga. Kwa mantiki hiyo aliomba wampe uwakilishi ili awe anahudhuria vikao vya madiwani Tanga kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika kujadili, kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo. Kwa hiyo basi hakutaka kuomba ubunge viti maalum kupitia Arusha kwa sababu zake azijuazo hivyo si mwakilishi wao halali licha ya kuwa katibu wa ccm wa mkoa kwa kipindi kadhaa. Na maana ya ccm kutenga viti maalum kimkoa ilikuwa kutoa fursa ya mikoa kuwakilishwa, nadhani hapa katiba ya ccm inayosema mbunge anakuwa mjumbe wa vikao vya halmashauri etc katika tawi na kata anayoishi imetafsiriwa kuwa sheria ya uchaguzi. Hii kwa hakika si haki. Natambua Chadema ilikuwa na utaratibu tofauti kidogo wa viti maalum, haikuchagua viti maalum kutokana na mikoa bali kutokana na pointi alizopata mgombea kwa mujibu wa vigezo vya elimu, mchango ktk chama, ugombea etc hivyo wabunge wa chadema wa viti maalumu wanaweza kuchagua wapi washiriki katika halmashauri/jiji kutokana na ukazi wao.

    ReplyDelete
  34. Waandishi acheni uvivu fanyeni kazi yenu kwa ukamilifu. Tumemsikia huyu mama Chatanda akitolewa maelezo yanayopingana toka chadema na ccm. Sasa je, sheria inasemaje? Hapa inabidi twende na sheria. Ndipo hapo nyinyi waandishi mnapopaswa kutueleza kuhusu sheria inavyosema badala ya kuendeleza ushabiki toka pande zote. Maana kuna watu hapa wanaongea kutafuta umaarufu. Mara waombe radhi maaskofu n.k. Mimi ni Padre mkatoliki, lakini naomba niseme hivi: Maaskofu wana haki ya kuongoza jamii kwa kukosoa, lakini hili tamko la Arusha linanipa wasi wasi na hawa viongozi wetu. Kila kitu walichokisema ni sahihi lakini pale waliposema hawamtambui meya hapo ndipo walipokosea. Hapa kuna pande mbili zinazovutana. Hawakupaswa kuonyesha wazi wazi kuwa wanasimamia upande mmoja, hata kama wana sababu nzuri ya kufanya hivyo. viongozi wa dini lazima watumie busara sana wakijua wanaongoza watu wote. Haitoshi kusema mama Chatanda ni mbunge wa tanga, lakini je sheria inasemaje? Kwanini chadema wanaogopa mkondo wa sheria badala yake wanakimbilia "Nguvu ya umma." Na ccm je, wako sahini wanaposema mtu anaweza kuwa mbunge wa viti maalumu popote na kuamua kufanyia kazi popote, je, hii ni sahihi? Naomba wataalamu watwambie. Halafu, huko Arusha, kimahesabu ccm ina madiwani 16 na chadema 14. Ukimtoa mama chatanda ccm itakuwa na madiwani 15 na chadema 14, ikimaanisha kura ikipigwa tena bado Meya atatoka ccm. Je, chadema wanaamua kuvuruga kwa kukimbilia nguvu ya umma kwa sababu mahesabu hayawaendei vizuri? Kwenye mauaji, hakuna anayekumbuka maneno ya Slaa akiwaambia wafuasi wa chadema kwenda kuwatoa viongozi wao polisi. Wewe ungekuwa polisi unasikia umati mkubwa unakuja kuvamia kituo ungefanyaje? Kwanza nawapongeza polisi walikufa watu 4 tu. Wazee wameongelea point hii lakini baadhi wamewaponda. Kwa maoni yangu Slaa ana kesi ya kujibu. Slaa anajua kuwa yeye ni kiongozi mwenye ushawishi kwa wafuasi wa chadema na wengineo who have nothing to loose, lakin bado anawaambia waende kuvamia kituo cha polisi. Anapaswa kukamatwa. Naomba tuache ushabiki katika hili, tuangalie kwa kina yaliyotokea na kuwachukulia hatua wote waliosababisha tatizo hili. IGP mwema naye inabidi atueleze kwa kina kwanini aliamua kupiga marufuku maandamano katika dakika za lala salama?

    ReplyDelete
  35. Mary Chatanda anaonewa bureeeee. Kisheria ana haki ya kushiriki katika kikao cha uchaguzi Arusha.Pana ubishi hapo ! Watu wanasahau kwamba alipowaomba maaskofu kuvua majoho, mwanzo alianza kwa kauli nzuri. Alisema anawaheshima ndipo akasema kama wanataka kuingia katika ulingo wa siasa basi wavue... Mzee John Malecela katika siku za nyuma mara nyingi alisema hayo hayo kwa wale ambao mnakumbuka.Pia wenzako katika enzi ya Mwalimu walikariri hayo hayo. Hoja hii ya wakuu wa dini kuvua majoho haikuanzia Tanzania. Ilianza huko Ulaya na hutumiwa hata katika nchi jirani wakati wakuu wa dini wanapojiingiza katika dini. Nauliza, mama kakosa nini? Mama simama kidete, hata Makamba akianza kuyumba. Na wanaokutakia shari: Dua za kuku hazimpati mwewe.

    ReplyDelete
  36. Uchu wa madaraka ndiyo tatizo. Na haki isipotendeka, hapo ndipo mwanzo wa matatizo.Matatizo mengi yamevuma baada ya kutojari haki. Amani haiwezi kupatikana bila haki kutendeka. Amani haiwezi kuptikikana kwa unafiki!

    ReplyDelete
  37. Waswahili wanasema yasikie kwa mwezio lakini yakiingi nyumbani kwako...... Serikali ninajua imetambua ya kuwa askari wake hawajui mbinu ya kupambana na ghasia yeyote inapotokea mahali na kusoma hali inayoendelea kama nia iliyopo ni ya amani au la. Na tushukuru mungu kwamba serikali hairuhusu kila askari kutembea na silaha kama nchi zingine tungesikia kilio kila kukicha.

    Tukiangali hata kwa upande mwingine, mkurugenzi na serikali lazima wabebe lawama kubwa tu. Nikiwa na maana Mkurugenzi angesimamisha uchaguzi baada ya kuona hali ya hewa haisomeki angeomba ushauri serikalini na bungeni limsaidie kuelimisha zaidi madiwani wa upande wa pili waelewe ndipo uchaguzi ufanyike kwa amani. Kama uchaguzi ungesimamishwa mambo yote haya yasingetokea kwa sababu yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu. Ninajiuliza hapa kuna nini mbona sehemu zingine wakurugenzi waliweza kuvumilia mpaka ikapatikana suluhisho na uchaguzi ukafanyika bila lawama hapa palikuwa na nini? Serikali mchunguzeni huyu jamaa atawaharibia, na ataendelea kuichafua serikali.

    Kwa upande wa serikali ni kupuuza haya malalamiko anzia mwanzo, wakati mbunge Lema alipopigwa ilikuwa wakati muafaka wa kutafuta amani kwa pande zote mbili. Sasa waliacha ushabiki ushabiki wa akina Makamba ndio huo sasa leo ni majonzi, ni maombolezo kwa ajili ya ushabiki.


    Mkamba anafurahisha wanaCCM, hawezi kuitolea tamko serikali. Sasa amelala nyumbani akina Mh Membe ndio wanapata shida ya kujibu mabalozi pamoja na taifa kwa ujumla. Serikali itambue haipo madarakani kwa ajili ya ushabiki wa chama kimoja ipo madarakani kwa ajili ya wananchi na kulinda raia kwa pande zote kila anaekosea lazima akosolewe na ambae haelewi lazima aelimishwe. Hakuna mtu ambae ni malaika anaeweza kuwa na kichwa cha kutatua matatizo ya kila mtu bila majadiliano, panapotokea mtafaruku.


    Poleni wafiwa, poleni mliopatwa na matatizo ya kujeruhiwa.

    ReplyDelete
  38. HAPA PANA UJANJA UJANJA TU WA WACHAGA. JIBUNI SWALI, GRACE KIWELU NA LUCY OWENYA NI MADIWANI VITI MAALUM WA KUTEULIWA NA WAMEPIGA KURA HAI,JE WAO NI WAKAZI WA HAI? ACHENI UZANDIKI SEMENI KWELI NA NDIO MAANA HAMTAKI KWENDA MAHAKAMANI MNASEMA MASHITAKA MNAYAPELEKA KWA WANANCHI AMBAO NI LAYMAN KATIKA SHERIA NA YENYEWE YAMEKAA KAMA MAKONDOO NA MBUZI MMOJA AKITANGULIA WANAFATA WOTE,MTAKUFA KAMA MBWA NYIE MNAFIKIRI MCHAGA ANA THAMINI UHAI WA MTU KWENYE PESA? AU HAMJUI STORI ZAO?

    ReplyDelete
  39. Hata magazetini hawa waandishi wana malengo yao kwenye habari hebu soma hapo juu "Mbunge kutoka Tanga" na nyingine hapohapo mwandishi anasema "BI Marry Chitanda ambaye pia ni katibu wa CCM mkoani Arusha" sasa tuelewe vipi?

    ReplyDelete
  40. Ni sheria ndiyo inaruhusu. Wasema Mary kavunja sheria? Mbona kabla ya kura Chadema haikumkataa awepo kwenye kikao cha uchaguzi? Wabunge wa Chadema waitumia sheria/ruksa hiyo hiyo kwa upana zaidi. Ndiyo maana hawathubutu kwenda mahakamani. Mbiyo za sakafuni huishia ukingoni.Na wale wanachochea mapigano,damu kumwagika na "nguvu za umma" wanafaa wafunguliwe mashtaka. Hawa wameshindwa katika uchaguzi - Watanzania wamewakana, sasa ujanja tufanye ghasia na tutumie dini.Lazima serikali ichukue hatua kali ili kuwalinda Watanzania wapenda amani. Ah,tumechoka.

    ReplyDelete
  41. Hapo juu nilimesema waandishi waache kunadika kwa ushabiki na kuwataka watwambie sheria inasmaje. Msajili wa vyama amenisaidia na nafikiri maelezo haya yatawasaidia nyote hapo juu mnaotoa shutuma bila kujua sheria inasemaje. Habari hii nimeitoa katika gazeti la Mwananchi. “Nadhani Chadema hawako wazi katika hili, kwani uhalali wa Mary Chatanda lilishatolewa ufafanuzi na katibu wa Bunge. Sheria iko wazi na ilifafanuliwa na katibu wa bunge baada ya madiwani wa pande zote mbili kuonyesha utata walipokuwa katika kikao cha kwanza cha uchaguzi wa Meya, ambapo vyama vyote viwili vilikuwa vikilalamikia ushiriki wa mjumbe mmoja mmoja kutoka kila chama”. Anasema ufafanuzi walioupata juu ya uhalali wa wabunge hao wa viti maalum waliokuwa wakilalamikiwa na vyama vyote viwili ni kwamba, sheria inawatambua wabunge kama madiwani wa sehemu wanazotoka na inaendelea kufafanua chama kinachowakilishwa na mbunge wa viti maalum, kitakuwa na haki ya kumpangia kazi sehemu yoyote isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi katika eneo lingine. Anasema baada ya ufafanuzi huo utata wa suala la uwakilishi wa mbunge huyo wa viti maalum ukawa umemalizika na kwamba haelewi sababu za Chadema kususa kuendelea na uchaguzi wa Meya na kushangazwa na chama hicho kukwepa kueleza wafuasi wake suala hilo huku ikiendelea kushikilia msimamo wa kutomtambua mbunge huyo wa viti maalum wa CCM.Haijulikani hasa wanataka nini, maana kama ni kweli ilikuwa uhalali wa Mary Chatanda walishasomewa sheria na wakaelewa. Awali walizungumzia suala la kutaka katiba, kila mtu aliunga mimi nimeunga mkono nimetoa maoni yangu, Waziri mkuu naye kasema, na mwisho rais ameridhia, sasa waeleze wanataka nini ili madai yao yawe wazi na yaeleweke,” anasema. Msajili anasema inavyoonekana, ndani ya chama hicho, wapo baadhi ya viongozi wanataka kudanganya wananchi na kuficha kuwaeleza ukweli na akasema ni vyema kwa vyama vya siasa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

    Naomba mnaowatetea maaskofu mfikirie mara mbili. Wamekosea wamekosea wamekosea. Period. Chadema wanajua sheria lakini wanafanya mambo kwa maksudi kabisa. Lengo ni kuvuruga nchi kuhakikisha Kikwete hawezi kutawala nchi. Huu ni ubinafsi na hawana uchungu wowote na nchi yetu kama wanavyosema. Chadema lazima wachukuwe lawama zote kwa yaliyotokea Arusha. Wanapaswa kuwajibishwa. Slaa amefanya uhani kwa kuwatuma watu kwenda polisi kuwatoa viongozi huku akijua sheria inasemaje kama mtu akikamatwa. Hii ligha ya nguvu ya umma inakera sana. Wanasahau hata vyama vingine vina wafuasi hata kuwazidi, sasa nao wakiamua kuja mitaani Tanzania itakalika? Nyie wote mnaoshabikia haya matendo ya chadema mtakuja kujuta.

    ReplyDelete
  42. Hata mjitafune imeshakula kwenu. Mnalo na mtalinywa. Huyo Chatanda wenu arudi kwao, hatumtaki wampeleke huko huko Tanga alikopangiwa na chama chake. Chama chake kiliona umuhimu wake huko Tanga ndio maana wakampeleka huko hakija kosea.

    Sasa kama msajili alikuwa analijua hilo anzia mwanzo kwa nini asinge waita na kuwakalisha kuwaelimisha pale palipokuwa na tatizo. Au angeitisha mkutano wa waandishi wa habari kuelezea hii sheria ijulikane. Kwa kweli ni mara ya kwanza tunaisikia hii sheria hapa Tz miaka yote ilikuwa imefichwa wapi. Chadema muundo wao unaeleweka hizo vululu vululu zenu CCM hazieleweki, hata ukimwelimisha mtu ambae haelewi hatakuelewa. Na kwa muundo huu ni vurugu tu ingekuwa chama kimojo sawa lakini kulivyo na vyama vingi lazima italeta matatizo kwa jamii.

    Ninacho wasifu chama cha CHADEMA hata wanachama wao hawapayuki payuki kama CCM, hawana ubinafsi kama hawa wengine.Oh mara mchaga oh mara maaskofu oh mara udini oh mara kafiri nk. Lakini huyu mchaga hutamsikia wanasungumzia kabila fulani au dini fulani ni wao na maisha ya watanzania bila kubagua.


    Chungeni sana midomo yenu inamaana hawa sio watanzania kama nyinyi, sasa huyu mchaga mnaemwandama yuko Dawans, yuko TTCL, yuko Reli, huko kote hamuoni mafisadi bado mnamgandamiza huyu mchaga. Na mkiendelea na hali hii ya kuchukua chambo fulani kwa jamii fulani mtakujafikia muafaka wa sudani kusini. Mimi japo sio mchaga lakini nimeishi nao na ninawajua na ndio maana kimeniuma.

    ReplyDelete
  43. Wewe hapa jibu hoja,umeambiwa sheria inasemaje na mimi naongezea wale wabunge wa kuteuliwa waliopiga kura Hai walichaguliwa pale au mkoa wa kilimanjaro.nyie ni makondoo tu,jibu hoja unaleta ya TTCL,RELI na DOWANS usiruke mada ukitaka ya dowans yaanzishe,hapa tunasema Mary Chitanda ni Mtanzania ana haki ya kuishi popote katika nchi hii kwani huyo mbunge wenu mhuni Lymo kwao ni Arusha aondoke aende kwao Moshi,majina ya Kiarusha ni kina Mollel,Ole Sululu.sokoine na wengineo.Huyo mchaga hagandamizwi kama unavyosema ni mchaga kwao ni Moshi sio Arusha,ni muhuni asiyejua kitu na mpenda sifa. CCM MKIWAKUBALIA CHADEMA KITU AMBACHO SHERIA IKO WAZI MJITAYARISHE NA MADAI MENGINE MAPYA

    ReplyDelete
  44. Mnawatukana wazee wa Dsm bure tuu,jibuni hoja. Wabunge wawili wa viti maalum wa chadema waliopiga kura Hai Bi Grace Na Lucy walichaguliwa Mkoa wa Kilimanjaro? au ni wakazi wa Hai? hapo kuna mchezo unachezwa na CCM kaeni sawa hao matajiri wa Kichaga Arusha watanunua diwani wenu kufanikisha lengo lao.msikubali uchaguzi urudiwe bila sheria kufafanuliwa,hata kauli ya maaskofu inashangaza ati kwa kusema Chitanda ni mbunge wa Tanga sasa nyie Maaskofu msio na haya wala aibu tuambieni hao wa Hai ni wabunge wa Kilimanjaro au Hai? msituletee mambo ya Ruanda na Kenya hapa maana mmehusika moja kwa moja na kadhia ya mauaji yaliyotokea huko.

    ReplyDelete
  45. "NINAWAAMBIA POLISI WAWAACHIE VIONGOZI WETU VINGINEVYO NITAWAACHIA WAFUASI WANGU WAAMUE NINI CHA KUFANYA,NA MIMI NISILAUMIWE KWA WATAKACHOKIFANYA" Hii ni kauli ya Padri Slaa akiwaambia wafuasi wake. " NA SASA WOTE TWENDENI KITUO CHA POLISI" anamalizia Padri Slaa. TWENDENI HUKO KWA OCAMPO MKAONE KULE SI MAHAKAMA ZA KWETU WANAMUANGALIA MHALIFU. PADRI SLAA NA KUNDI LAKE LA WACHAGA WOTE HUKO MNALO SHITAKA LA KUJIBU NA MSIFIKIRIE HUKO NI KWA VIONGOZI WA SERKALI TU NA WACHOCHEZI PIA.

    ReplyDelete
  46. KWELI HUYO UNAEISHI NAE ANAPATA SHIDA KWELI, NINAMPA POLE SANA, MPAKA UNAMPIGA MWANDISHI MAKOFI ALIKUKOSEA NINI, SASA IMEBAKIA KUWA CHIZI. TUMESHA SEMA CHITANDA ONDOKA HATUKUHITAJIIIII. WAFUATE MASHEHE WAKO HUKO PANGANI. HATA UREMBUE ARUSHA HUKAI. SHEHE.

    ReplyDelete
  47. WEWE MBWA NA NGURUWE MMOJA UKOME MSIKITI WA PANGANI

    ReplyDelete
  48. MSIJIFANYE HAMJUI. ISHU SIO MTU ANAISHI WAPI JAMANI. ISHU NI KUWA KAMA WEWE NI MBUNGE WA VITI MAALLUMU KWA KUPITIA DIRISHA LA MKOA FULANI BASI UTAKUWA DIWANI KATIKA MKOA HUO. TA TARATIBU ZINARUHUSU WABUNGE WA MKOA X KUPIGA KRA KAMA MADIWANI KATIKA MKOA X NA SIYO Y. KAMA MARY NI MBUNGE WA VITI MAALUMU KWA MKOA X BASI ATAPIGIA KRA ZA KIDIWANI KWENYE MKOA X. KAMA LUCY NI MBUNGE WA VITI MAALUMU KWA MKOA Y BASI ATAPIGIA KURA ZA KIDIWAI KWA MKOA Y. HIVI NDIVYO TATARATIBU ZAO TAMISEMI ZINAVYOELEKEA KUSEMA. UNIT OF REFERENCE NI MOA NA SIO HALMASHAURI. LAKINI KUNA WATU WANAPINDISHA MAMBO KILA LEO KUJINUFAISHA. SASA NI NANI KAPINDISHA MARY AU LUCY? CCM AU CHADEMA? NANI KAHAMIA MKOA AMBAO KIUBUNGE SIO MKOA WAKE? SWALA SI NANI KAZALIWA WAPI AU AMEKULIA WAPI AU KAOA AU KUOLEWA WAPI??

    ReplyDelete
  49. Hujajibu swali bado unapindishapindisha tu,Mary na Lucy ni wabunge wateule wa mkoa upi? ok Chitanda ni mkoa wa Tanga,je hawa wawili? nenda Chadema waulize viti maalum wanateua vipi? au hukusikia migogoro wakati wa kuteua viti maalum.

    ReplyDelete
  50. MIMI NAONA TUANZISHE VITA VYA KIDINI ILI TUWE NA NIDHAMU KIDOGO

    ReplyDelete
  51. TUANZE KUCHAMBUA SAFU YA UONGOZI ILI TUONE UDINI UKOWAPI.
    . RAIS WA JAMHURI - JAKAYA M. KIKWETE
    . MAKAMU WA RAIS - DR. GHARIB BILALI
    . RAIS WA ZANZIBAR - DR. ALLY M. SHEIN
    . MAKAMU WA I WA RAIS -MAALIM SEIF SHARIF HAMAD
    . MAKAMU WA PILI WA RAIS-BALOZI SEIF
    . IGP - SAID MWEMA
    . WAZIRI WA FEDHA - MUSTAPHA MKULO
    . WAZIRI WA MAMBO YA NDANI- SHAMS VUAI NAHODHA
    . NAIBU WAKE - HAMIS KAGASHEKI
    . M/KITI WA CHAMA TAWALA - JAKAYA KIKWETE
    . KATIBU MKUU CCM - YUSUSPHU MAKAMBA.
    KWA UCHACHE TU HIZO IDARA NYETI ZINAZOWEZA KUDHIBITI MAMBO YOTE KATIKA NCHI HII NA KANCHI KETU KADOGO KA ZENJI HALAFU LEO HII WATU HAO WANAUZUNGUMZA UDINI. HIVI KWA MFANO KARATA JUU KARATA FUNIKA INGEKUA SAFU HIYO NI WAKRISTO INGEKUAJE KWA HAWA HAWA WANAOUZUNGUMZA UDINI??
    HEBU BAADA YA KIKWETE ANAYEFUATA AWE MKRISTO NA MAKAMU WAKE MUONE NGOMA ITAKAVYORINDIMA.
    HEBU WAISLAM TUACHE KUCHOKOZA MAMBO AMBAYO MIFANO HAI TUNAYO NA DHAMIRA INATUSUTA.TUANGALIE NI KWANAMNA GANI TUTAIJENGA NCHI KWA MASLAHI YA WOTE.HAO VIONGOZI WETU NI WENGI WAMESOMA SHULE ZA DINI HIZOHIZO NA KUFIKA HAPO WANAPO PAONGELEA LEO KAMA UDINI. NIWATOTO WANGAPI WAKIISLAM AMBAO KWA LEO WANASOMA SHULE ZA MADHEHEBU YA KIKRISTO BILA KUBAGULIWA.
    TUKOME NA TUACHE MAMBO YA UCHOCHEZI

    ReplyDelete
  52. Wewe mama Chitanda sijui nimekosea jina au ni mama kitanda . Jaribu kuwa na haya usoni. heshimu aliyo yasema Mzee Malechela.Acha kung'ang'ania Arusha nenda huko Tanga kipigie kura huko. Laiti ungekua mke wangu kwa hili ningekulamba Talaka.
    Kumwagika kwa damu kunatokana na wewe. huwezi kukwepa dhana ya kumwaga damu. duniani utaonekana shujaa lakini kwa Mungu huna nafasi.

    ReplyDelete