tag:blogger.com,1999:blog-1185314680614945258.post8171052431194905993..comments2024-03-02T21:58:22.701+03:00Comments on MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Kinachoibua vita baridi Tanzania na MalawiHallhttp://www.blogger.com/profile/10857587611357173970noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-1185314680614945258.post-4276935758490802442012-08-10T05:21:03.788+03:002012-08-10T05:21:03.788+03:00Napenda kumshukuru Mungu aliyaepusha haya yote isi...Napenda kumshukuru Mungu aliyaepusha haya yote isiwepo vita tangu nchi zote mbili zilipopata Uhuru Tanzania 1961 na Malawi 1962

Tukisoma kwa makini taarifa hizi za viongozi wetu waliopita utaona kuwa pamoja na kuvutana kwao walifikia wakati wakawa wamoja wakatoa sauti moja ya kuwa waacheni Wamalawi na Watanzania waogelee kwenye ziwa Malawi/Nyasa kama linavyojulikana.

Lakini kinachoonekana sasa ni kama cheche za moto zilizotupwa kwenye majani makavu. Cheche hizo siyo nyingine ila ni utafutaji wa mafuta na gesi katika ziwa hili na makampuni haya ya nje.

Kwa mtizamo wangu kila mahali ambapo kuna mafuta au gesi ambayo ndiyo chanzo cha mafuta na kunakuwepo na harufu ya vita,

Nitoe mfano nikianzia na nchi yetu Tanzania , tumeshughudia baada ya kuwepo na dalili za kuwepo na mafuta huko Zanzibar harufu iliyopo ni kuvunja muungano na Wanzanzibari wanatakata eneo la mafuta na gesi waachiwe wenyewe.

Tumekaa nao kwa amani kwa miaka hiyo hamsini tangu nchi ilipopata Uhuru wake lakini baada ya cheche hizo za mafuta na gesi ugovi unafuka maelewano yaliyokuwepo kwenye muungano yanatoweka wanataka hata katiba irekebishwe na swala hili la mafuta na gesi lisiwe la muungano
Na kama hilo litakubalika basi cheche hizo zinaweza kuwashwa na mataifa ya mashariki na magharibi kwa ajili ya mafuta hayo

Twende Sudani watu wengi wamekufa eneo la kusini kwenye wakristo wengi na kwenye mafuta hadi umoja wa mataifa ukaona ni vyema kugawa nchi hiyo kuwa mbili Sudani ya kaskazini na Sudani ya kusini

Ni hivi majuzi tu hali ya kivita ilitaka kuanza baada ya Sudani ya ksakazini kudai eneo lenye mafuta kutoka sudani ya kusini lakini Mungu akaepusha vita hivyo tulisikia hata waziri wa mambo ya nje wa Marekani alisuluhisha mgogoro huo

Twende Libya mapigano yalikuwepo chanzo kikubwa ni mafuta

Sasa turudi Tanzania tulisha mwaga damu ya kutosha kule Uganda , hatutaki kumwaga tena damu sii Zanzibar wala Malawi .Hekima alizoachiwa Raisi Kikwete na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipoyapuuza haya yote ya Kamuzu Banda na mwenzake Mutharika ni vema aedelee kuzitumia kulinda nchi yetu.

Nasema kulinda nchi, siyo lazima nchi ilindwe kwa vita ona Syria ni watu wangapi anakufa bila hatia kila siku, maneno mazuri yanaweza kuilinda nchi kama uemi unaosema maneno mazuri hutoa nyoka pangoni,

Jumuiya za kimataifa , mahakama zinaweza kabisa kuamua mgogoro huu kwa amani kabla ya ukamilishaji wa utafutaji wa mafuta na gesi kufanyika.

Kama ilivyozungumzwa kuhusu mgogoro huko Chadi na kuamuliwa kwa amani basi hata sisi tunaweza kufuata mkondo huo.

Ni matumaini yetu kuwa Amani iliyokuwepo itaendelea kuwepo badala ya kuvurugwa na wachache wanaotafutafuta kujitajirisha wenyewe kwa haraka

Mungu endelea kuwapa viongozi wetu subira na wawe na upendo wa kweli kwa watu wao.Endelea kuzibariki Tanzania na Malawi waendelee kuogelea pamoja kwenye ziwa Malawi /Nyasalcshttps://www.blogger.com/profile/10852352736159901885noreply@blogger.com