30 August 2013

MTIHANI KWA POLISI:MATAPELI STENDI YA MABASI UBUNGO

  • WAJIFANYA USALAM WA TAIFA,POLISI,UHAMIAJI
  • WADAIWA KUTOA VIZA KWA WAGENI SH.20,000
 Baadhi ya matapeli wakiwa wanajipanga kwa ajili ya kumtapeli mwanamke ambaye hakufahamika jina (aliyejifunga ushungi) akitokea mkoani Kigoma na kushuka Dar es Salaam juzi katika basi la Adventure.

 Mmoja wa matapeli ambaye hutumika kama dereva teksi isiyo rasmi
Na Waandishi Wetu
HALI si shwari ndani ya kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT), Dar es Salaam, kutokana na utapeli mkubwa unaowafanywa na watu wanaojifanya waajiriwa wa Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na Uhamiaji.Utapeli huo unafanywa kwa abiria wanaoingia jijini humo, wakitokea mikoa ya mbali kama Kigoma, Bukoba na nchi jirani za Kenya, Uganda, Bunjumbura na Malawi

ASKOFU KULOLA AFARIKI DUNIA



 Na Mwandishi Wetu
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God nchini (EAGT), Dkt. Moses Kulola (83), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.Taarifa zilizolifikia gazeti hili, zinasema Askofu Kulola amefariki jana saa sita mchana katika Hospitali ya Army, iliyopo Msasani, Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa.

MAMILIONI YAPORWA DAR



  •  MAJAMBAZI WAITEKA BENKI,WENGINE WATEKA MAGARI,WAUA DEREVA
 Na Waandishi Wetu

MAJAMB AZIweny e sila ha,janawalivamiaOfisizaBenkiyaHabibLTD, iliyok oKar ia koo , MtaawaLivingtone-Uhuru,DaresS alaamnakupo ra d olazaMare kan i181,8 85pa mojanama mi lioniyaf edhaza Tanzaniaambazo thamani yake haijafaham ika.

ASKARI JWTZ AUWAWA GOMA



Na Rehema Mohamed
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Khatibu Mshindo, ambaye ni miongoni mwa wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani Mjini Goma, nchini Kongo (DRC), ameuawa baada ya kuangukiwa na bomu.

TRA YAANZA KUTUMIA MFUMO MPYA BANDARI



Na Ester Maongezi
MAMLAKA ya Mapato Ta n z a n i a ( T R A ) imesema kuanzia sasa itakuwa inapokea taarifa moja kwa moja kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania juu ya mizigo inayoingia na kutoka ili kuondoa tatizo la udanganyifu uliokuwa ukifanywa na wafanyabiashara na watendaji. Hatua hiyo inalenga ukwepaji ulipaji kodi

LHRC YATOA MAPENDEKEZO RASIMU YA KATIBA



Na Leah Daudi
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimewasilisha maoni yake ya katiba mpya ambapo kimependekeza kushika wadhifa huo kwa vipindi vitatu vya kukaa. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurungenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Helen -Kijo Bisimba, alisema kituo kimechambua vifungu vyote na kuainisha masuala mbalimbali ambayo yanahitajika kurekebishwa.

MAOMBI YA RUFAA DHIDI YA ZOMBE WIKI IJAYO



 Na Rachel Balama
WAPINGA rufaa katika k e s i y a ma u a j i y a w a f a n y a b i a s h a r a iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na askari wenzake wanane walioachiwa huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wameiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kupewa muda ili kuwasilisha majibu ya maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya kuongezewa muda wa kukata rufaa.

KESI YA EPA YAKWAMA



Na Rehema Mohamed
UPANDE wa Mashtaka katika kesi ya kughushi na wizi wa zaidi ya sh.milioni 400 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) imekwama kusikilizwa kutokana na jopo linalosikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani.

WAFUNGWA WARUHUSIWE TENDO LA NDOA KATIBA MPYA



Na Yusuph Mussa, Korogwe
BAADHI ya wadau wa masuala ya jinsia wamependekeza kuwa ili kukabiliana na masuala ya ushoga na usagaji, Katiba Mpya iruhusu wafungwa kukutana kimwili na wenza wao, kwani vitendo hivyo chanzo chake ni gerezani hasa kwa vijana wanaokula 'unga' na kuvuta bangi.

MATATANI AKITUHUMIWA KUMUUA MUMEWE



Na Abdallah Amiri, Igunga
JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora jana lilimfikisha mahakamani, Msua Malanda (37), mkazi wa kijiji cha Segerei, Kata ya Igoweko wilayani Igunga kwa kosa la kumpiga mumewe chupa kichwani na kusababisha kifo chake.

TPAWU YAPINGA KIMA CHA MSHAHARA



 Na Rehema Maigala
MW E N Y E K I T I wa Kama t i y a W a n a w a k e mashambani na Kilimo (TPAWU), Patricia K i s h i m b a a m e s e m a hawakuridhishwa na kima cha chini cha mshahara kilichotangazwa na Serikali sh 100,000

BRANDTS AMTUPIA LAWAMA MWAMUZI

  • UONGOZI 'WAANGUA KILIO' TFF


 Na Elizabeth Mayemba
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts amemtupia lawama mwamuzi wa mechi Ligi Kuu kati ya timu yake na Coastal Union juzi, Martin Saanya kwa kushindwa kumudu mchezo huo na kutoa maamuzi yenye utata.

CHEKA,WILLIAMS KUDUNDANA LEO



 Na Fatuma Rashid
MABONDIA Phil Wiliums wa Marekani na Francis Cheka, wamepima uzito kwa ajili ya pambano lao la ngumi la ubingwa wa WBF la uzito wa kati linalotarajiwa kufanyika leo, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

RAGE AIRUDISHA SIMBA DAR KUCHEZA NA MAFUNZO



 Na Elizabeth Mayemba
MWENYEKITI wa klabu ya Simba Aden Rage ameamuru timu hiyo irudi Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na Mafunzo ya Zanzibar itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa lengo la kuwatambulisha wachezaji wao kutoka Burundi

29 August 2013

SAKATA DAWA ZA KULEVYA:UPEKUZI MKALI KWA VIONGOZI



  •  NI WA SERIKALI WANAOKWENDA NJE YA NCHI
  • NI KUTOKANA NA TANZANIA KUGEUKA UCHOCHORO
  • SERIKALI YAGOMA KUTAJA MAJINA YA WAHUSIKA

Na Waandishi Wetu
SIKU chache baada ya Tanzania hasa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kugeuka uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya kutoka na kuingia nchini, hali hiyo imesababisha viongozi na watu mashuhuri nchini kufanyiwa upekuzi mkali wanapofika kwenye viwanja mbalimbali vya ndege nje ya nchi

AJALI YAUA 13

  • WENGINE 11 HOI,WAVUNJIKA MIKONO,NYONGA


Suleiman Abeid, Shinyanga na Faida Muyumba, Geita
WATU 13 wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea saa 2.30 usiku wa kuamkia jana baada ya gari dogo aina ya Hiace kugonga kwa nyuma gari aina ya Scania lililokuwa limeharibika na kuegeshwa pembeni mwa barabara.

MWIGULU AMVAA MBOWE,DKT. SLAA



 Goodluck Hongo na Hytham Mushi
SIKU mbili tangu kuanza kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, ameanza kuwasha 'moto' bungeni kwa kuhoji sababu za Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dkt. Willbrod Slaa, kuendelea kuwa huru, wakati wanastahili kuwa jela kwa kusababisha mauaji ya raia.

TIMUATIMUA YAKWAMA TAZARA



 Anneth Kagenda na Salma Mzee

TARATIBU za kuanza kuwakabidhi barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi wa Idara ya Karakana na Ujenzi katika Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA), uliokuwa uanze jana, umekwama kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja

MAKATIBU CCM KIKAANGONI



 Na Thomas Mtinge, Dodoma
MAKATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ngazi ya mikoa na wilaya nchini wameagizwa fedha zilizowekwa kwenye benki ya CRDB kwa ajili ya kuanzisha Family Benki, zirudishwe mara moja vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

POLISI KUSHIRIKIANA NA WATAALAMU WA MAJENGO



 Na Gladness Mboma
JESHI la Polisi nchini limesema liko tayari muda wowote kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Ujenzi (AQRB) ili kuhakikisha ujenzi wa majengo yote nchini unashirikisha wabunifu majengo.

BILIONI 4/- KUTUMIKA UJENZI WA CHUO KASULU



Na Respice Swetu, Kasulu
ZAIDI ya sh. bilioni nne zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Nyamidaho kinachojengwa katika Tarafa ya Makere wilayani Kasulu Mkoa wa Kigoma.

TBS WARUHUSU MAFUTA YA OKI



Na Grace Ndossa
SHIRIKA la Viwango nchini (TBS) limesema mafuta ya kula aina ya OKi yanaruhusiwa kusambazwa kwenye soko la ndani baada ya kubainika hayana madhara. Uamuzi huo unatolewa zikiwa zimepita siku kadhaa, TBS kutangaza kwa umma kuwa mafuta hayo ambayo yanazalishwa nchini Malaysia hayafai kwa matumizi ya binadamu.

MULUGO KUFUNGUA MAONESHO VODACOM ELIMU EXPO



Na Rose Itono
NAI BUWazir i waElimunaMa funzoya U fundi Bw.Philipo M ulugo jana amefunguamaoneshoyakwanza yawadauwa elimuyal iyopewajina la Voda comElimu Expo.Taarifa iliyotolewa kwa vyom bovyahabariDar esSalaamjanana Mk urugen zi wa Elimu Soluti ons,JoelNjam ainasema kuwa,maonesho hayaya tafanyikakwamar ayakwan zanch inina kwa mbay ata anzaras mikes honak umalizi kaSeptem ba m wakahu ukatikavi wanjavyaPosta Kijitonyama

'KAMPUNI ZINAZOSAIDIA WAKULIMA ZIPUNGUZIWE KODI'



 Na Grace Ndossa
SERIKALIi meshauriwakuzipunguzi akodi kampuni mbalimba lizinazowasaidiawakulimaili waweze kulima mazao mengizaidi.Piaw ameta kiwakuwapunguzia ushuru wak ulimawana popelekamazaoyaosoko ni iliwaweze kunufaik a nakilimokwakupatamapatoyatak ayokid hi m ahitaji yao.

WAFANYABISHARA KARIAKOO WALIA ONGEZEKO LA KODI



JUMUIYA yaWafan yabiashara Kariakoo (J WK),imesemakuwawafanyab iash arawa ke wanak abiliwa nakerokub wayaongezekolako dihukuk ukiwana mazingira ha baya kipat okutoka nanawin giwamac hingaambaoser ikaliime shin dwakukabili ana nao, anaripoti Mariam Mziwanda.

WATUMISHI WA UMMA KUSHUGHULIKIWA



 Na Yusuph Mussa, Lushoto
MK U U w a Wi l a y a y a Lu s h o t o , Al h a j j M a j i d M w a n g a amesema ataendelea kuwashughulikia watendaji wa kata na vijiji wanaodharau utawala wake kwa kusema kwa sasa Jimbo la Bumbuli halina Mkuu wa Wilaya hivyo kukataa kutii maagizo yake.

RIPOTI YABAINI UKATILI WA KUTISHA NCHINI



 Na Pendo Mtibuche, Dodoma
RIPOTI ya utafiti wa hali ya ukatili nchini kwa kipindi cha mwaka 2010 inaonyesha kuwa theluthi moja ya wanawake wote Tanzania wameathirika kwa namna moja au nyingne na ukatili wa kijinsia tangu wakiwa na umri wa miaka 15.Hali hiyo pia inaonyesha kuwa wanawake hao hao pia wameathirika na vitendo vya ukatili katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo y

YANGA YAKWAA KISIKI SIMBA SC YATAKATA



 Na Elizabeth Mayemba
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana wamekwaa kisiki baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo, Yanga iliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu Ashanti United.

RAIS WBF ATOA NENO PAMBANO LA CHEKA



Na Fatuma Rashid
SHIRIKISHO la Kimataifa la Ngumi za Kulipwa (WBF), limeshukuru Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBO kwa kufanikisha pambano la ngumi la kimataifa uzito wa kati.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kumtambulisha bondia Phil Wiliums kutoka marekani Rais wa WBF, Howard Goldberg alisema pambano hilo litasaidia kukuza mchezo wa ngumi hapa nchini

GRAND MALT YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR



 Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KINYWAJI kisicho na kilevi cha Grand Malt, ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu kama 'Grand Malt Premier League' jana wamekabidhi vifaa kwa timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Bwawani, mjini hapa.

28 August 2013

UKWELI NA UWAZI : WALIONASWA NA 'UNGA' WATAJWA

  • WAPO WATANZANIA,RAIA WA MATAIFA MENGINE

 Na Mwandishi Wetu
WAKATI Serikali ikiendelea k u u s a k a m t a n d a o unaofanya biashara ya dawa za kulevya nchini, Jeshi la Polisi Kitengo cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, limekiri kuwanasa zaidi ya watu 100 waliokuwa na dawa za kulevya na kesi zao zinaendelea mahakamani.

MADIWANI BUKOBA SASA KICHEKO



Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), imetoa maamuzi juu ya sakata la madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri kuu ya chama hicho mkoani Kagera hivi karibuni.
Katika maamuzi yake, Kamati Ku u ime b a t i l i s h a u amu z i uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM, mkoani humo Agosti 13 mwaka huu wa kuwafukuza uanachama madiwani hao

POLISI MBARONI KWA UJAMBAZI DAR

  • ALIKUWA NA WENZAKE WAPORA DOLA 20,000

 Na Masau Bwire

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala, linawashikilia watu wanne akiwemo askari wake mmoja kwa tuhuma za kufanya ujambazi kwa kutumia silaha (bastola) na kupora dola za Marekani 20,000, sawa na sh. milioni 32 za Tanzania.

WAKAZI KAGERA KUKOSA UMEME KWA WIKI 40



Na Livinus Feruzi, Bukoba
MATENGENEZO ya uboreshaji njia kuu za kusafirisha umeme yanayotarajiwa kufanywa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kutoka Masaka nchini Uganda hadi Mutukula nchini Tanzania, yatasababisha Wilaya tatu za Mkoa wa Kagera kukosa huduma ya umeme kwa wiki 40.

MGOMO WA WAFANYAKAZI TAZARA HALI TETE



 Anneth Kagenda na Salma Mzee
WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), wamesema kama Serikali italazimisha treni hiyo iendelee na safari zake, wasilaumiwe kwa lolote ambalo linaweza kutokea kwa abiria wanaosafiri

KURASINI WAFUNGA BARABARA KUSHINIKIZA KULIPWA HUNDI


Baadhi ya wakazi wa Mivinjeni Kurasini wakiwa na bango kando ya Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam jana, lenye ujumbe wa malalamiko ya kudai kulipwa hundi za fidia ili kupisha mradi wa ujenzi wa bandari kavu kwenye eneo hilo.

 Na Waandishi Wetu

WAKAZI wa Mivinjeni Kata ya Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam wanaotakiwa kuhama makazi yao ili kupisha mradi wa Mamlaka ya EPZ, wamefunga barabara ili kuishinikiza Serikali kuwalipa hundi zao na si viwanja.

MSD YAWASITIRI WANAWAKE TEMEKE



BOHARI ya Dawa nchini (MSD) imetoa mapazia mazito katika wodi ya wazazi iliyopo Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kudhibiti kundi la vijana ambao wamekuwa na tabia ya kuwachungulia mama wajawazito pindi wanapojifungua, anaripoti Mariam Mziwanda.

UTUPAJI TAKA HOLELA WAMPANDISHA KIZIMBANI



 MTU mmoja mkazi wa Mtoni, Wilaya ya Temeke amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Jiji Sokoine Drive kwa kosa la kutupa takataka eneo lisilo rasmi, anaripoti Revina John.

VYAMA VYAMTAKA JAJI MUTUNGI KUCHAPA KAZI



 Penina Malundo na Leah Daudi
BAADHI ya viongozi wa vyama vya siasa wamemtaka msajili mpya wa vyama vya siasa nchini, jaji Francis Mutungi atekeleze majukumu yake bila upendeleo kwa chama chochote.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara, Julius Mtatiro alisema kuwa msajili mpya anatakiwa kufanya kazi yake kwa umakini bila kupendelea chama kimoja.

WAZIRI MAHANGA AWASHUKIA WAAJIRI SEKTA BINAFSI



 Na Mwandishi Wetu, Njombe
NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, amesema Serikali haitaivumilia sekta binafsi yoyote ambayo itawalipa wafanyakazi wake kiwango cha mishahara pungufu ya kile cha kima cha chini kilichotangazwa na Serikali.

WADAU WANOLEWA JINSI YA KUTUMIA KIWANGO CHA ISO



 Neema Rajab na Flora Nkya (TUDARCO)
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Uledi Musa, amelitaka Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo nchini (SIDO) na kampuni binafsi za biashara kushirikiana na Shirika la Viwango vya Tanzania (TBS) ili kuwahamasisha matumizi ya viwango vya ubora vya kimataifa

UKWEPAJI KODI WACHANGIAARUSHA KUPATA HATI CHAFU



 Na Omari Moyo, Arusha
UKWEPAJI wa kodi unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu katika halmashauri ya jiji la Arusha kunachangia manispaa hiyo kupata hati chafu mara kwa mara.Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema kuwa mianya yote iliyokuwa ikichangia kuingiwa kwa mikataba 'feki' katika miradi ya jiji hilo na ambayo imeiletea jiji hilo hasara kubwa pamoja na ukwepaji kodi itazibwa.

KERO

Mkazi wa jiji akipita kando ya wanawake na watoto wanaojishughulisha na kuomba misaada kwa
wasamaria, kama walivyokutwa wamelala kando ya Barabara ya Bibi Titi Mohamed Upanga, Dar es Salaam jana. Juhudi zinazofanywa na mamlaka za jiji kuwaondoa mitaani ombaomba hazijafanikiwi.Baadhi ya ombaomba wamekuwa wakichafua mazingira kwa kujisaidia kando ya barabara
.

PTA YAZIDI KUONGEZA UFANISI



Na Frank Monyo

MAMLAKA ya Bandari Ta n z a n i a ( T PA) , imeendelea kufanya maboresho katika utendaji kazi kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi wakati wa kuwahudumia wateja wake.Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Meneja Mawasilino wa TPA, Janeth Ruzangi, alisema juhudu za pamoja kati ya wadau na mamlaka zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi katika bandari hiyo.

"Mafanikio yaliyopatikana ni kuongezeka kwa shehena kutoka tani milioni 10.9 kwa mwaka 2011/12 hadi kufikia tani 12.5 mwaka 2012/13 ikiwa ni ongezeka la asilimia 15.0 pia katika shehena yote iliyohudumiwa mwaka 2012/13,shehena za chini zitumiazo bandari (landlocked countries) ilikuwa tani milioni 4 ambayo ni sawa na asilimia 32 ya shehena," alisema Ruzangi.

Alisema shehena yote ya mizigo ya nchi 6 zitumiazo Bandari ya Dar es Salaam; za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda imeongezeka kutoka tani milioni 3.55 mwaka 2011/12 hadi kufikia tani milioni 4.05 mwaka 2012/13. Alisema ongezeko hili ni asilimia 14.2.

Aliongeza kuwa muda wa ukaaji wa meli bandarini umepungua kutoka siku 6 hadi siku 4 ambapo ni sawa na asilimia 19.7 wakati idadi ya siku kwa meli kusubiri nje kuingia ndani kwenye gati imepungua kutoka siku 3 hadi kufikia siku 1 mwaka 2012/13 kinyume na siku 28 zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

"Hata hivyo, kasi ya kupakua magari imeongezeka kutoka upakuaji wa magari 343 kwa shift hadi magari 672; ongezeko hili ni asilimia 95.9," alisema Ruzangi.

Alibainisha sababu za kuongezeka kwa ufanisi huo kuwa ni hatua zilizochukuliwa na serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kwa kusimamia kwa karibu utendaji kazi wa mamlaka hiyo.

DOLA MIL.100/- KUWEKEZWA MRADI DARTS



Na Grace Ndossa
DOLA za Marekani milioni 100 zinatarajiwa kutumika kununua mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam kwa upande wa sekta binafsi.Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mifumo na Uendeshaji wa DARTS, John Mashauri, wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana.

CUF YALAANI UCHOMAJI MAKANISA



Na Rehema Mohamed
CHAMA Cha Wananchi (CUF) kinasikitishwa na tukio la kuchomwa moto kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.Pia chama hicho kimelitaka Jeshi la Polisi na mamlaka za usalama wa taifa kupambana na matukio hayo. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi Agosti 24, 2013.

WAWILI TFF WAWEKEWA PINGAMIZI



.  Na Amina Athumani

WAGOMBEA wawili wa nafasi ya urais na Kamati ya Utendaji walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamewekewa pingamizi kuwania nafasi hizo katika uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27, mwaka huu.

YANGA YAILALAMIKIA TFF ADHABU YA NGASSA



 Na Amina Athumani
UONGOZI wa Yanga umelalamikia rufaa waliyoiwasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kuhusu kupinga kufungiwa mchezaji wao, Mrisho Ngassa bado haijasikilizwa huku muda ukizidi kwenda.

WATU 27 WAUAWAWA NA FISI GEITA



Na Daud Magesa, MWANZA
WIZARA ya Maliasili na Utalii, imesema mwaka jana hadi Juni, mwaka huu watu 27 waliuawa na fi si na wanne kujeruhiwa na wanyama hao. Pia fi si 22 wanaodaiwa kujeruhi na kuua watu waliuawa mkoani Geita katika kipindi cha mwaka jana hadi Juni mwaka huu. Kutokana na matukio hayo, 

27 August 2013

ZITTO: SITAKI URAIS 2015

  • AFICHUA SIRI NZITO KUHUSU UBUNGE WAKE


Na Anneth Kagenda
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), ame s ema h a f i k i r i I kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasiliBw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015. Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo

CCM YAMTIMUA UWAKILISHI MANSOUR

  • HALMASHAURI KUU YARIDHIA,YATEUA MAKATIBU


Na Pendo Mtibuche, Dodoma
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana imemaliza kikao chake cha siku tatu
mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete. Kikao hicho kimeridhia baadhi ya mapendekezo ya Kamati Kuu ya CCM, pamoja na kumvua uanachama Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Kiembesamaki, Jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar, Bw. Mansour Yusuf Himid.

MTANDAO UNAOFADHILI UJAMBAZI HADHARANI



Anneth Kagenda na Salma Mzee
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wiki ijayo litaweka hadharani majina ya mtandao unaofadhili matukio ya ujambazi na kuendeleza uhalifu nchini. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

KIKWETE AMWAPISHA JAJI MUTUNGI



Na Penina Malundo
RAIS wa Jakaya Kikwete, jana amemwapisha Msajili Mpya wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji mstaafu Francis Mutungi baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Bw. John Tendwa kustaafu. Ak i z u n g umz a b a a d a y a kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema ingawa kazi hiyo inachangamoto kubwa,
amejipanga kikamilifu kuifanya kwa uadilifu.

POLISI YANASA MAJAMBAZI 4 ARUSHA



Omari Moyo na Queen Lema,Arusha
JESHI la Polisi mkoani Arusha, imewakamata watu wane wanaodaiwa kuhusika na tukio la ujambazi kwa mfanyabiashara wa madini ya tanzanite hivi karibuni, wakiwa na bastola mbili zinazodaiwa kutumika katika
tukio hilo.

OMAN WAVUTIWA KUWEKEZA ATCL



Na Salim Nyomolelo
SHIRIKA la Maendeleo na Uwekezaji la Alhayat kutoka nchini Oman litatumia dola za Kimarekani milioni 100 kuwekeza katika Shirika la Ndege nchini (ATCL), sambamba na kujenga jengo la ghorofa 25 katika eneo la Posta jijini Dar es Salaam kama serikali ikiridhia kusaini mkataba nao.

SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA HAIKIDHI VIWANGO - CHIZA



Na Grace Ndossa
WAZIRI wa Kilimo Chakula na Ushirika Christopher Ch i z a a n awa s i l i s h a mswada wa sheria ya vyama vya ushirika Bungeni kesho kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya pili.Akizungumza hivi karibuni alisema kuwa mswada huo utasaidia kurekebisha sheria ya vyama vya ushirika pamoja na kuundwa kwa Tume ya kusimamia vyama hivyo ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.

TAZARA WAENDELEZA MGOMO,WAMTAKA PINDA


Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), wakiwa kwenye viwanja vya ofisi za mamlaka hiyo, Dar es Salaam jana, wakati wa mgomo unaotokana na kutolipwa mishahara ya miezi 4 mfululizo kuanzia mwezi Mei.


Rehema Maigala na Darlin Said

SAKATA la mgomo wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), limeendelea kuchukua sura mpya ambapo jana wameendelea na mgomo wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aende kusikiliza madai yao.

WANANCHI WALALAMIKIA USIRI WA SERIKALI



Na David John

WANANCHI wa Kijiji cha Nganje, Kata ya Magawa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani wameilalamikia Ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho kwa kushindwa kuitisha mkutano wa wananchi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kwa lengo la kutoa taarifa ya maendeleo ya kijiji hicho

NSSF KUKUSANYA BILIONI 706/- KUTOKA KWA WANACHAMA



Na Fatuma Mshamu
SHIRIKA la Hifadhi ya Taifa (NSSF) linatarajia kukusanya kiasi cha sh. bilioni 706.41 kutoka kwenye michango ya wanachama wake katika mwaka huu wa fedha.Meneja kiongozi wa huduma kwa wateja Eunice Chiume alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatokana na uandikishaji wa wanachama 169,241 wa mpango wa lazima na wanachama 85,158 wanaojiunga kwa hiari.

RUFAA DHIDI YA ZOMBE AGOSTI 29



Na Rachel Balama
MA O M B I y a M k u r u g e n z i w a Ma s h t a k a Nchini (DPP) ya kuongezewa muda wa kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaama, Abdallah Zombe na askari wenzake wanane walioachiwa huru katika shtaka la mauaji yanatarajiwa kusikilizwa Agosti 29, mwaka huu

WAZEE 300 WAUAWA KILA MWAKA



 Na Theonestina Juma, Kagera
ZAIDI ya wazee 300 huuawa hapa nchini kila mwaka kutokana na umaskini na uchu wa kutaka mali na si kwa madai ya ushirikina kama inavyodaiwa katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mratibu wa chama cha Saidiawazee wilayani Karagwe (SAWAKA), Livingstone Byekwaso katika warsha ya siku moja iliyoendeshwa na chama hicho kwa waandishi wa habari mkoani Kagera kuwajengea uelewa juu ya ufuatiliaji wa matatizo yanayowakabili wazee.

MSONGAMANO BANDARINI

Magari yakiwa katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam jana yakisubiri kuchukuliwa na wahusika. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),ipo katika mkakati wa kuondokana na tatizo la msongamano wa mizigo kwa kuongeza vifaa vya kisasa vya upakuaji na upakiaji pia kuondoa urasimu kwa wateja wanaotumia bandari hiyo.

TAKUKURU YAWABURUTA KORTINI VIGOGO USHIRIKA



 Na Hamisi Nasiri, Nachingwea
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi imewafikisha mahakamani viongozi wawili wa chama cha msingi cha ushirika cha Naipanga wilayani humo kwa makosa ya kula njama ya kutenda kosa la rushwa,matumizi mabaya ya nyaraka na ubadhirifu wa fedha za chama hicho.

WATAKA RASIMU IFAFANULIWE KIKAMILIFU



 Na Lilian Justice, Morogoro
WAKAZI wa kata tatu za Manispaa ya Morogoro wameiomba Serikali kupitia baraza la katiba kuhakikisha marekebisho ya rasimu ya Katiba Mpya yanafafanua kwa kina masuala ya kijamii ikiwemo kipengele cha afya, elimu na maji kufuatia vipengele vingi kukosa ufafanuzi.

CHADEMA YAMJIBU DADA YAKE MBOWE



Na Goodluck Hongo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakishangazwi na Grace Mbowe, ambaye ni dada wa Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani si jambo la kushangaza na chama hicho si cha kifamilia.

UZINDUZI WA JENGO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadik, akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi
wa jengo la ghorofa 6 la Nemax Royal Hotel, iliyopo Vijana Kinondoni, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa jengo hilo Bw. Steven Rupia

TAMBWE,KAZE KUTAMBULISHWA KWA MASHABIKI SIMBA J'PILI



Na Elizabeth Mayemba
UONGOZI wa Klabu ya Simba unatarajia kuwatambulisha rasmi wachezaji wake wa kimataifa kutoka Burundi, katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Mafunzo ya Zanzibar itakayochezwa Jumapili ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

26 August 2013

SAKATA LA OFISA USALAMA:SIRI NZITO

  • ADAIWA KUTOA AMRI KWA VIGOGO WA POLISI
  • POLISI KUWEKA HADHARANI UTAPELI WAKE



 Na Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kumnasa Bw. Alquine Masubo (42), akidaiwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa, siri nzito juu ya vitendo vinavyodaiwa kufanywa na mtuhumiwa huyo, sasa zimeanza kufichuka.

MLIPUKO KANISANI DAR: KOVA KUPASUA 'JIPU'



Na Anneth Kagenda
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, leo litazungumzia tukio la mlipuko unaodaiwa ni bomu ambalo lilirushwa kwenye Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Segerea, Dar es Salaam

MAHAKAMA YA KADHI BALAA



 Na David John
BARAZA Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, limesema kipengele cha uwepo wa Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba Mpya, hakiepukiki hivyo ni wajibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kuhakikisha Waislamu wanapata haki yao ya msingi.

DC NZEGA,MADIWANI SASA KUMVAA PINDA



Na Moses Mabula, Nzega
MKUU wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Bituni Msangi, anatarajia kuwaongoza baadhi ya madiwani kwenda kwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kulalamikia mpango wa Wilaya hiyo kucheleweshwa kuwa Halmashauri ya Mji.

SERIKALI TATU YAIBUA MAZITO LUSHOTO



 Na Yusuph Mussa, Lushoto
BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, wamesema Serikali tatu inaweza kusambaratisha muungano uliopo na vyama vinavyopigia debe mfumo huo vina uchu wa madaraka.Walisema mfumo wa Serikali tatu unaweza kuipasua nchi vipande vipande na kusababisha mateso kwa wanawake, watoto, wazee hivyo maoni ya Katiba Mpya lazima yazingatie umakini.

VITABU VITAKATIFU VISITUMIKE KUAPA


Na Yusuph Mussa, Lushoto

BAADHI ya wadau wanaoboresha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametaka Serikali itunge kitabu chake, ambacho viongozi wake watakitumia wakati wa kuapa katika utumishi wao badala ya kutumia vitabu vitakatifu kama Kurani ama Biblia.

UTANDAZAJI BOMBA LA GESI KUANZA LEO



Na Godfrey Ismaley,Aliyekuwa Lindi
SERIKALI imeweka wazi kuwa kuanzia leo shughuli ya utandazaji wa bomba la gesi kutoka Mnazibay mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam unaanza na inatarajia kabla ya Septemba mwaka huu litakuwa limekamilika

WAVUVI ,WAFUGAJI ZIWA RUKWA WAPIGANA



Rashid Mkwinda na Esther Macha, Momba
VU R U G U k u b w a iliyosababishwa na kile kinachoelezwa kugombea mpaka kati ya vijiji vya Senga wilayani Momba mkoani Mbeya na Kijiji cha Ilambo kilichopo Kata ya Kapeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa imeibuka na kusababisha nyumba 24 kuchomwa moto.Pia katika vurugu hizo watu sita walijeruhiwa kwa kupigwa fimbo na mapanga.

UDA KUINGIZA MABASI MAPYA 2000



Na Reuben Kagaruki
SHIRIKA la Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam (UDA) linatarajia kuingiza mabasi 2,000 kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri jijini ifikapo Juni mwaka 2014.Haya yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Saimon Group, Robert Kisena, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika ndani ya UDA kuhusiana na uwekezaji.

TUZO ZA RAIS KWA WACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO YATOLEWA



Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya utafiti madini ya urani yenye mradi wake ujulikanao kama Mto Mkuju ya Mantra ya Tanzania, imeibuka mshindi kwa kunyakua tuzo tatu kwenye Tuzo za Rais katika Tasnia ya Uziduaji kwa makampuni yanayofanya vizuri katika Miradi ya Kijamii na Uwezeshaji (Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment) kwa mwaka 2012.

SERIKALI YATAKIWA KUSIMAMIA UINGIZAJI SARUJI KUTOKA NJE



 Na Grace Ndossa
SERIKALI imeshauriwa kuanzisha juhudi za makusudi zitakazosaidia kukabiliana na uingizwaji wa bidhaa zisizo na viwango zinazoingizwa nchini ikiwemo saruji.Ushauri huo umetolewa na kampuni ya kuzalisha saruji ya Tanzania Portland Cement Company (TPCC).

TAHLISO YAWAVAA WANAFUNZI WANAOTUMIKA KISIASA NCHINI



Na Darlin Said
TAASISI ya Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu (TAHLISO) imelaani vikali matukio yaliyojitokeza katika mkutano wa baadhi ya viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vya elimu ya juu hapa nchini uliofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni na kudai kuwa ni ulikuwa kinyume na maadili.

WASINDIKAJI ALIZETI WANG'AKA



Na Elizabeth Joseph, Dodoma
CHAMA cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Tanzania (TASUPA) kimetoa siku kumi na nne kwa mmiliki wa Kiwanda cha Murzah Oil Mills Group of Companies kukanusha kauli yake aliyoitoa kudai kuwa mafuta ya alizeti hayana ubora kwa matumizi ya binadamu

YANGA,ASHANTI ZAINGIZA MILIONI 102/-



Na Mwandishi Wetu
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), kati ya Yanga na Ashanti United iliyochezwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 102,856,000

SHANGWE ZA CASTLE LAGER,FC BARCELONA ZAITEKA MWANZA



Na Mwandishi Wetu
MAE LFUyamashabikiwasoka jiji ni Mwanza, wamepata burudani ya aina yakekutokananashamrashamr a zaut ambul ishowa udhamini waCast leLagerkwa FCBarce lona,zi lizofany ikamwishoni mwawiki n akuvutiamas habiki wakandanda.

MASHABIKI WA LIVERPOOL WANYAKUA UBINGWA



Na Mwandishi Wetu, Singida

TIMU ya soka ya mashabiki wa Li v e r p o o l n c h i n i Uingereza wa mjini Singida, juzi imenyakua ubingwa wa bonanza la Serengeti Fiesta mkoani hapa, baada ya kuichapa Bayern Munich ya Majengo mabao 2-0.Kwa ushindi huo, Liverpool imejinyakulia kombe na sh. 300,000 taslimu. Mshindi wa pili Bayern Munich, wao walizawadiwa sh. 200,000.

RIPOTI MAALUM - 2:UBAKAJI WAJANE



Na Reuben Kagaruki
SEHEMU ya kwanza ya makala hii ya Okosomboka, ilieleza kwa kina maana halisi ya mtu anayesombokwa na jinsi usombokaji unavyofanyika kwa wakazi waishio Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza hasa kwa Wakala na Wajita.

24 August 2013

KAMATI YABAINI MADUDU HAZINA



Anneth Kagenda na Mariam Mziwanda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imebaini wizi wa mabilioni unaofanywa na Hazina kwa kutakatisha fedha katika malipo ya halmashauri nchini.Utakatishaji huo unadaiwa kufanywa kwa kufoji malipo hewa na kuongeza takwimu za fedha kwenye bajeti za halmashauri

WIZI WA KUTISHA TPA-KAMATI



Mariam Mziwanda na Anneth Kagenda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imebaini wizi wa kutisha katika Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na kuhoji kwa kina matumizi ya fedha mbalimbali zikiwamo sh. bilioni 9.1 zinazodaiwa kutumika katika Mkutano Mkuu wa wanachama.Pia kamati hiyo ilihoji matumizi ya sh. bilioni 10 zilizodaiwa kutumika kwa safari za ndani na nje pamoja na sh. bilioni 6.2, zinazodaiwa kutumika kwenye matangazo.

KORTINI KWA KUFOJI SAINI YA PINDA



Na Rehema Mohamed
MFANYABIASHARA Ahmed Popi (35), jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kufoji barua na saini ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda.
Mbele ya Hakimu Waliyarwande Lema, wakili wa Serikali Hamisi Saidi, alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo muda na terehe isiyofahamika jijini Dar es Salaam.