31 January 2013
Wajasiriamali mnapaswa kungeza nguvu-TIC
Na Mwandishi wetu, Mbeya
KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema wajasiriamali nchini wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika kuendelea biashara kwa kuwa biashara zao ni nguzo ya uchumi wa nchi.
Serikali yashangazwa wageni kufavamia mbunga
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeshangazwa na hatua ya wageni kuvamia mbuga mbalimbali na misitu nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.
KESI YA PONDA KUENDELEA LEO
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo inatarajiwa kuendelea na kesi ya wizi na uchochezi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake kutokana na upande wa mashtaka kukosa mashahidi.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo inatarajiwa kuendelea na kesi ya wizi na uchochezi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake kutokana na upande wa mashtaka kukosa mashahidi.
Wabunifu 25 kushiriki Lady in Red
Na Mwali Ibrahim
WABUNIFU 25 nchini, wanatarajia kuonesha mavazi katika mashindano ya Lady in Red 2013, yanayotarajia kufanyika Februari 9 mwaka huu katika Ukumbi wa Serena Hoteli, Dar es Salaam.
Vijana FC yapenya nusu fainali
Na Omary Mngindo, Kibaha
VIJANA FC ya Kongowe Kibaha mkoani Pwani, juzi imeingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mikoba Cup,
inayoendelea katika Kata ya Misugusugu wilayani hapa.
Msanii Bluestar kuachia Tunachafua
Na Queen lema, Arusha
MSANII wa jijini Arusha anayekuja kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya,
Hamisi Omari (20) 'Bluestar' anatarajia kuachia singo yake ya tatu inayokwenda kwa jina la Tunachafua.
Twende Kanisani kuzinduliwa Febr. 10
Na Mwandishi Wetu
MSANII wa nyimbo za injili anayekuja juu nchini, Kennedy Daudi ameahidi burudani ya nguvu kweli katika uzinduzi wa video ya albamu yake ya ‘Twende Kanisani’ utakaofanyika katika Bwalo la Magereza, Ukonga Dar es Salaam Februari 10, mwaka huu.
Stars yazitosa Rwanda, Congo *Sasa kucheza na Cameroon
Na Zahoro Mlanzi
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema lilipata maombi ya kucheza na nchi nne tofauti katika 'FIFA date', lakini imeamua kuachana nazo kutokana na kushindwa kufikia muafaka na kuamua kuikubalia Cameroon.
29 January 2013
LULU KUTOKA RUMANDE
Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' akiongozwa na askari magereza, wakati akitoka Mahabusu ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana, baada ya taratibu za dhamana kutokamilika. Msanii huyo anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii wa filamu, marehemu Steven Kanumba. (Picha na Charles Lucas)
CCM yajitosa sakata la gesi *Kinana adai wananchi Mtwara wana hoja *Nape asisitiza rasilimali kunufaisha wote *53 wafikishwa kortini, Nchimbi atoa agizo
Na Waandishi Wetu, Mtwara na Dar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Abdulrahman Kinana, amesema wananchi mkoani Mtwara wana hoja ya msingi kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam, hivyo wanahitaji majibu sahihi ya kuwaridhisha.
Mpina alipuka utoroshaji tril. 11.6/- *Aitupia lawama serikali, apeleka hoja bungeni
Na Benedict Kaguo
MBUNGE wa Kisesa, mkoani Simiyu, Bw. Luhaga Mpina (CCM), amefichua mpango wa Serikali kuwalinda viongozi walioficha fedha katika benki zilizopo nje na kusababisha umaskini kwa Watanzania.
DC Korogwe ategwa kwa magogo
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MSAFARA wa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, juzi uliwekeza magogo barabarani na kusababisha taharuki kubwa kwa watu waliokuwa katika msarafa huo.
Kisandu amtega Zitto
Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Uhusiano na Uenezi Taifa, Kitendo cha Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. Deogratius Kisandu, amesema Tanzania imekosa vijana wazalendo ndio sababu ya kushindwa kutekeleza wanachokisema.
Bulembo amshukia Bujugo
Na Gladness Mboma
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Bw. Abdallah Bulembo, amemtaka Diwani wa Kata ya Magomeni Dar es Salaam, anayeendesha Chuo cha Kilimo cha Kaole, kilichopo Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Julian Bujugo, kukikabidhi chuo hicho kwa jumuiya hiyo kabla hajachukuliwa hatua za kisheria.
Uchumi umekua kwa asilimia 6.7-Mgimwa
Na Eliasa Ally, Iringa
WAZIRI wa Fedha na Uchumi Dkt.william Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Kalenga katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini amesema kuwa hali ya uchumi hapa nchini inaendelea kuimarika ambapo kwa sasa uchumi ndani ya nchi umekua hadi kufikia asilimia 6.8 hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wananchi na serikali yao.
WAZIRI wa Fedha na Uchumi Dkt.william Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Kalenga katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini amesema kuwa hali ya uchumi hapa nchini inaendelea kuimarika ambapo kwa sasa uchumi ndani ya nchi umekua hadi kufikia asilimia 6.8 hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wananchi na serikali yao.
BoT yataka Katiba Mpya iwabane wanasiasa wasiingilie utendaji
Anneth Kagenda na Rehema Maigala
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imependekeza kuwekwa kipengele cha sheria ambacho kitawabana wanasiasa kutoingilia kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na benki hiyo.
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imependekeza kuwekwa kipengele cha sheria ambacho kitawabana wanasiasa kutoingilia kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na benki hiyo.
Wazee waliopigana Vita ya Dunia wailaumu Serikali
Na Darlin Said
CHAMA cha Wazee Waliopigana Vita vya Pili ya Dunia hapa nchini (TCL) wameilaumu serikali kwa kuwatelekeza na kuwaacha wakihujumiwa mali zao.
Bilioni 8/- zatengwa kwa ajili ya mradi wa UMATA
Na Grace Ndossa
JUMLA ya sh. bilioni nane zimetengwa kwa ajili ya kuendesha mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) ambao utaanzia katika Mkoa wa Dodoma na jumla ya watu milioni moja watafaidika na mradi huo.
Wenyeviti waitaka Serikali kuzitambua kazi zao kikatiba
Na Rose Itono
UMOJA wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam (UWESEMIDA)umeitaka Serikali kuzitambua kazi zao kikatiba kama viongozi wengine kulingana na majukumu yao kikazi.
Polisi Pwani yawashikilia wahamiaji haramu watano
Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia wahamiaji haramu watano wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kuingia nchini bila kibali.
Wakulima wa kahawa watuhumiana K'njaro
Na Gift Mongi
MRAJISI Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Kilimanjaro, Kasya Kasya amedaiwa kukikingia kifua Chama Kikuu cha Ushirika mkoani humo (KNCU) ikiwemo kulihujumu zao la kahawa.
TRA yatakiwa kutafuta mbinu mpya ya ukusanyaji kodi
Na Mariam Mziwanda
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi Bi.Saada Mkuya ameitaka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kutafuta mbinu mpya za ukusanyaji wa kodi ili kuliongezea taifa mapato.
JK kuzindua mkutano wa TNBC
Na Heri Shaaban
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuzindua mkutano wa biashara wa Kitaifa Machi mwaka huu, utakaohusu semina elekezi kuhusiana na majadiliano ya ushirikiano kwa wote.
WAKIPONGEZANA
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto), akipongezana na mmoja wa wanachama wa chama hicho katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Bi. Fatma Bakari wakati wa mkutano wa kumbukumbu ya Miaka 12 ya mauaji ya wanachama wa chama hicho yaliyotokea Zanzibar. (Picha na Peter Twite)
PFT yaitaka jamii kufahamu umuhimu wa VICOBA
Na Rose Itono
SHIRIKA la Kupambana na Umasikini (PFT) limeitaka jamii kufahamu kuwa VICOBA ni silaa kubwa katika kupambana na umasikini.
Haki za binadamu waombwa kuingilia mgogoro wa mirathi
Na Mariamu Mziwanda
FAMILIA ya marehemu Juma Maulid wameiomba wanasheria za haki za binadamu iwasaidie kupata mirathi ya marehemu baba yao pamoja na Serikali kutokana na baadhi ya ndugu wa familia kuzikumbatia mali hizo kwa miaka mitatu na kusababisha watoto kuishi maisha ya shida na kushindwa kwenda shule.
Maktaba sekondari ya Baobab kugharimu mil. 800
Na Rehema Maigala
SHULE ya sekondari ya Baobab iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani inajenga maktaba ya kisasa itakayoghalimu sh.milioni 800 ili kukidhi haja ya wanafunzi wao
28 January 2013
MAKABIDHIANO
Inspekta wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema akimkabidhi Kamanda wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova kwa niaba ya makamanda wote pikipiki 564 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi nchini. (Picha kwa hisani ya Mtandao.)
Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi unaimarisha usalama nchini-Mwema
Na Stella Aron
MATUKIO ya uhalifu nchini yameonyesha kupungua kutokana na ushirikiano mzuri kati Jeshi la Polisi na wananchi kwa kutoa taarifa za uhalifu.
MAONI YA KATIBA
Tusitafute Katiba Mpya Pekee
NENO “Pekee” kwa tafsiri ya lugha ya kigeni yaweza kuwa “Special”. Kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita tumeweza kutawaliwa na katiba yenye sifa za kipekee, nasema katiba ya kipekee kwa vile katiba tunayoitumia hivi sasa ilikuwa haifanani na katiba nyingine yoyote ile duniani.
TBS yajipanga kumaliza tatizo la bidhaa bandia nchini
Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na chagamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limeweza kutimiza wajibu wake wa kuwahudumia Watanzania na wateja wake kwa ujumla na kuahidi kutoa huduma bora mwaka huu.
Kauli ya Mangula iwe kwa vitendo
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM,Bw Philip Mangula ameweka msimamo wake dhidi ya wanachama wa chama hicho walioanza kujipitisha kwenye majimbo mbalimbali ya uchaguzi kwa lengo la kujiandaa na uchaguzi ujao.
Bao la Tegete lamvua nguo mlemavu *Domayo augua gafla, Yanga ikishinda 3-1
Na Zahoro Mlanzi
UKISTAAJABU ya Mussa utayaona ya filauni, ndivyo unavyoweza kusema baada ya shabiki aliyedaiwa kuwa wa timu ya Yanga, kuingia uwanjani huku sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa tupu akishangilia bao la tatu lililofungwa na Jeryson Tegete katika mchezo uliopigwa Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Nyamlani, Malinzi wawekewa pingamizi TFF
Na Zahoro Mlanzi
WAGOMBEA wote wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Bara, wamewekewa pingamizi wasigombee uongozi kwa sababu mbalimbali.
Stewart avua nguo Chamazi
Na Mwandishi Wetu
KITENDO cha kocha wa Azam FC, Stewart Hall kuonyesha nguo yake ya ndani, kimetafsiriwa tofauti na mashabiki waliohudhuria mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya timu yake ilipoumana na Kagera Sugar, juzi katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
MAZUNGUMZO
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, Bw. Augustine Mrema, akizungumza na baadhi ya wahariri wa Majira, katika chumba cha habari cha gazeti hili Dar es Salaam jana, kuhusu malalamiko ya wakazi wa Himo wilayani Moshi Vijijini, wanaolalamikia kujengwa kwa kiwanda katika kiwanja namba 16 eneo ambalo ni makazi ya watu. Kushoto ni Mhariri wa Habari za Mikoani Bw. Benedict Kaguo na Mhariri wa Majira Jumapili, Bi. Gladness Mboma. (Picha na Charles Lucas)
Serikali yashauriwa kuacha kuwakumbatia wawekezaji
Na Suleiman Abeid,
Maswa
MWANAFUNZI anayesoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mataba wilayani Maswa mkoani Simiyu Christopher Andrea ameishauri serikali iache mtindo wa kuwakumbatia wawekezaji wa kigeni vinginevyo Tanzania itageuka kuwa nchi ya kibebari.
Vijiji vitatu vyadaiwa kutaka kuanzisha vurugu tena Kilosa
Severin Blasio, Kilosa
BAADA ya kuzuka vurugu katika eneo la Dumila wilayani Kilosa hali si shwari katika vijiji vya Kilangali,Kivungu na Mbamba kata ya Kilangali wilayani humo baada ya shamba la Summer Grow walilokuwa wakilima wananchi wa vijiji hivyo kupewa
wafugaji.
Wanasiasa wanawatia hofu wafanyakazi-TUGHE
Na Daud Magesa,Mwanza
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), Ali Kiwenge amewashukia viongozi wa kisiasa nchini akisema kuwa kauli zao zinawatia hofu
wafanyakazi na wananchi.
Sera ya utunzaji mazingira iwe endelevu
Na Jovin Mihambi.
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais kitengo cha mazingira imeweka bayana kwamba kila jamii hapa nchini iweze kutunza na kuhifadhi mazingira ili kurudisha mandhari ya mazingira kama yalivyokuwa kabla ya nchi ya Tanganyika kupata uhuru wake miaka 51 iliyopita.
Waushutumu NASA kuficha sayari tishio
Na Danny Matiko
KATIKA toleo lililopita tulishia kuona baadhi ya wananchi wa Marekani wakilishutumu shirika la anga za juu la nchi hiyo, NASA, wakidai kuwa limekuwa na tabia ya kuficha masuala mengi ambayo ni matokeo ya uchunguzi wa anga za juu
"Mbeya msizike walio hai"
Adhabu mbadala jibu la msongamano magerezani
Na Aziz Msuya
MWENYEKITI wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama, Bw. Edward Lowassa amekaririwa akisema kuwa asilimia 90 ya wafungwa walioko magerezani ni vijana
MAZUNGUMZO
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Habari, Wamiliki na Wahariri wa Vyombo
vya Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, wakati alipozungumza nao kwenye
makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam juzi. (Wa tatu kushoto) ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Business Times Limited, Bw. Aga Mbuguni. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Kalonga waikataa taarifa ya tume
Na Suleiman Abeid,
Shinyanga
WAKAZI wa mtaa wa Kalonga manispaa ya Shinyanga wameikataa taarifa ya Tume ya uchunguzi iliyokuwa imeundwa kuchunguza ubadhirifu wa shilingi milioni 26.2 zilizokuwa zimetolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Kila shule iwe na mabweni-TGNP
Na Mariam Mziwanda
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeeleza umuhimu wa kuwa na sera itakayowezesha kila shule nchini kuwa na mabweni ya wasichana ili kuwaandaa wanawake katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa dunia.
Wananchi watakiwa kujenga nidhamu Temeke
Na David John
MKUU wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujenga nidhamu ya kusimamia vizuri huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao.
Ni mapambano tena Dar,Moro *WANANCHI WACHOMA MAGARI,WAPORA,WAVUNJA NYUMBA *RC,DC WADAIWA KUWA CHANZO,MMOJA AFA *DAR,POLISI MACHINGA WAPAMBANA
Na Waandishi Wetu Dar, Kilosa
WANANCHI wenye hasira katika Kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro walifanya vurugu kubwa zilizoambatana na wizi, uporaji na uharibifu wa mali, ambapo nyumba mbili za kulala wageni zilivunjwa na magari kadhaa kuharibiwa kwa kupigwa mawe na mtu mmoja kufariki dunia kwa mshtuko wa mabomu.
Zitto amtaka Sitta kufikiria upya chama cha kugombea urais
Na Gladness Mboma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe amesema, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Sumuel Sitta ana haki ya kugombea nafasi ya urais kama ilivyo kwa Mtanzania mwingine, lakini anapaswa kufikiria upya kuhusu chama anachotaka kupeperusha bendera ya urais.
Njama za kumng'oa meya Bukoba zagonga mwamba
Na Livinus Feruzi
Bukoba.
KITENDAWILI cha madiwani kumi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba akiwemo Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki cha kutaka kumg'oa Meya wa manispaa hiyo Dkt. Anatory Amani katika wadhifa wake kimeshindwa kuteguliwa, baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa,Bw.Philip Mangula kuwataka viongozi hao kufuata taratibu za chama kabla ya kumng'oa.
Vurugu,Rufiji,familia 19 za polisi zaishi kituoni *watu 28 mbaroni
Na Masau Bwire
WATU 28 wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika na uchomaji moto wa nyumba nne za askari wa Jeshi la Polisi na kuteketeza mali zote zilizokuwemo.
Diwani CHADEMA asimamishwa akituhumiwa kuuza chakula cha msaada Kenya
Na Timothy Itembe, Rorya
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya Rorya kimemsimamisha uongozi kwa muda mwenyekiti wake ambaye pia ni Diwani kata ya Tai, Bw.Goodfrey Masirori kwa tuhuma za kuuza chakula kilichotolewa na serikali kwa ajili ya kugaiwa katika kata ambazo zimekumbwa na baa la njaa wilayani humo.
SHAMRASHAMRA
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu, wakiwa juu ya gari namba T 561 BWJ huku wakiwa wamenyanyua bendera zao juu kwa ishara ya kusherehekea Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W),katika barabara ya Nyerere Dar es Salaam jana.(Picha na Peter Twite)
Kiwanda cha kutengeneza mafuta ya albino kuzinduliwa Moshi
Rachel Balama na Anneth Kagenda
KIWANDA cha kutengeneza mafuta kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kilichopo mkoani Moshi kilichogharimu sh. milioni 68 kinatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote kuanzia sasa.
Waislam watakiwa kujiepusha na vurugu
Na Florah Temba,Moshi.
WAISLAM kote nchini,wametakiwa kujiepusha na vurugu mbalimbali ambazo zinahatarisha amani na utulivu wa nchi, kutokana na kwamba madhara ya uvunjifu wa amani katika Taifa lolote duniani ni makubwa.
UBANI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akitia ubani kama ishara ya ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa juzi katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Waumini wa Dini ya Kiislamu. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
Radi yawajeruhi mama,watoto
Na Cresensia Kapinga,Songea
MWANAMKE mmoja Zainabu Ally (33) na wanawe wawili,Ally Khamisi (5) na Hawa Nigange (4)wote wakazi wa kijiji cha Rwinga nje kidogo ya mji wa Namtumbo mkoani Ruvuma wamejeruhiwa vibaya kwa radi nje ya nyumba yao wakati walipokuwa wakila chakula.
Tanzania kunufaika na miradi mitatu mikubwa kutoka China
Na Anneth Kagenda
TANZANIA inatarajia kuneemeka na miradi mikubwa mitatu kutoka nchini China ambayo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 28.2 za kitanzania ukiwamo mradi wa chakula ambapo chakula hicho kitasambazwa katika maeneo yote nchini hasa yale ya vijijini ili kupunguza tatizo kubwa lililopo.
Rais Kikwete kutetea ripoti utawala bora leo
Na Hassan Abbas, Addis Abbas
Rais Jakaya Kikwete leo Jumamosi anatarajiwa kuiwasilisha na kuitetea
Ripori ya hali ya Utawala Bora mbele ya viongozi wenzake wa nchi za Afrika
zinazoshiriki katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
KARIBISHWA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya mkesha wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W). Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Albino waomba kupewa huduma bure ya DNA
Na Peter Mwenda, Kisarawe
WATU wenye ulemavu wa ngozi (albino) wilayani hapa wameiomba Serikali kutoa bure huduma ya kupima vinasaba (DNA)kuondoa utata katika ndoa zao hasa wanapozaa watoto ambao hawana ulemavu huo.
Tunataka kutembelea miradi yote ya UKIMWI-Kamati ya Bunge
Na Rose Itono
WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,sheria na utawala wametaka kupewa umuhimu wa kutembelea mara kwa mara miradi na shughuli mbali mbali zinazohusiana na kampeni dhidi ya UKIMWI nchini ili kujua hasa thamani ya fedha zinazotolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kupambana na ugonjwa huo.
Kamati Kuu Chadema kukutana leo
Na Stella Aron
KAMATIi Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kufanya mkutano maalum wa siku mbili kwa ajili ya kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo taarifa ya fedha kwa mwaka 2012.
Wasanii kupamba Siku ya Ma-Star kesho
Na Elizabeth Mayemba
WASANII wa Bongo flava nchini watashirikiana na wa Bongo muvi katika onesho maalumu la Usiku wa Ma-Star, linalotarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala, Dar es Salaam.
CHANEDA kuandaa michuano maalumu
Na Mwali Ibrahim
CHAMA cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA), kukinatarajia kuandaa mashindano maalumu ya netiboli kwa timu za mkoa huo wiki ijayo, ili kuchagua timu ya mkoa.
TASWA kuwapambanisha Malinzi, Nyamlani
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimepanga kufanyika mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Februari 15, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Bulembo ataka walimu kusimamia michezo
Na Andrew Ignas
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo amewata walimu kuhakikisha wanasimamia sera ya michezo shuleni, ili kujenga Taifa lenye kuthamini michezo.
Vodacom yataka klabu kutoa ushindani
Na Zahoro Mlanzi
WADHAMINI wa Ligi Kuu Bara, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imezitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuendelea kuonesha ushindani, kama zilivyofanya katika mzunguko wa kwanza.
Kocha wa kikapu akata tamaa
Na Amina Athumani
KOCHA wa timu ya Taifa ya mpira wa kikapu, Evarist Mapunda amesema matumaini ya Tanzania kuingia hatua ya robo fainali ni madogo.
MASHINDANO
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Rwabda, Kamana Issa (kulia) akiwania mpira sambamba na mchezaji wa Burundi Henderson Tema, wakati wa mechi ya mashindano ya Kanda Tano ya Afrika iliyofanyika Dar es Salaam jana. Rwanda ilishinda kwa pointi 62-52. Picha na Rajabu Mhamila
Vibonde wa Yanga waitafuna Simba
Na Elizabeth Mayemba
MABINGWA wa Tanzania Bara Simba jana walifungwa bao 1-0 na timu ya Afrika Kusini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
TBL yamwaga vifaa Simba, Yanga
Na Elizabeth Mayemba
KLABU za Simba na Yanga, jana zimekabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 70 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza kesho.
22 January 2013
Makamba afumua menejimenti TTCL
Na Mariam Mziwanda
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameahidi kufumua uongozi uliopo katika Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kutokana na shutuma za ubadhirifu yakiwemo matumizi mabaya ya uongozi.
21 January 2013
Nape afichua siri za kifo Chadema *Asema hakuna dawa ya kutumia lazima kife *Adai ni laana ya Nyerere, wasitafute mchawi
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kisitafute mchawi anayewamaliza nje ya chama chao.
MKUTANO
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza jana ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa
chama chicho Bara, Bw. Philip Mangula. (Na Mpigapicha wetu)
Ajali yaua mmoja, 48 wajeruhiwa
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
MTU mmoja amefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Kampuni ya Nganga Express lenye namba za usajili T 413 AVU, baada ya kupinduka kwenye Mlima wa Imezu, jana asubuhi.
Waandidhi Mbeya watimua viongozi wao kwa ubadhirifu
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mbeya, umelazimishwa kujiuzulu na wanachama kutokana na tuhuma
za ubadhirifu wa fedha za klabu uliofanyika kwa miezi minne.
Katibu wa CHADEMA ahamia NCCR
Na Darlin Said
ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Mbeya, Bw. Eddo Makata, ametangaza rasmi kujiunga na chama
cha NCCR-Mageuzi.
SALAMU
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Philip Mangula (kulia), akiwasalimia mabalozi wa nyumba 10 kutoka kata 21 za Ilemela na Nyamagana, mkoani Mwanza baada ya kuzungumza nao kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini humo jana. Nyuma yake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Bw. Nape Nnauye. (Picha na Bashir Nkoromo)
Ugonjwa unaomsumbua DCI Manumba kuwekwa hadharani
Na Stella Aron
UONGOZI wa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, leo unatarajia kueleza umma ugonjwa unaosumbua Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Robert Manumba.
Ridhiwani: Nakerwa na ushabiki wa siasa vyuoni
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MJUMBE wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC), Bw. Ridhiwani Kikwete, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa Vyuo Vikuu mkoani Mbeya kujiingiza katika ushabiki wa kisiasa.
Bulembo atishia ajira za watendaji
Peter Mwenda na Andrew Ignas
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Abdallah Bulembo, ametishia kuwafukuzisha kazi watendaji wa Serikali ambao watabainika kutoa ushirikiano kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Askofu: Mgawanyo wa rasilimali usio wa haki unachangia vurugu
Na Heckton Chuwa, Moshi
BALOZI wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Fransisco Padilla, amesema vurugu zinazotokea kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani, zinachangiwa na mgawanyo wa rasilimali usio
wa haki katika nchi husika.
DIRISHANI
Mkazi wa jijini akipanda gari kwa kuingilia dirishani, kwenye gari namba T 288 AZB linalo fanya ruti kati ya madafu Kariakoo, kama alivyo kutwa na mpiga picha wetu Dar es Salaam jana.Abiria wamekuwa kero kwa makonda kutokana na uharibifu wa kuvunjwa vioo vya madirisha.Picha na Prona Mumwi
Hukumu ya Mchina mtoa rushwa yazua gumzo
Na Raphael Okello, Bunda
SAKATA la raia wa China aliyeshtakiwa kwa kutaka kumpa
rushwa ya sh. 500,000, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, mkoani Mara Bw. Joshua Mirumbe na kukwepa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kulipa faini ya sh. 700,000, limeibua hisia tofauti
miongoni mwa wananchi juu vita dhidi ya rushwa nchini.
'Wana CCM jibuni mapigo ya wapinzani'
Na Severin Blasio, Morogoro
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UWT), Bi. Sophia Simba, amewataka wana CCM kufunguka na kujibu mapigo ya wapinzani ili kukijenga chama chao.
CHADEMA yawataka wanawake wasitishike
Na David John
MBUNGE wa Ubungo, Bw. John Mnyika, amelitaka Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA), kutoogopa vitisho ambavyo vinaenezwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa mwaka huu utakuwa wa vurugu.
Fenella ataka vijana wapige vita dawa za kulevya
Na Amina Athumani
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mkangara amewataka wachezaji wanaocheza wa Kombe la Meya kuwa mabalozi wazuri katika kupiga vita utumiaji wa dawa za kulevya kwa vijana.
Wawili watakiwa kuachia ngazi bodi ya filamu
Na Amina Athumani
KATIBU Mtendaji wa Bodi ya filamu Tanzania aliyechaguliwa na Serikali, Joyce Fisoo na Ofisa wa COSOTA, Yustus Mkinga wametakiwa kuachia nyadhifa zao kwa madai kuwa utendaji wao si mzuri.
ZAWADI
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb akimkabidhi bahasha yenye fedha taslimu sh. mil 1 beki wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa (kulia) wakati wa Mkutano Mkuu wa kila mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo na Polisi, Oysterbay Dar es Salaam jana.Na Mpigapicha Wetu
Wanachama Yanga wampa rungu Manji *Nsajigwa alamba mil. 1 nidhamu bora
Na Zahoro Mlanzi
WANACHAMA zaidi ya 1444 wa Klabu ya Yanga, wameridhia kumpa ridhaa Mwenyekiti wao, Yusuph Manji pamoja na Makamu wake, Clement Sanga kuteua Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaowataka wao pamoja na kumfukuza mjumbe yeyote atakayeonekana hafai.
Pinda kufungua kikapu Zone V leo
Na Amina Athumani
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda leo atazindua mashindano ya Kanda ya Tano ya mpira wa kikapu (Zone v) katika Uwanja wa Ddani Taifa, Dar es Salaam.
Tusikemee rushwa bila wahusika kukamatwa, kuchukuliwa hatua
TATIZO la rushwa nchini, lipo katika sekta mbalimbali lakini hali hiyo haina maana kuwa inakubalika katika jamii.
Ukweli ni kwamba, rushwa haikubaliki kutokana na madhara yake ndio maana Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.
Waishitumu NASA kuficha sayari Tishio
Na Danny Matiko
MAKALA yaliyopita tuliwaletea habari za kukanusha madai ya kuwepo sayari tishio kwa dunia, hususan kufuatia uvumi uliosambaa duniani mwishoni mwa mwaka jana 2012, kwamba kulikuwa na sayari kubwa ikija kuigonga dunia na kuisambaratisha.
Tusiwahukumu wananchi wa Mtwara
Na Danny Matiko
ITAKUMBUKWA kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania wananchi waliandamana mkoani Mtwara Desemba 27, mwaka jana, kupinga gesi-asili inayochimbwa mkoani humo kusafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Dar es Salaam.
Tuhoji polisi inapotumia mabomu kudhibiti sisimizi
Na Gladness Mboma
JUZI wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wanaokaa katika makazi ya mtu binafsi Kigamboni waliandamana hadi Makao Makuu ya Polisi, ambako pia ni Makao Makuu ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutoa malalamiko yao juu ya vitendo vya kubakwa, kulawitiwa na kuibiwa mali zao na watu wanaodhaniwa majambazi mara kwa mara.
Marufuku mifuko ya jamii kujenga bila mikataba-POAC
Anneth Kagenda na
Rachel Balama
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC),imeipiga marufuku Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kujenga miradi yoyote bila kuwa na mikataba kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta madhara siku za usoni.
Ajinyonga hadi kufa kwa madai anakwenda kwa yesu
Na Patrick Mabula,
Kahama,
MWANAUME mmoja mkazi wa mitaa ya Vumilia mjini Kahama, Bw.Mayala Mwagala 58 amejinyonga hadi kufa chumbani kwake kwa madai kuwa anakwenda kwa Yesu.
Kipindi hichi siyo cha msimu wa vyakula
Na Heri Shaaban
MFUMUKO wa bei katika bidhaa za vyakula Dar es Salaam unadaiwa kuwa unatokana na kipindi hichi kutokuwa cha msimu wa vyakula.
Kesi ya Badwell yapigwa kalenda
Na Rehema Mohamed
KESI ya kuomba na kupokea rushwa ya sh.milioni 8 inayomkabili Mbunge wa Bahi (CCM) Bw.Omary Badwell itaendelea kusikilizwa Februari 15 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Viongozi mitaa,watendaji wailalamikia serikali
Na Darlin Said
VIONGOZI wa Serikali za mitaa na Watendaji wameilalamikia serikali kushindwa kuwashirikisha katika kufanya maamuzi mbalimbali ya kimaendeleo hali inayosababisha kutokuwa na uhusiano nzuri baina yao na wananchi.
Nitawachongea watendaji wote wa Halmashauri
Na David John.
MBUNGE wa Kisarawe Seleman Jafu amesema atahakikisha anawachongea kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda watendaji wote wa halmashauri hiyo ambao wanachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wake.
Jiji kuandaa ramani,ujenzi wa kituo cha mabasi Mbezi
Na Heri Shaaban
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam inaandaa mchoro wa ramani kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo Mikoani na Nchi Jirani eneo la Mbezi kwa Ruis.
Mmoja afariki dunia, watano wajeruhiwa Dar
Na Leah Daudi
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Hatibu Halfani (33) amefariki dunia mara baada ya gari alilikuwa akiendesha kugongana na gari lingine na kumsababishia kifo.
TWB kufungua tawi la pili Kariakoo
Na Amina Athumani
BENKI ya wanawake nchini (TWB) inatarajia kufungua tawi lake la pili maeneo ya Kariakoo mwezi Februari mwaka huu baada ya kufikisha mtaji wa sh. bilioni 6.8 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo miaka mitatu iliyopita.
Marufuku korosho kununuliwa kwa vipimo vya kangomba-DC
Na Steven Augustino, Tunduru
MKUU wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Bw. Chande Nalicho amepiga marufuku ununuzi wa kutumia Vipimo vya KANGOMBA chenye ujazo wa zaidi ya kilo moja unaoendelea sasa kutokana na kuwanyonya wakulima wa Korosho.
Teknolojia Mbola kusambazwa nchini kuondoa umaskini
Na Moses Mabula, Uyui
WAZIRI wa Fedha Dkt Wlliam Mgimwa amesema Serikali
inaangalia uwezekano wa kusambaza teknolojia na mbinu zilizotumika katika kijiji cha millennia cha Mbola mkoani Tabora, zitumike katika vijiji vingine
hapa nchini.
Watanzania watakiwa kutii mamlaka zilizopo serikali
Na Florah Temba,
Moshi
WATANZANIA wametakiwa kujituma katika kazi ikiwa ni pamoja na kutii mamlaka zilizopo katika serikali na hata kwenye dini, hatua ambayo itasaidia kudumisha amani na mshikamano ulioachwa na hayati mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
DC ataka mazungumzo kuhusu gesi
Na Godwin Msalichuma, Mtwara
MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, amesema upo umuhimu wa kuzungumza na wananchi wa kada mbalimbali mkoani humo kuhusu suala la gesi ili kuleta utulivu na amani katika halmashauri zote za Mkoa huo.
Serikali kuendelea kushirikiana na Misri kuboresha huduma ya maji
Na Jovin Mihambi, Maswa
WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amesema,
serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Watu wa Misri katika kuboresha huduma ya maji hususani kwa wananchi waishio kwenye vijiji ambavyo vimekuwa vikikumbwa na janga la ukame ili waweze kupata maji
salama.
Wafanyabiashara wasiotumia mashine za kieletroniki kuchukuliwa hatua
Na Severin Blasio,Morogoro
MALAKA ya mapato Tanzania (TRA) itawachukulia hatua wafanyabiashara waliosajiliwa
kwenye ongezeko la thaman (VAT) watakaobainika kutotumia mashine za kielektroniki
zinazotoa risiti kwenye biashara zao.
MALAKA ya mapato Tanzania (TRA) itawachukulia hatua wafanyabiashara waliosajiliwa
kwenye ongezeko la thaman (VAT) watakaobainika kutotumia mashine za kielektroniki
zinazotoa risiti kwenye biashara zao.
ZECO yaaswa kutoa huduma bora
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
UONGOZI wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO)limeaswaa kuwa makini katika taratibu zake za kutoa huduma bora kwa lengo la kupunguza kero na lawama kutoka kwa wateja wa huduma hiyo.
18 January 2013
Shibuda achoshwa na vitisho Chadema *Sasa kuanika siri ya mgogoro unaondelea kufukuta *Adai chama hicho hakina mvuto tena Kanda ya Ziwa
Na Benedict Kaguo
MBUNGE wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda (CHADEMA), anakusudia kuuweka wazi mgogoro unaondelea ndani ya Chama hicho.
Mchina jela miaka 3 akimpa rushwa DC
Na Raphael Okello, Bunda
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, imemuhukumu raia wa China, Bw. Mark Wang Wei (30), kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh. 700,000, baada ya kutiwa hatiani na kosa la kutaka kutoa rushwa ya sh.500,000 kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Bw. Joshua Mirumbe.
JK amtembelea DCI Manumba, bado kalazwa ICU
Na Goodluck Hongo
RAIS Jakaya Kikwete, jana alikwenda kumjulia hali Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi nchini, DCI Robert Manumba, ambaye amelazwa katika chumba cha watu mahututi (ICU), kwenye Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam.
Lema kutoshirika ziara za Kikwete
Na Martha Fataely, Moshi
SAKATA la kukataliwa kwa Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Gaudence Lyimo, sasa limekuchukua sura mpya baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema (CHADEMA), kutangaza nia yake ya kutoshiriki ziara za Rais Jakaya Kikwete, mkoani humo kama
Bw. Lyimo atakuwepo.
TIC 'yakalia kuti kavu' kwa Kamati ya Zitto
Mariam Mziwanda na Rehema Maigala
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imetoa siku moja kwa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), kuandika barua ya ufafanuzi juu ya uwekezaji katika mkataba wa Star Media.
Bodi TANAPA sasa kuburuzwa mahakamani
Na Daud Magesa, Mwanza
WANANCHI wa vijijji saba vya kata mbalimbali, katika Wilaya
ya Serengeti, mkoani Mara, wanakusudia kuiburuza Mahakamani
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi
za Taifa (TANAPA), kwa madai ya kupora maeneo yao.
KERO
Mkazi wa jiji akipita karibu na lundo la matawi ya miti yaliyotelekezwa kwa zaidi Wiki moja katika makutano ya Mtaa wa Mosque na Mshihiri Posta, Dar es Salaam jana. Ukataji wa miti na kuachwa katika barabara pamoja na kuchafua mazingira pia unasababisha kero kwa watumiaji wa barabara hizo. Picha na Peter Twite)
Katibu CCM achunguzwa na TAKUKURU
Na Patrick Mabula, Kahama
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, inamchunguza Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), wilayani humo, Bw. Masoud Melimeli.
Polisi Kishapu watupiwa tuhuma nzito
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
BAADHI ya viongozi katika Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, wamelitupia lawama Jeshi la Polisi, wilayani humo kutokana na baadhi ya askari wake, kudaiwa kushirikiana na wahalifu pamoja
na kupokea rushwa.
Uhamiaji yakamata wahamiaji 234
Na Wilhelm Mulinda, Mwanza
IDARA ya Uhamiaji, mkoani Mwanza, imewakamata wahamiaji haramu 234 kwa nyakati tofauti mwaka 2012 wengi wao wakiwa
raia wa nchi ya Congo (DRC), pamoja na Burundi.
Nchemba ahofia ajira za wabunge CHADEMA
Na Benedict Kaguo
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Bara, Bw. Mwigulu Nchemba, amefichua siri ya kutoyaweka bayana majina ya wabunge saba
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walioomba kujiunga na chama chao.
TCRA
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za mitandao ya simu Tanzania wakisikiliza maoni mbalimbali, Dar es Salaam jana, kuhusu utozaji wa viwango sawa kwa upigaji simu kwa mitandao yote nchini ifikapo Mwezi Machi mwaka huu. (Picha na Charles Lucas)
Katiba Mpya iwabane na kukomesha uzembe kwa watendaji
Taasisi na viongozi mbalimbali waliopo serikalini na wastaafu,
wapo katika mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya kwa
Tume anayoratibu mchakato huo jijini Dar es Salaam.
16 January 2013
Bilal: Vifo vya uzazi nchini vimepungua
Na Queen Lema, Arusha
IDADI ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini, vimepungua kwa asilimia 50 ukilinganisha na mwaka 2009 ambapo takwimu zinaonesha wajawazito 500 walipoteza maisha ambapo
mwaka 2010, vifo hivyo vilipungua na kufikia 250.
Wananchi Shy wampa ushauri JK
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Shinyanga, Bw. Deogratias Saimon, amemuomba Rais Jakaya Kikwete, aombe
ushauri kwa Rais wa Marekani, Bw. Barrack Obama, kuhusu
mbinu mbadala za kupambana na ugonjwa wa malaria nchini.
Dkt. Slaa awapa 'rungu' madiwani
Na Martha Fataely, Moshi
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amewahamasisha madiwani wa chama hicho Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumfungia nje ya ofisi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bi. Bernadette Kinabo.
Mtemvu atoa ushauri kwa Mahakama
Na David John
MBUNGE wa Temeke, Dar es Salaam, Bw. Abbas Mtemvu, amezishauri mahakama nchini kuharakisha usikilizaji wa kesi
za watu waliojenga na kuzuia mifereji ya maji machafu.
Rais Kikwete awahakikishia ulinzi Mabalozi
Na Kassim Mahege
RAIS Jakaya Kikwete, amesema Tanzania itaendelea kuimarisha ulinzi kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini pamoja
na kuzikabili changamoto zilizojitokeza mwaka 2012.
Wakulima wapewe elimu ya kilimo cha kisasa
KILIMO kwanza ni mpango unaotekelezwa na Serikali ili kuhamasisha wakulima waongeze juhudi kwenye kilimo cha kisasa, kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.
15 January 2013
MAANDAMANO
Mamia ya Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Mwalimu Nyerere Kivukoni wakiwa katika Kivuko cha Mv Kigamboni, kabla ya kuandamana jijini jana. Wanachuo hao waliandamana kupinga vitendo vya unyanyasaji wa aina mbalimbali ukiwamo wizi unaofanyika vyuoni. (Picha na Heri Shaaban)
JK: Mapinduzi Z’bar yamefungua fursa ya elimu kwa Wazanzibari
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RAIS Jakaya Kikwete amesema, miongoni mwa faida ambazo zimetokana na Mapinduzi ya Zanzibar ni kupatikana kwa fursa
ya elimu kwa wazawa pamoja na watoto zao.
Ajali ya basi yaua saba, yajeruhi 28
Robinson Wangaso na Veronica Modest, Mara
WATU saba wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso katika Barabara Kuu ya Mwanza, Kijiji cha Nyatwari, wilayani Bunda, mpakani mwa Mkoa wa Mara na Simiyu.
Masaburi: Watendaji wanakula fedha za mapato
Na Anneth Kagenda
FEDHA nyingi zinazokusanywa katika taasisi mbalimbali za umma, asilimia tano ya mapato imekuwa ikichukuliwa na watendaji wa kawaida na wale wakubwa wanachukua mara tisa ya fedha hizo.
Bilali kufungua mkutano wa afya leo
Na Queen Lema, Arusha
MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, leo anafungua mkutano wa kimataifa wa Afya ya Mama ambao utahusisha washiriki kutoka zaidi ya nchi 68 wakiwemo wanasiasa.
Wananchi wamshukia DC K'ndoni
Na Gladness Theonest
WAKAZI wa Mbezi Beach, eneo la Salasala, Dar es Salaam, wamemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Fotnatus Fwema, kutokutumia cheo chake kukandamiza wananchi wanyonge.
USAFI
Mkazi wa jiji akisafisha daladala lililokuwa katika foleni, kama alivyokutwa makutano ya Barabara za Nyerere na Msimbazi (KAMATA), Dar es Salaam jana. Baadhi ya vijana wamebuni njia ya kujipatia kipato kwa kusafisha magari yakiwa barabarani ingawa hufanya hivyo bila makubaliano na mhusika. (Picha na Charles Lucas)
Wahamiaji 21 wakamatwa Kilimanjaro
Na Florah Temba, Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wahamiaji haramu 21 kutoka nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuingia
nchini kinyume cha sheria.
Afa kwa kuangukiwa na kifusi mgodini
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti yaliyotokea mkoani Shinyanga, likiwemo la msimamizi wa machimbo ya madini ya dhahabu, Wilson Mapengo (28), kuangukiwa na kifusi cha udongo akiwa katika shughuli za kukagua mashimo.
Mbaroni akidaiwa kumbaka, kumlawiti mzazi mwenzake
Na Jamillah Daffo, Babati
JESHI la Polisi mkoani Manyara, linamshikiliwa mkazi wa Kijiji cha Gijachameda, Wilaya ya Babati, Bw. John Barandi (35), kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzazi mwenzake Mwanaisha Iddi
(25), baada ya kumbaka na kumlawiti.
MALALAMIKO
Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki za Kubeba Abiria 'Bodaboda' mkoani Mbeya, Bw. Idd Ramadhan, akizungumza na Wanachama wa umoja huo jana, wakati wa kutoa tamko kuhusu kusudio la kutaka kumpeleka kumshtaki Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kutokana na madai kuwa aliwatuhumu kupewa rushwa, Bw. Joseph Mbilinyi. Kushoto ni Katibu wa umoja, Bw. Ernest Mwaisango. Picha na Charles Mwakipesile
Diwani CCM afikishwa kortini akihusishwa na mauaji Musoma
Na Raphael Okello, Musoma
WATU wanne akiwemo Diwani wa Kata ya Mugango, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Wandwi Kunju (34), mkazi wa Mugango, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, jana wamefikishwa mahakamani akidaiwa kujihusisha na mauaji ya mtu mmoja.
Adondoka kutoka juu ya Mnazi
Christina Mokimirya na Lead Daudi
MKAZI wa Mkuranga, mkoani Pwani, Mwarami Shamte (32), amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Mifupa (MOI) baada ya kudondoka kutoka juu ya mnazi na kuumia sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mafunzo kwa waendesha pikipiki yatapunguza ongezeko la ajali
HIVI karibuni, usafiri wa pikipiki mijini na vijijini katika mikoa mbalimbali nchini, umeongezeka kwa kasi kubwa.
SAMAKI
Wafanyabiashara katika Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, Juma Khamis (kushoto) na Bw. Said Ally, wakiwa wamembeba samaki aina ya Kitoga wakimpeleka katika mnada kwa mauzo, kama walivyokutwa na mpigapicha wetu, Dar es Salaam jana. Kwa maelezo ya wafanyabiashara hao samaki huyo walitarajia kumuuza kwa sh. 60,000. (Picha na Peter Twite)
Serikali yakiri haijatenga ardhi ya kilimo, ufugaji
Na Peter Mwenda
SERIKALI imekiri kuwa haijatenga ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji kama ilivyotengwa kwa ajili ya wanyama pori.
Wavamizi pori Mbangara watiwa mbaroni
Na Esther Macha,
Mbeya
WATU watano jamii ya wafugaji wanashikiliwa na Polisi Wilayani Chunya mkoani Mbeya wakituhumiwa kuwashawishi wafugaji wenzao kuwavamia maofisa wa Halmashauri hiyo waliokowa wakiendesha zoezi la kuwaondoa wafugaji waliovamia hifadhi ya misitu katika pori la Mbangara wilayani humo.
14 January 2013
Walemavu wakiwezeshwa vitendea kazi watajikwamua kiuchumi
Na Lilian Justice
IMANI potofu kuwa mlemavu katika familia ni mkosi ni moja ya chanzo cha kuwatenga na kuwanyima huduma muhimu watu wenye mahitaji maalumu.
MSAADA
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro, Bw. Amos Makalla (katikati) akipeana mkono na muuguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Matale wilayani humo mwishoni mwa wiki (wa pili kulia), baada ya kukabidhi vitanda viwili na matandiko kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa. Wengini ni baadhi ya viongozi wa kijiji hicho. (Na Mpigapicha Wetu)
Mbunge atoa msaada wa shuka za mil. 17.5/-
Na Mwandishi Wetu, Geita
MBUNGE Viti Maalumu, mkoani Geita, Bi. Josephine Chagula (CCM), ametoa msaada wa shuka 400, kwa Hospitali za Wilaya
mkoani humo, zenye thamani ya sh. milioni 17.5, kwa ajili ya
wanawake wajawajito waliolazwa katika hospitalini hizo.
Slaa kuanza ziara ya kichama K'njaro leo
Na Martha Fataely, Moshi
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, anatarajiwa kufanya ziara
ya siku mbili mkoani Kilimanjaro kuanzia leo kwa ajili ya
kuelezea mafaniko ya chama na shughuli za mwaka 2013.
RAIS
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiangalia vitabu katika maktaba ya Shule Mpya ya Sekondari Mlimani Matemwe, iliyopo Zanzibar muda mfupi baada ya kuifungua rasmi jana. Kulia ni Ofisa mwandamizi kutoka Ofisi ya Benki ya Dunia nchini anayeshughulikia masuala ya elimu Bw. Nobuyuki Tanaka na kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Mohamed Mzee (Picha na Freddy Maro)
RC aagiza ujenzi wa mabweni ya askari
Na Daud Magesa, Simiyu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Pascal Mabiti, ameuagizi uongozi wa Jeshi la Polisi mkoani humo, kujengwa kwa mabweni mawili ambayo wataishi askari polisi ambao hawajao.
Serikali yatoa chakula cha msaada Igunga
Na Abdallah Amiri, Igunga
SERIKALI imetoa chakula cha msaada tani 1,790 za mahindi katika Wilaya ya Igunda, mkoani Tabora na fedha sh. milioni 89,700 ili kiweze kusambazwa kwa wananchi wilayani humo.
UZUNDUZI DARAJA
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda, (wa pili kulia) akiongozana na wakazi wa eneo la Mbezi Ndubwi, kwenda eneo la uzinduzi wa ujenzi wa daraja kwenye eneo hilo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni baadhi ya viongozi wa manispaa. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira wa Manispaa hiyo. Diwani wa Kata ya Kigogo, Richard Chengula. (Picha na Charles Lucas)
Katiba Mpya itoe adhabu kwa wanaokataa kuwatambua viongozi wanaochaguliwa
Na Suleiman Abeid
MFUMO wa uongozi nchini unaundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2005 ambapo viongozi wake hupatikana kwa njia ya kidemokrasia kwa kuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura.
Tupinge mauaji ya raia wasio na hatia kulinda amani nchini
Na Daniel Samson
HAKI za binadamu ni moja ya mambo muhimu ambayo sheria na taasisi za kimataifa za haki za binadamu zinasisitiza kuwepo kwa usawa na haki miongoni mwa watu wa jamii mbalimbali.
Suala hili linatekelezwa kwa mitazamo tofauti na watawala katika nchi mbalimbali kutokana na mfumo wa sheria unaoongoza nchi.
Lugha kali za wauguzi kwa wagonjwa zikomeshwe
Na Esther Macha
KAMA nguzo ya familia, mwanamke anatakiwa kuheshimiwa na kuthaminiwa kutokana na majukumu yake ili kufanya vizuri zaidi.
Wanatakiwa kupewa nafasi ya pekee ili kuwapa nguvu zaidi ya kusimamia waliyoanzisha kwa manufaa ya jamii.
Ongezeko la majengo si maendeleo ambayo tunayahitaji
WATAWALA na baadhi ya wananchi, wanatumia nguvu kubwa kufafanua maendeleo kwa kuyahusisha na ongezeko majengo ya kifahari na magari barabarani.
Miaka ya 1980, mashirika ya misaada yalifanya jitihada kubwa za kuhamasisha maendeleo na kuongeza misaada kwa nchi maskini.
MSAADA
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Star Media Tanzania, Bw. David Kisaka, akimkabidhi mgonjwa Abubakar Ramadhani mkazi wa Manzese Tip Top, king'muzi, Dar es Salaam jana kwa niaba ya wagonjwa wengine wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Mwananyamala. Kampuni hiyo imetoa seti za runinga na ving'amuzi zitakazotumika katika wadi mbalimbali za wagonjwa katika hospitali hiyo. Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu, Dkt. Kariamel Wandi na Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo. Bw. Elic Sprian. (Picha na Charles Lucas)
Subscribe to:
Posts (Atom)