Na
Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania
(TANESCO) Mkoa wa Temeke limethibitisha kuwa Kituo cha Polisi Tandika, Azimio
(Vyaniza) jijini Dar es Salaam, kimekuwa
kikiibia Serikali malipo ya ankara
za umeme kutokana na hujuma iliyofanyika kituoni hapo kwa kuwaunganishia umeme
baadhi ya wafanyabiashara kinyume cha sheria. Hayo yalithibitishwa jijini Dar
es Salaam jana na Meneja wa TANE S CO Mk o a wa Temeke, Richard Mallamia,
wakati akizungumza na maofisa waliotumwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, ili kujiridhisha kuhusiana na hujuma hiyo kutokana na habari
iliyochapishwa na gazeti la Majira, Jumamosi iliyopita.
Mallamia
aliwaambia maofisa hao kuwa ni kweli umeme umekuwa ukiibiwa kupitia kituoni
hapo na kusambazwa kwa wafanyabiashara (majina tunayo). Kwa mujibu wa uchunguzi
wa Majira, wafanyabiashara hao kila mwezi walikuwa wakilipa sh. 30,000 kwa
kituo hicho na kuingia kwenye mifuko ya waliohusika kusuka mpango huo. "
Tume t h i b i t i s h a umeme umekuwa ukisambazwa kinyume cha taratibu kwa
wafanyabiashara, lakini tunaoibiwa sio TANESCO bali polisi wanaiibia Serikali
ambapo wizara husika inatumia fedha za walipa kodi kulipa bili za umeme za
Jeshi la Polisi," alisema.
Alifafanua kwamba
kitendo cha polisi kuwasambazia umeme wafanyabiashara hao ni hatari kwakuwa
waya umepitishwa chini ya ardhi, jambo ambalo linaweza kusababisha maafa
makubwa kwa wapita njia.
Wakati wawakilishi
hao wa waziri wakifanya ukaguzi kituoni hapo na kwenye maeneo ya biashara
walikuta tayari mfumo wa kusambaza umeme uliokuwa umeunganishwa awali
umefumuliwa ili kuficha ushahidi.
Hata hivyo maofisa
hao baada ya kufuatilia kwa undani walibaini kufanyika hujuma hiyo, huku baadhi
ya wafanyabiashara waliokuwa wame u n g a n i s h iwa umeme wakishikwa
kigugumizi kujibu maswali waliyokuwa wanaulizwa.
Mmoja wa watu
wanaotajwa kuhusika kwenye hujuma hiyo (jina tunalo) alipoulizwa na maofisa hao
kutoka wizarani alikataa hujuma hiyo kufanyika. Lakini alipooneshwa jinsi
hujuma hiyo ilivyokuwa ikifanyika baada ya kuchimba chini ya ardhi na kukuta
waya unaotoka kituoni hapo na kuingia kwa wafanyabiashara hao, alipatwa na
kigugumizi na kuanza kutokwa machozi.
Mkuu wa kituo hicho,
Mohamedi Jaf Khamisi, alipoulizwa na maofisa hao, alisema ana wiki tatu tangu
ahamishiwe kituoni hapo, hivyo hafahamu kitu chochote.
Aliongeza kuwa tayari
taarifa za suala hilo
ameziandikia maelezo na kuziwasilisha kwa Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Temeke,
Engelbert Kiondo.
Kwa upande wake
Kamanda Kiondo, alisema ana ripoti iliyoandaliwa na wahandisi wa TANESCO
waliokwenda kukagua awali mara baada ya taarifa hiyo ya wizi wa umeme
kuchapishwa gazetini ambayo haioneshi tuhuma zozote za kuibwa umeme katika
kituo hicho.
"Uc h u n g u z
i u l i o f a n ywa na wahandisi wa TANESCO haukuonesha kasoro zozote, na hivi
sasa jalada lake linakaribia kukamilika, hivyo sisi tunaifanyia kazi ripoti
hiyo," alisema na kuongez a; " hiyoripo tinyin gine(yamaofisawawaz
iri)nd iyokwa nza naisikia kutoka kwako.".
NayeMkaguzi kutoka
Kanda ya Pwan i, Ch ristian Simon, alisema kituochapolisikinauzaumemewakati wiz
arainap ata hasarakwa kulipabiliamb ayosiosahihi.
Ali semawames hawa andi kiafomuya u
kaguzikwaajiliya kuangalia mfumo wa bili halafu hatua stahiki zitafuata.
HAO NDIYO POLISI WETU CHEZEA POLISI WEWE!
ReplyDeleteBAADHI YA POLISI NI HATARI KULIKO MARALIA