16 July 2013

WENGER BADO AWEWESEKA NA SAINI YA SUAREZ London, Uingereza
WASHIKA bunduki wa Kaskazini mwa London nchini England, klabu ya Arsenal wamejipanga tena kutuma ofa ya pauni milioni 35 wiki hii ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, raia wa Uruguay, Luis Suarez.
Suarez amekuwa chaguo namba moja kwa kocha wa Arsenal majira haya ya kiangazi ya usajili barani Ulaya, Mfaransa, Arsene Wenger na sasa anaandaa kitita hicho ingawa Liverpool walisema kama anataka kumsajili nyota huyo anatakiwa kulipa ada ya uhamisho ya pauni milioni 40.

Awali Wenger alituma ofa ya pauni milioni 30 na Liverpool wakakataa, sasa wiki hii ameongeza pauni milioni 5 na kufikia 35, lakini sijui kama Liver watakubali kwani walishasema wanahitaji 40 na si vinginevyo.
Mashabiki wa Arsenal wana imani kubwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye matatizo makubwa nchini England ataweza kuwasili Emirates, na wanataka kitita cha pauni milioni 70 alichopewa Wenger kwa ajili ya usajili kitumike kumleta Kaskazini mwa London.
Wenger yupo katika presha kubwa ya kusajili wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kutokana na klabu hiyo kusema kuwa kwa sasa ina uwezo wa kushindana katika soko la kutafuta wachezaji ghali zaidi  duniani.

No comments:

Post a Comment