Na Pamela Mollel, Arusha
KAMPUNI za madini hapa nchini zimetakiwa kulipa kodi ikiwemo
ile ya faida ili Serikali iweze kupeleka huduma za msingi katika maeneo
yaliyopo pembezoni mwa migodi.M a e n e o a m
b a y o yalielezwa kwa asilimia kubwa yameachwa nyuma kimaendeleo. Hali hiyo
inadaiwa inatokana na kampuni nyingi pindi zinaporidhia kuwekeza katika maeneo
hayo kuahidi mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, vituo vya afya na
maji bila mafanikio
. Rai hiyo
ilitolewa hivi karibuni jijini Arusha na mwakilishi wa Kamati ya Utekelezaji
Kupitia Taasisi ya Tanzania Extractive Industry Tranparent Initiative (TEITI),
Buberwa Kaiza kwa niaba ya Jaji Mark Bomani wakati akizindua ripoti ya utafiti
wa uwajibikaji wa makampuni kwa jamii ya sekta ya madini hasa Tanzanite.
Buberwa alisema
kuwa, kama makampuni ya madini yangekuwa yanalipa kodi basi serikali ingepata
fursa kupeleka huduma zote muhimu ikiwemo kujenga barabara, hospitali, shule
huku akidai kuwa eneo kama Mererani lisingekuwa maskini ilhali linatoa madini
ya Tanzanite.
"Ripoti
iliyofanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mererani na kuwashirikisha
wachimbaji wadogo wadogo wengi wamelalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu
unaofanywa na wawekezaji kama kuwafungulia maji ndani ya mashimo, kuuawa kwa
wachimbaji," alisema Buberwa.
Alisema kuwa,
katika ripoti moja ya kamati hiyo kuna kampuni moja ya madini haikulipa kodi
kutokana na kudai kuwa ilipata hasara hivyo inafidia kwanza hasara ndiyo ilipe
kodi jambo ambalo alisema huwezi kulikuta katika nchi za wenzetu.
Kwa upande wake
Katibu wa Muungano wa Asasi Zisizo za Kiserikali Arusha Angonet, Peter Bayo
ambayo ndiyo waandaaji wa ripoti hiyo alisema kuwa, utafiti huo umechukua
takriban miezi 3 na ulifanyika Mererani.
Alisema kuwa,
kubwa katika utafiti huo ni kutengeneza mfumo wa kuwezesha uwajibikaji wa
kampuni kwenye jamii ikiwa ni pamoja na jamii kunufaika na rasilimali
zinazopatikana.
"Uwe p o wa uwa z i katika
mikataba pamoja na mapato kuwa ni kiasi gani kinapatikana...wananchi wanahaki ya
kufahamu hayo yote," alisema Bayo
Pia alieleza lengo la utafiti huo kuwa
ni kuangalia hali ya mchango wa shughuli za uchimbaji wa madini aina ya
Tanzanite katika maendeleo ya jamii, uhifadhi na utunzaji wa mazingira, usalama
wa haki za binadamu na uwazi katika masuala ya kodi.
Mmoja wa waalikwa katika uzinduzi huo
ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Hakimadini, Amani
Mhinda akichangia mada alisema kuwa utafiti huo ni muhimu sana na umekuja
wakati ambapo kuna mjadala mkubwa kuhusu jinsi gani nchi ya Tanzania itafaidika
na rasilimali zake
"Utafiti
huu unatoa ushahidi kwa wananchi na serikali za mitaa kufahamu athari za
uwekezaji ili kushawishi serikali kuu kuboresha sera za uwekezaji katika sekta
ya madini," alisema Mhinda.
No comments:
Post a Comment