Na Damiano Mkumbo, Singida
WATU watano wamejeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji
cha Kitukutu, Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba Mkoa wa Singida barabara Kuu
ya Singida Nzega.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alieleza kuwa watu
hao walijeruhiwa katika ajali hiyo Julai 14 baada ya gari aina ya Scania T 922
BUC/T539 BUH kugongana na Fuso T 748 BCM.
Kamwela aliwataja majeruhi hao ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Iramba Kiomboi kuwa ni pamoja na Mustafa Mohamed (43),mkazi wa Sanya
juu, dereva wa Fuso na Msilumi Emmanuel (21) mkazi wa Ubungo Dar es Salaam,
wote wakiwa na majeraha usoni.
Alisema wengine ni Swalehe Idd (21), utingo wa Fuso mkazi wa Kilimanjaro
aliyevunjika miguu yote miwili na kuwa na majeraha usoni, Leila Mohamedi (40),
mkazi wa Chanika Dar es Salaam na Aley Simba (32) wa Mbezi Beach ambao wote
wamepata maumivu na michubuko mikononi, mabegani, kifuani, kiunoni na miguuni.
Akizungumza
kuhusu ajali hiyo na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Kamanda Kamwela
alibaini kuwa lori hilo lililokuwa likiendeshwa na Nicodemus Hanery lilitokea
Uganda kuelekea jijini Dar es Salaam wakati gari jingine aina ya Fuso lilikuwa
likiendeshwa na Mustafa Mohamed lilitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.
"Chanzo
cha ajali ni mwendokasi wa dereva wa Fuso ambaye alijaribu kupishana na lori
hilo lililokuwa na trela kati sehemu isiyoruhusiwa kitendo kilichosababisha
magari hayo kugongana uso kwa uso."
Aliongeza kuwa
majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Kiomboi na hali zao
zinaendelea vizuri na dereva wa Fuso yupo chini ya ulinzi na anatarajiwa
kufikishwa mahakamani mara taratibu zitakapo kamilika.
"Kutokana na tukio hilo nina
washauri madereva wanapokuwa barabarani kuendesha magari yao kwa kuzingatia
sheria za usalama wa barabarani na kuwajali watumiaji wengine wa barabara
No comments:
Post a Comment