23 July 2013

WANANCHI WACHANGIA MILIONI 10/- KUJENGA MADARASA Na Patrick Mabula, Kahama
MA K A M U Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama, Tabu Katoto amewa t a k a wa n a n c h i wa s i bwe t e k e k a t i k a kuchangia huduma za kijamii ili kuharakisha maendeleo. Wito huo aliutoa wiki iliyopita katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu katika sekondari ya Kata ya Igunda ambapo wananchi wa kata hiyo waliweza kuchanga kiasi cha shilingi milioni 10.5.

Katoto aliwataka wananchi kuendelea kuwa na moyo wa kuchangia maendeleo katika huduma za kijamii hali itakayosaidia kuharakisha maendeleo kwenye maeneo yao. Katoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Igunda ambayo haina shule ya sekondari aliwapongeza wananchi kwa hatua waliyofikia ya kujenga na kukamilisha vyumba vitatu vya madarasa na nyumba moja ya mwalimu kwa nguvu zao ambavyo hadi sasa wametumia kiasi cha shilingi milioni 18 .
Kwa upande wake mgeni rasmi katika harambee hiyo Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli aliyechangia kiasi cha shilingi milioni tatu na bati 100 kwa ajili ya kuezeka boma la nyumba ya walimu iliyojengwa kwa nguvu ya wananchi. Akiongea katika harambee hiyo Lembeli alitoa onyo kwa watendaji wa vijiji na kata kuacha mara moja kuchakachua na kutafuna michango ya wananchi hali ambayo imekuwa ikiwavunja moyo na kuwakatisha tamaa katika suala la kujiletea maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu, Juma Kimisha katika kuunga mkono jitihada hizo za wananchi, alitoa jumla ya mifuko ya saruji 15, huku ofisa toka ofisi ya CAG, Elias Kuandikwa ambaye ni mzaliwa wa kata hiyo aliwachangia kiasi cha shilingi milioni moja taslimu.

No comments:

Post a Comment