Na Darlin Said
WANAFUNZI 10 wa Kitivo
cha Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), wamepata udhamini wa masomo ya
shahada ya kwanza chuoni hapo kwa lengo la kuongeza wataalam wa masuala ya
madini na mafuta nchini.
Udhamini huo kwa wanafunzi hao umetolewa na kampuni
inayojishughulisha na masuala ya mafuta na gesi ya Swala Oil and Gas Tanzania
Limited (Swala) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni hiyo, Dkt. David Ridge,wakati akitangaza udhamini huo ambao ulitangazwa
Juni, mwaka huu.
"Tumefurahi kupata wanafunzi h awa amb a o t u n a t a r a j
iwa kuwadhamini waliojitokeza kuomba msaada wetu walikuwa wengi ila
tumezingatia wale waliofaulu kwa kiwango cha juu katika matokeo yao ya kidato
cha sita katika masomo husika," alisema Dkt. Ridge.
Aliwataja wanafunzi hao kuwa pamoja na Joel Haule, Robert Kisimbo,
Andrew Marong, Denis Muhoka, Rafael Ngole, Levina Pangani, Lucy Pangani,
Emmanuel Rajabu, Anita Ringia na John Sospeter.
Naye Mkuu wa Idara ya Jiolojia UDSM, Dkt. Shukrani Manya, alisema
msaada uliotolewa na Kampuni ya Swala kwa wanafunzi hao utasaidia kusoma na
kufanikiwa kupata shahada yao ya kwanza.
"Ms a a d a h u u mb a l i n a kuwawezesha kupata shahada yao
ya kwanza, pia utasaidia katika kuwajengea uwezo wao hasa katika masuala ya
mafuta na gesi katika sekta ndogo ndogo ambako ndio maendeleo ya Watanzania
yanapotokea," alisema.
Alisema uamuzi wa
kampuni hiyo utasaidia kujenga ushirikiano baina ya vyuo vikuu vya Tanzania na
sekta binafsi za madini.
No comments:
Post a Comment