Na Fatuma Rashid
WANACHAMA wa Klabu ya Simba, wamewashtaki v i o n g o z i wa
o kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kutaka wapewe adhabu kwa
madai kwamba wamevunja kanuni za Mkutano Mkuu wa mwaka.Mkutano huo
ulifanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi
Oysterbay, Dar es Salaam.
Hata hivyo,
mkutano huo uliingia dosari, baada ya baadhi ya wanachama kupinga ajenda ya
mpango mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo, ingawa Mwenyekiti wa Simba Aden Rage
alifanikiwa kuzima vurugu hizo kwa kushirikiana na polisi na mabaunsa.Akizungumzia
sakata hilo Dar es Salaam Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema amepokea
barua kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba, wakilitaka shirikisho
hilo kuwaadhibu viongozi wa klabu wakidai viongozi hao wamevunja masharti ya
mkutano huo.
Lakini Osiah alisema TFF aihusiki kwa
lolote katika hilo na wanashangaa kupelekewa mzigo na wanachama kutaka
kuwaadhibu viongozi wao.“Klabu yoyote inapokuwa na mkutano, TFF
hatuhusiki sasa linapokuja suala la kutokuelewana tunashangaa tunapopewa mzigo
na wanachama, ili tuwaadhibu viongozi wao,” alisema.
Aliongeza kuwa wanachama hao inawabidi
waombe Mkutano wa Dharura, ili waweze kuelewana vizuri na viongozi wao na kama
wakishindwa kuelewana, basi waangalie katiba inasemaje.Katika mkutano huo uliofanyika muda mfupi, Rage aliwaahidi
wanachama wa Simba hasa waliokuwa wakiupinga uongozi wake kwamba wataitisha
mkutano wa dharura Novemba mwaka huu pamoja na kuzungumzia kuuzwa kwa Emmanuel
Okwi nchini Tunisia.
No comments:
Post a Comment