23 July 2013

WAKIMBIZI 11,000 WAUGUA MALARIA


Na Grace Ndossa
CHAMA cha Msalaba Mwekundu Tanzania ( R E D C R O S S ) kimesema kuwa kati ya Januari hadi Aprili mwaka huu wakimbizi 11,000 wanaoishi katika Kambi ya Nyarugusu iliyopo Kigoma wameripotiwa kuugua kutokana na ugonjwa wa malaria.Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na rais wa chama hicho, Dkt. George Nangale alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugawaji wa vyandarua vya mbu katika Kambi ya Nyarugusu iliyopo Kigoma.

Alisema kuwa, kutokana na tatizo hilo kwa kushirikiana na serikali pamoja na vyama vingine watazindua mradi wa kugawa vyandarua kwa kambi hiyo ambayo ina wakimbizi zaidi ya 680,000.“Tafiti zinaonesha katika kipindi cha miezi minne tangu Januari hadi Aprili, mwaka huu wakimbizi wanaoishi Kambi ya Nyarugusu Kigoma wameripotiwa k u u g u a u g o n jwa wa malaria ambapo, watoto na wanawake wajawazito ndiyo wanaoathirika kwa kiasi kikubwa,” alisema Dkt. Nangawe.
Alisema, mradi huo utazinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Issa Machibya Julai 30 mwaka huu na vyandarua vitagawiwa Julai 31 mwaka huu.Alisema kuwa ni pamoja na vijana 100 ambao watakuwa wanapita nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kuhamasisha utumiaji wa vyandarua hivyo ili waweze kujilinda na ugonjwa wa malaria.
Hata hivyo, alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa ugonjwa wa malaria unaua watu 700,000 duniani kila mwaka na Tanzania ni nchi mojawapo iliyoathirika na tatizo hilo Afrika.Pia, alisema chama hicho tangu mwaka 2002 wameweza kusambaza vyandarua milioni 16.5 na kukinga watu milioni 29.7 kwa ugonjwa wa malaria.

No comments:

Post a Comment