16 July 2013

WAAJIRI KUBURUZWA KORTINI


 Na Suleiman Abeid, Simiyu
CH A M A c h a Wa f a n y a k a z i wa Serikali Kuu na Afya nchini (TUGHE) kimetishia kuwashtaki waajiri wote wanaozuia kufanyika kwa vikao vya mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi yaliyoundwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kusudio hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Ally Kiwenge alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu katika ziara yake ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwahamasisha wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii.

Kiwenge alisema pamoja na mabaraza ya wafanyakazi kuundwa kwa mujibu wa sheria, lakini bado kuna baadhi ya waajiri ambao huzuia kufanyika kwa vikao vya mabaraza hayo na kwamba kitendo hicho ni kupingana na sheria za uanzishwaji wake.
"Mabaraza ya wafanyakazi yapo kwa mujibu wa sheria, wapo waajiri wanazuia yasifanyike na wengine wanakataza yasiundwe, s a s a n iwa e l e z e wa z i kwamba TUGHE tumeanza ufuatiliaji, mwajiri yeyote atakayebainika kuzuia vikao hivi kwa makusudi hatutasita kumshtaki, tutampeleka mahakamani.
"Wapo waajiri wanaodai kutopewa mafungu kwa ajili ya kuendeshea mabaraza hayo, sasa tunaiomba Serikali ihakikishe inatoa fedha kwa ajili ya vikao hivyo, na ninawaagiza makatibu wote wa TUGHE wa mikoa watoe taarifa za mwajiri ye yote atakayetajwa kuzuia kufanyika kwa v i k a o h i v y o k a t i k a sehemu zao za kazi, halafu waonetutakachokifanya," alisema Kiwenge.
Kwa upande mwingine k a t i b u m k u u h u y o a l i w a t a h a d h a r i s h a viongozi wa vyama huru vya wafanyakazi nchini k u t o k u b a l i k uwe kwa mifukoni na waajiri na kueleza kuwa vyama hivyo vimeundwa kwa mujibu wa sheria, hivyo wahakikishe wanatimiza wajibu wao katika kuwatumikia wanachama wao.
"Viongozi wa vyama vya wafanyakazi tuwe makini tusikubali kugawanywa na waajiri, wapo ambao hivi sasa wanadiriki kuwachagulia wafanyakazi wao vyama gani wajiunge navyo, hii ni hatari, tuache kugombania wanachama, kila chama kishughulike na wanachama wake kwa mujibu wa katiba yake," alisema Kiwenge.

No comments:

Post a Comment