22 July 2013

VOCHA ZA SIMU ZAMPELEKA JELA MAKA SITANa John Gagarini, Kibaha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoa wa Pwa n i imemh u k umu mkazi wa Miembe Saba wilayani Kibaha, Amosi Chacha (40) kwenda jela miaka 6 baada ya kukutwa na hatia ya wizi wa vocha za mtandao wa simu pamoja na kukutwa na mihuri bandia.Mtuhumiwa huyo alikutwa na hatia kwa makosa yote mawili yaliyokuwa yakimkabili katika kesi iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi, Aziza Mbadyo.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Emmanuel Maleko ameieleza mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na mihuri ya Ofisa Mtendaji Mtaa wa Kwesimu pamoja na wa Kituo cha Ukaguzi wa Maliasili cha Soni kilichopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga mnamo Juni 3, 2013 eneo la Sinza, Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mihuri hiyo katika usafirishaji wa mali asili kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam kwa lengo la kuweza kuvuka vizuizi vya maliasili vilivyopo kwenye barabara kuu.Aidha Maleko alieeleza mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Kibaha Mkoa wa Pwani akiwa na vocha za muda wa hewani zenye thamani ya sh. milioni 5 akizisafirisha kwenda Tanga akitokea Dar es Salaam. Mwendesha Mashtaka huyo wa Serikali aliongeza kuwa makosa yote hayo mawili alikutwa na hatia dhidi yake, Chacha anadaiwa kuyatenda kwa nyakati tofauti.
Akisoma hukumu hiyo kwa muda wa saa moja na nusu, Mbadyo alisema kuwa Mahakama imeridhika na maelezo ya upande wa Jamhuri hivyo imemtia hatiani Amosi Mwita Chacha kwenda jela miaka sita ambapo katika kosa la wizi wa vocha alihukumiwa miaka minne na kosa la kukutwa na mihuri bandia alihukumiwa miaka miwili hivyo adhabu zote mbili zitakwenda pamoja na atatakiwa kwenda Jela miaka sita.  

No comments:

Post a Comment