19 July 2013

VIONGOZI WASHAURIWA KUACHA UBINAFSI



Na Goodluck Hongo
VI O N G O Z I n c h i n i wameshauriwa kuacha ubinafsi wa kujali maslahi yao na badala yake wawatumikie wananchi ili kuyadhibiti makampuni makubwa yanayokwepa kulipa kodi kupelekea kushindwa kuwaondolea wananchi umaskini unaowakabili.Akizungumza na Majira jana Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kupambana na Matumizi Mabaya ya Rasilimali za Taifa (CFRI), Bw. Andendekisye Mwakabalula alisema tatizo la ukwepaji kodi linatokana na viongozi wengi kuangalia maslahi yao ikiwemo kutokuwa na utashi hivyo kupelekea kuongezeka kwa ukwepaji wa kulipa kodi na vitendo vya rushwa kuongezeka.

Alisema kama viongozi hawatabadilika basi tatizo hilo litaendelea kuwa kubwa na ifike mahali sasa wananchi waseme sasa basi ili kuwaondoa viongozi wote ambao wanashindwa kufuata misingi ya kazi zao na kusabisha kuongezeka kwa ukwepaji wa kulipa kodi na kuongezeka kwa rushwa.“Unajua sisi tumejikita zaidi katika utafiti kwani Serikali inapoteza mabilioni ya fedha kwa baadhi ya makampuni kukwepa kulipa kodi lakini hiyo yote inasababishwa na viongozi wengi kujali zaidi maslahi yao kuliko matatizo yanayowakabili wananchi kwani kama kila kiongozi angefuata misingi bora ya kazi tatizo la ukwepaji kodi na rushwa lisingeongezeka nchini,”alisema Bw.Mwakabalula.
Alisema ni vyema wananchi nao wakapewa elimu juu ya utoaji wa rushwa na ukwepaji wa ushuru kwani kitaalamu wafanyakazi wa kawaida wana uwezo mkubwa wa kubaini vitendo vya rushwa kwa asilimia 51.Kwa mujibu wa ripoti ya matumizi ya nafasi za kazi na madaraka kwa Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka 2012 inayotolewa na taasisi ya kupambana na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa (ACFE) inaonesha kuwa rushwa huanzia juu kwa viongozi na baadaye ndio huwahusisha watu wa ngazi za chini lakini viongozi ndio wahusika wakubwa kabisa wa rushwa kwa mujibu wa ripoti hiyo.Ripoti hiyo ilishauri kuwa ni lazima vitendo vya rushwa vizuiwe kwanza na ndipo ufumbuzi wa kuzuiwa ufanyike kutokana na kwamba wahusika wakubwa wa rushwa ni watu walio na vyeo vikubwa ambapo wao hutoa ama kupokea fedha nyingi katika kufanikisha masuala yao. Nayo ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2012 inaonesha kuwa asilimia 30 ya bajeti inaingia katika mifuko ya

No comments:

Post a Comment