17 July 2013

VIGOGO KUBURUTWA KORTINI LEO


Rachael Balama na Heri Shaban
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), leo inatarajia kuwaburuta mahakamani baadhi ya vigogo wa mashirika ya umma kujibu mashtaka yanayowakabili.
Vigogo hao walikuwa wafikishwe kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijni Dar es Salaam jana, lakini kutokana na baadhi ya taratibu kutokamilika watafikishwa mahakamani hapo leo asubuhi.
Mmoja wa maofisa wa TAKUKURU aliyezungumza na Majira kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini, alithibitisha taarifa za vigogo hao kuburutwa mahakamani leo
.
Hata hivyo, ofisa huyo alikataa kutaja majina na mashirika waliyokuwa wakifanyia kazi vigogo hao. Jana maofisa wa TAKUKURU walionekana mahakamani hapo wakihaha kukamilisha taratibu za kufikisha vigogo hao mahakamani, lakini
Dkt. Edward Hosea ilishindikana baada ya taratibu hizo kutokamilika.
Mmo j a wa ma o f i s a wa TAKUKURU aliyezungumza na gazeti hili jana mchana, alisema imeshindikana kuwafikisha mahakamani hapo jana na taratibu hizo zitaendelea leo.
Mmoja wa mawakili wa Serikali aliyezungumza na gazeti hili, alithibitisha kesi za vigogo hao kusajiliwa mahakamani hapo, lakini alikataa kutaja kesi hizo zinahusu watu gani na badala yake aliwaelekeza waandishi wa habari kwenda kuuliza ofisi za makarani.
Mmoja wa makarani alipoulizwa alijibu; "Nyie ni waandishi wa 10 kufika kuulizia suala hilo, lakini sina taarifa hizo, wakifikishwa mtawaona.

No comments:

Post a Comment