15 July 2013

UMEME WAANZA KUSAMBAZWA VIJIJINI


MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani "Marufu Profesa Maji Marefu" amesema wakala wa umeme vijijini (REA) tayari wameanza utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati hiyo katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo.
Maji Marefu aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Makweli Kata ya Vugiri huku akivitaja vijiji ambavyo REA watafikisha umeme kuwa ni Mkwakwani, Kwamzindawa na Gereza vilivyopo Kata ya Mnyuzi na Matalawanda, Kijango, Mbuyu huko katika Kata ya Magoma.

Mbunge huyo alivitaja vijiji vingine vitakavyofikiwa kuwa ni Makumba, Lusanga, Kibaoni, Kijungu Moto, Dindira, Vugiri, Darajani, Mgobe, Makumba, Kituo cha Afya Kwalukonge, Kitivo na kwenye miradi ya skimu za uwagiliaji Mombo,Kijango na Kwamazandu utekelezaji wake utafanyika katika mwaka huu wa fedha 2013/14.
Maji Marefu alisema upatikanaji wa miradi hiyo umetokana na ushawishi wake kwa bunge na viongozi wenzake kuisukuma Serikali ili kufikisha huduma hiyo kwa wananchi na kuweza kuharakisha maendeleo yao ambapo aliwasihi kuendelea kumpatia ushirikiano kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili.
"Ndugu zangu ninachotaka kusema maendeleo siwezi kuyaleta peke yangu, ni ushirikiano kati yangu mimi na ninyi wananchi kwa ushirikiano mlionipa nimebanana na wenzangu bungeni hadi Serikali kupitia REA baadhi ya vijiji sasa vinapata umeme," alisema.
Akizungumzia utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme ya REA, Maji Marefu alisema kwamba, utekelezaji wake tayari umeshaanza kwenye maeneo ya Magoma Mbuyu ambapo aliwaasa baadhi ya watendaji kutojihusisha na masuala ya kisiasa badala yake watekeleze majukumu yao kulingana na sheria na taratibu lengo likiwa kuharakisha upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.
Wakati mbunge huyo akiwasisitiza watendaji umuhimu wa kuzingatia kanuni na sheria katika utendaji wao tayari kumeibuka suala la watendaji wa halmashauri kukwamisha ujenzi wa madaraja katika tarafa ya Bungu ambapo licha ya mfuko wa jimbo kutolewa na baadhi ya vifaa kununuliwa kazi hazifanyiki.
Hayo yalibainika kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo na mbunge huyo walipotembelea
eneo hilo ambapo wananchi walimlalamikia DC kuhusu kutotekelezwa kwa ujenzi wa madaraja ambapo kiongozi
huyo wa serikali alilazimika kuwasiliana na mkurugenz kulikoni

No comments:

Post a Comment