18 July 2013

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI - DKT. NAGU


Na Rehema Mohamed
SERIKALIimeahidi kuendelea kufanyakazikwakari bunasekta binaf si ilikuz idi kuijenge auwez oil iziwezekusaidiau kuajiw au chumi, kucho cheamae ndele ona kutoahudu maborak wawananch i.
Kaulihiyo ilitolewa Dar esSalaamj ana naWaziriwa Nc hi Ofisi yaWa ziri Mk uuUwek ezajin aUwez eshaji, Dkt.Mary N agu,baadayakufung akonga manolili lo husishase kta zaumma nabinafs ikwalengo la kuc hocheam aend eleo.
A lisemahiyonimojayahatua z ilizoc huk uliwa naSerikal ikw aku tambuaum uhimuw ase k tabinafsi kwa taifa. Dkt. Nagu alisema sekta hiyo imetoa msukumo mkubwa kwa maendeleo ya nchi.

Kwa mujibu wa Dkt. Nagu Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kujenga sekta binafsi yenye nguvu itakayoweza kuleta matokeo mazuri kwa uchumi.
Alisema hatua hiyo itasaidia kufikiwa kwa vipaumbele vilivyowekwa na Serikali katika nyanja za kilimo, maji, miundombinu, elimu na afya.
"Sekta binafsi haina budi kushirikishwa kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wake kufikia malengo yanayokusudiwa," alisema.
Alifafanua kuwa Serikali i t a e n d e l e a k u b o r e s h a mazingira ya wawekezaji na biashara nchini ambapo t a y a r i ma t u n d a y a k e yameanza kuonekana ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri, nishati ya umeme, elimu, afya, teknolojia na mawasiliano na huduma nyingine.
Dk t . Na g u a l i s ema ushirikiano wa pande hizo mbili unasaidia kuleta ushindani wa uzalishaji bidhaa kwa soko la ndani na la nje.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye, alisema kwa kuzingatia matokeo makubwa, taasisi hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuweza kuinua uchumi wa Taifa na watu hasa katika maeneo ya kipaumbele

No comments:

Post a Comment