Na
Timothy Itembe, Tarime
SHIRIKA la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Wanyama Serengeti imetoa msaada wa
mabati 6,000 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kama sehemu yao
ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Wilaya na vijiji vinavyozunguka
Hifadhi za Taifa.
Akikabidhi mabati hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa,
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Allan Kijazi amesema kuwa Tanapalimetoa
mabati 6,000 yenye thamani ya sh.milioni 124 kwa ajili ya kusaidia katika
maendeleo ya wananchi.
Kijazi amesema kuwa mabati hayo yatasaidia kuezeka madarasa ya shule,
nyumba za walimu na vituo vya polisi na zahanati ndani ya Wilaya ya Tarime na
kwamba msaada huo unatokana na ushirikiano na mahusiano mazuri kati ya Tanapana
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Akielezea changamoto Kijazi alisema kuwa kumekuwepo na migogoro baina ya
wananchi na Hifadhi ya Serengeti kwa kujenga nyumba katika maeneo ya hifadhi na
kuchunga mifugo hifadhini, kuchoma mkaa, huku baadhi ya wananchi wakiwaua
wanyama kwa ajili ya vitoweo jambo ambalo amedai kuwa linavunja mahusiano
mazuri baina yao na wananchi katika maeneo yaliyo jirani na hifadhi.
Kijazi aliongeza kuwa changamoto nyingine kumekuwepo na baadhi ya
viongozi wa kisiasa kutetea uovu na kushawishi wananchi kuendelea kuchunga
mifugo katika maeneo ya hifadhi na hivyo kusababisha mkanganyiko kati ya
wananchi na hifadhi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa amewataka viongozi wa
kata na vijiji kutohusisha siasa katika maendeleo ya wananchi na badala yake
watatue matatizo ya wananchi ili kuwepo na mahusiano mazuri kati yao na Shirika
la Tanapa.
Tuppa amewataka wananchi kutojihusisha na vitendo vya kuua wanyama
kwakuwa wanyama ni vivutio vya watalii na kupitia wanyama hao taifa linapata
fedha ambazo zinatumika katika maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Tarime, John Henjewele amelishukuru Shirika la Tanapakwa msaada wa mabati
akawataka wananchi kulinda mapitio ya wanyama kwa madai kuwa wanyama wanatoka
nchi jirani ya Kenya kuingia Hifadhi ya Serengeti
No comments:
Post a Comment