Shufaa Lyimo na
Nasra Kitana
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wametua mjini Mu s oma Mk o a wa Mara
jana katika ziara yao ya kimichezo ambapo kesho watacheza na Kombaini ya huko.
Katika mechi
yake ya kirafiki iliyochezwa juzi mjini Kahama Simba waliifunga timu ya Kahama
United bao 1-0, bao hilo lilifungwa na Zahor Pazi mchezaji mpya wa Simba.
Akizungumza kwa simu jana wakiwa njiani
kuelekea Musoma Kocha Mkuu wa timu hiyo Abdalla Kibadeni alisema, mara baada ya
kufika mjini humo watacheza mechi na Kombaini ya huko au timu yoyote
watakayoandaliwa.
"Sasa hivi tupo njiani tunaelekea
Musoma tumetoka alfajiri lakini mpaka sasa bado sijajua tutakutana na timu gani
ingawa tumepanga kucheza na kombaini ya huko ila tukifika tutajua,"alisema
Kibadeni.
Alisema kikosi chake kwa sasa
kinaendelea vizuri na kila mchezaji ana morali wa hali ya juu kuhakikisha msimu
ujao wanafanya vizuri.
"Kikosi changu kinaendelea vizuri
kabisa na vijana wote wapo katika hali nzuri wakiwa na imani ya kufanya vizuri
msimu ujao wa ligi kuu ambao utaanza mwezi ujao," alisema,
Simba iliondoka wiki iliyopita ambapo
mchezo wake wa kwanza ilikutana na timu ya Rhino Rangers na kuwafunga mabao
3-1, wakati mchezo wa pili ilicheza na Kahama Utined na kuifunga bao 1-0.
Wakati huo huo Kaimu Mwenyekiti wa Simba
Joseph Itang'are amesema kuwa timu yao ipo fiti kuivaa URA ya Uganda
watakayochezanayo Julai 20, mwaka huu.
"Kiukweli timu yetu sasa
inaleta raha kwakuwa kila mechi vijana wanafanya vyema na tunaahidi hata
tukicheza na URA pia lazima tuwapige bao," alisema Itang'are.
No comments:
Post a Comment