SERIKALI imeshauriwa kutenga bajeti maalumu kwa ajili
ya kusaidia kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kuepukana na adha ya
kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo, anaripoti Lilian Justice, Morogoro.
Ushauri huo ulitolewa jana mkoani Morogoro
na Diwani wa Kata ya Bigwa, Zamoyoni Abdalah wakati akizungumza na majira
ofisini kwake.
Abdalah alisema kuwa kutokana na wananchi
kukumbana na kero kubwa ya ukosefu wa maji katika maeneo mengi kumepelekea
kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
“Serikali vyema ikatenga bajeti maalumu ya
kutosheleza kuendeleza miradi ya maji kuanzia ngazi ya chini kwani ndiko kuliko
na changamoto kubwa,” alisema .
Aidha Diwani huyo alisema kuwa katika
kukabiliana na changamoto hiyo tayari kwenye kata yake kumeanzishwa mradi wa
I-WASH ambao umesaidia kujenga tenki kubwa la maji ili kuweza kuwasaidia
wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi ukilinganisha na hapo awali.
"Mradi huu wa I-WASH wa kutoka nje
umeweza kujenga tenki lililogharimu kiasi cha shilingi mil.78 na unahudumia
katika Kata ya Bigwa ambapo umeweza kuwahudumia wananchi wapatao 2,800.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kuepuka
kuharibu miundombinu ya miradi mbalimbali inayoanzishwa ndani ya kata hiyo
ikiwemo ya maji kwani kutapelekea kukosa huduma muhimu sambamba na wahisani
kushindwa kuwasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi afya na hata
barabara.
“Tunaomba kila mwananchi awe
mstari wa mbele kulinda miundombinu na atakayebainika k u j i h u s i s h a n a
u h a r i b i f u atachukuliwa hatua kali za kisheria kwani miundombinu iliyopo
au inayoanzishwa ni mali ya wananchi hivyo haina budi kutunzwa ili iweze kuwa
endelevu kwa kizazi hadi kizazi,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment