18 July 2013

NBC KUWAKOMBOA KIUCHUMI WAAJIRIWA


Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imezindua Kampeni ya Uelewa ya Mikopo kwa Makundi, huduma itakayowalenga waajiriwa wenye mishahara.
NBC ni moja kati ya benki zenye kuaminika nchini ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 45 katika kutoa huduma za kifedha.
Aidha, mpango huo wa mikopo kutoka NBC unalenga kuwanufaisha waajiriwa wanaopata mishahara huku wakibanwa kwa kutokuwa na kipato cha ziada kinachoweza kuelekezwa ama kwenye uwekezaji au shughuli nyingine yoyote.
Sharti pekee linalomfanya mwajiriwa kukubalika kwenye mpango huo ili kupata mkopo ni uthibitisho kutoka kwa mwajiri wake
.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya uelewa iliyofanyika Makao Makuu ya NBC jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Mizinga Melu alisema hayo ni mafanikio.
"Hii ni hatua muhimu sana kwa benki yetu, kwa kufanikiwa kutimiza moja ya malengo yetu ya kuwasaidia watu kufikia matamanio yao, kwa njia sahihi. Tunaishi kwenye mazingira magumu ya kiuchumi ambapo kipato cha wengi kinashindwa kukidhi mahitaji yao.
“Kwa hiyo, kwa kupitia mpango huu tutasaidia kuwapunguzia wateja wetu mzigo mkubwa walionao kwa kuwapa fursa ya kufanya mengi zaidi kutokana na fedha zao," alisema.
Alisema, mikopo ya NBC kwa makundi ipo katika aina mbili ikiwemo ya Mfumo wa Mikopo ya Uthibitisho (NBC Group Loan Guarantee Scheme) ambayo mwajiri anakuwa mthibitishaji mkuu kwa mikopo ya waajiriwa (wafanyakazi) wake.
Pia alisema kuna Mikopo ya NBC kwa Makundi (NBC Group Loans Scheme) ambapo mwajiri anasaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) n a k u t a k iwa kuleta benki mishahara ya mwajiriwa pamoja na madai mengine.
"Ukifananisha na mipango mingine ya mikopo, huu wa NBC umetengenezwa kwa kuendana na mfumo wa maisha wa wateja wetu. Ulipaji wake ni rahisi kwani unaendana vyema na wakati, muda na kiwango cha malipo ambacho ni kidogo na kila mmoja anakimudu,” alisema Melu.
Hata hivyo, kiwango cha chini kabisa cha mikopo hiyo ni sh. 1,000,000 na cha juu ni sh. milioni 50 katika kipindi cha malipo cha kati ya miezi sita hadi 60 (miaka mitano).
"Ninawashauri waajiri n a w a a j i r i w a w o t e kuitumia ipasavyo nafasi hii kutoka NBC. Mpango huu utawanufaisha sana waajiriwa kwani hawana haja ya kuwa na dhamana binafsi ili wanufaike nao. Dhamana pekee ni ajira yao.
" L i k i t o k e a j a m b o lisilotarajiwa kama kifo au ulemavu wa kudumu, h a k u t a k uwa n a d e n i litakalobaki kwa wategemezi wa mkopaji kwani bima ya mkopo italitatua hilo,” alisisitiza Mkurugenzi huyo.

1 comment:

  1. punguzeni riba kwanza ndio mtuzindulie hiyo kampeni!

    ReplyDelete