Na Mwandishi Wetu
WANAWAKE 400 k a
t i k a Wi l a y a y a T e m e k e wamenufaika na mikopo isiyokuwa na riba, hii
ni katika utekelezaji wake wa azma ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
kubadili maisha ya wanawake kwa kuwawezesha kukuza mitaji ya biashara na
kuongeza kipato.
Meneja wa
mpango huo kusaidia wanawake wanaojishughulisha na biashara ndogondogo (MWEI),
Grace Lyon alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa mchakato wa
kuwapatia mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana. Alisema kuwa, kampuni hiyo
imepanua wigo wa mpango wake ambapo sasa inawafikia wanawake hata wa mijini.
Alisema kuwa
wanawake wajasiriamali zaidi ya 400 wamepatiwa mkopo huo ili kujiendeleza
kiuchumi na kuwa na familia zenye maendeleo.
Alisema kuwa
pamoja na kuwepo kwa maombi ya kuwafikia wanawake wa mijini kampuni ya Vodacom
imekubaliana na mawazo hayo na kwamba wanawake wa mijini watajiweka tayari
kutumia fursa ya mikopo ya Mweikujiinua kiuchumi.
“Kwa zaidi ya
miaka minne sasa Mwei imekuwa ikielekeza nguvu zake vijijini ambako tayari
tumewafikia wanawake wengi katika mikoa mbalimbali, sasa tumeona ni vyema
mafanikio yale yawafikie na wanawake wa mijini ambao nao kimsingi wanahitaji
kujengewa uwezo wa kumudu maisha,” alisema Lyon
Kuhusu utekelezaji wa azma hiyo, Lyon
alisema wameanza na Temeke lakini mipango ni kuzifikia wilaya nyingine za jiji
la Dar es Salaam huku akiwasihi wanawake hao kutambua kuwa hakuna kikubwa kilichoanza
na kingi bali siku zote kikubwa huanza na kidogo.
Kwa upande wao baadhi ya
wafanyabiashara hao wa Temeke wameelezea kufurahishwa na mpango huo hasa katika
kipengele cha kutokuwepo kwa riba katika mikopo hiyo.
No comments:
Post a Comment