Na Abdallah Amiri, Igunga
JESHI la Polisi
Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limemfikisha mahakamani Masanja Ndongo 15, Mkazi
wa Igunga mjini kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Mshtakiwa huyo
alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga jana saa 11:30 asubuhi huku
wananchi wakiwa wamefurika mahakamani hapo kushuhudia kesi hiyo.
Akisomewa shtaka mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, Mwendesha mashtaka wa
Polisi, Dezidery Kaigwa alisema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai tisa
mwaka huu saa 12:00 jioni katika Mtaa wa Kilabu cha chini wilayani humo.
Aidha mwendesha mashtaka huyo alisema kuwa
mshtakiwa huyo ni mwanafunzi anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi
Chipukizi iliyoko mjini Igunga.
Alisema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo
kinyume na kifungu namba 130(1)na 2(e)pamoja na kifungu namba 131 sura ya 16 ya
kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mshtakiwa
baada ya kusomewa shtaka alikana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada
ya kukosa mdhamini na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 26, mwaka huu
itakapotajwa tena
No comments:
Post a Comment