24 July 2013

MOURINHO AMKOMALIA ROONEY. LONDON, Uingereza
KOCHA Jose Mourinho amesema Wayne Rooney ndiye shabaha pekee ya uhamisho majira ya joto kwa Chelsea baada ya Manchester United kuikataa ofa yao kumsaini mshambuliaji huyo wa England.
Mourinho alikanusha taarifa kwamba David Luiz au Juan Mata walikuwa wabadilishane na Rooney.
Kocha huyo Mreno anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kesho wakati Chelsea watakapotua Malaysia katika ziara yao kabla ya msimu wa ligi kuanza.
Taarifa za Chelsea kumtaka mshambuliaji huyo zilivuja siku ambayo makamu mwenyekiti wa United, Ed Woodward, aliporudi mapema kutoka ziara ya klabu kabla ya msimu wa ligi kuanza.
Hata hivyo, Man United imesisitiza kwamba kurudi kwa Woodward hakuhusiani na suala la Rooney.

No comments:

Post a Comment