12 July 2013

MAZITO

  • Vinara wa rushwa nchini wadaiwa kulindwa
  • Vigogo wannewatajwa kuhusika na mtandao
Na Penina Mhando
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, B w. Reginald Mengi, am esema ipo hatari ya Tanzania kuongozwa na viongozi watoa rushwa amba o baadhi yao wapo mahakamani lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao.
Bw. Mengi aliyasema hayo DaresSalaam ja na katika mkut ano wa majadiliano ul ioshirikisha wadau wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TP SF) na Ser ikali.

Alisema kuna watu wanne ambao  ni waku bwa(hakuwata jamajina), ambao wan ashindwa kudhibiti vitendo vya rushwa kwa sababu wao ni w ahusika wakubwa katika mtandao huo 
“Hapa Tanzania kuna kitu kinaitwa utash i wa siasa wahusika wanamaanisha kupi ga vita rushwa... jambo hili linafanyika kwa maneno si vitendo kwani asilimia kubwa ya watu wa ngazi za juu ndio wahusika wakubwa wajanga hili.
“Kwa mawazo yangu na maeneo niliyopita, kuna wakubwa wanne hapa nch ini ambao ndio vinara wa mtandao wa rushwa lakini hakuna mtu yeyote anayewataja kutokana na nafasi zao,”alisema Bw.Mengi.
Aliong eza kuwa,asilmia kubwa ya watoaji rushwa ni watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya nchini na kuwapa vijana ili waziuze hivyo kuhari bu maisha yao na wengine hujikuta wakikamatwa katika nchi mbalimbali.
“Tatizo la rushwa pia lipo kwa viongozi wajuu ambao ndio wahusika wakubwa wa mtandao huu... ni vyema vita ya rushwa na dawa za kulevya ikafanywa kwa vit endo ili kuharakisha maendeleo ya nchi, ”alisema

4 comments:

  1. HIVI YALE MADAI YA KILICHOKUWA KIKUNDI CHA THE COMEDY BAADA YA KUHAMIA TBC KUWA HAKUNA MNAFIKI KAMA REGNALD MENGI AMBAYE ANA TABIA YA KUTOA CHAKULA CHA BURE KWA WASIONACHO ILI KUFICHA MADHAMBI KWA KUDHULUMU WAFANYAKAZI WA TAASISI ZAKE WAKILIPWA MISHAHARA MIDOGO WENGI VIBARUA HAWANA AJIRA ZA KUDUMU ILI MUNGU HAMFICHI MNAFIKI IKO SIKU ATAMVUA NGUO HADHARANI KWANI KILA BINADAMU ANAMWABUDI MUNGU IKUMBUKWE IWAPO MUNGU ANAPOKEA RUSHWA ASINGERUHUSU TAJIRI AENDE MOTONI NA MASKINI AENDE PEPONI ASOME BIBILA ASITAFUTE HURUMA ZA WANYONGE BEPARI YEYOTE NI NYANG'AU TU UBEPARI NI UNYAMA HADANGANYWI MTU

    ReplyDelete
  2. Hizo ni hadithi,hakuna mfanyabiashara asiyependa kupata faida. Lakini ukweli ni kwamba rushwa imekithiri na wahusika hawana habari kama asemavyo mengi.
    Labda kama unaona hawatendei haki kwa hayo uliyosema na wewe anzisha kampuni yako then uwalipe wafanyakazi wako mamilioni uone kama kampuni itaendelea kuwepo, acha majungu

    ReplyDelete
  3. Mbona mnamtetea. Wacha ukweli wa mambo uje na ajitetee mwenyewe. wengi watoao misaada wanaficha mambo.

    ReplyDelete
  4. Hivi kweli ninyi watu wawili mliotoa mawazo hapo juu akili zenu ziko sawa mmenifanya niwe na wasiwasi na ninyi. Kwa sababu mnaongelea mtu (you are discussing people) badala ya tukio (yaani event).
    Watu kama ninyi rais wa zamani wa Marekani (Lincoln) alisema mna mtazamo finyu (yaani short minded).
    Nawaomba muwe mnatafakari kwanza kabla ya kutoa maoni.

    ReplyDelete