24 July 2013

MARTINO AMRITHI VILANOVA KLABU BARCELONABARCELONA, Hispania
BA R C E L O N A wamemchagua Gerardo Martino kutoka Argentina kama kocha wao mpya baada ya kukubali mkataba wa miaka miwili kuifundisha klabu hiyo.Martino (50), kocha wa zamani wa Paraguay, anachukua nafasi ya Tito Vilanova, ambaye alijiuzulu kama kocha wa Barcelona ili aendelee na matibabu yake ya saratani.
Martino hivi karibuni alikuwa akiifundisha klabu ya Old Boys ya Newell, ambao aliwaongoza kunyakua kombe la Argentina la Torneo msimu uliopita. Taarifa za kuwasili kwake Barcelona zilitarajiwa kutangazwa jana na mabingwa hao wa Hispania.
Martino anakuwa raia wa nne wa Argentina kuifundisha Barca baada ya Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti. 
Hiyo itakuwa kazi ya kwanza kwa Martino nje ya Amerika ya Kusini tangu alipoichezea Tenerife kwa miezi sita mwaka 1991. Awali, makocha wengi walikuwa wakihusishwa kutaka kujaza nafasi hiyo, akiwemo kocha Luis Enrique wa Barcelona B, Andre Villas-Boas wa Tottenham, Michael Laudrup wa Swansea na Guus Hiddink, ambaye juzi alijiuzuru kuifundisha Anzhi Makhachkala

No comments:

Post a Comment