19 July 2013

MANDELA 95

  • Dunia yasherehekea siku ya Mandela
PRETORIA, Afrika Kusini

RAIS wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia kuiongoza Afrika Kusini, Nelson Mandela, amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 95 akiwa amelazwa hospitalini mjini Pretoria, huku matukio ya sherehe hiyo yakifanyika karibu duniani kote. Wananchi wa Afrika Kusini pia walihimizwa kuadhimisha utumishi wa umma wa miaka 67 wa rais huyo wa zamani na kiongozi wa kupinga ubaguzi wa rangi kwa kutumia dakika 67 kufanya shughuli za hisani wakati wa sherehe hiyo.

Mz e e Ma n d e l a , amb a y e yuko mahututi huku hali yake ikiimarika kutokana na ugonjwa wa maambukizo kwenye mapafu, alilazwa hospitali Juni 8, mwaka huu.

Kwa mujibu wa BBC, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alisema afya ya Mzee Mandela inazidi kuimarika.

"Tukiwa kama wananchi wa Afrika Kusini, tunajivunia kuwa na mtu huyu mashuhuri kimataifa na tunamtakia afya njema," alisema Rais Zuma katika taarifa yake na kuongeza;

"Tunawashukuru watu wetu wote kwa kumuunga mkono Madiba katika kipindi chote alicholazwa hospitali kwa upendo na huruma."

Kwa upande wake, binti wa Mandela, Zindzi, alisema juzi kwamba afya ya baba yake ina maendeleo makubwa na kwamba alimkuta akiangalia luninga, huku akiwa na spika za masikioni na akiwasiliana kwa macho yake na mikono wakati alipomtembelea wiki hii.

"Nadhani ataruhusiwa kutoka hospitali wakati wowote," Zindzi alikiambia kituo cha televisheni cha Uingereza, Sky News.

Siku ya kuzaliwa Mzee Nelson Mandela pia ni siku yake ya Kimataifa, siku iliyotangazwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2009 kama njia ya kutambua mchango wa maridhiano wa mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel.

Kiongozi huyo wa zamani anahusudiwa duniani kote kwa jukumu lake la kukomesha ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Mandela aliendelea kuwa rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu 1994 wa raia wenye rangi tofauti.

Chama tawala cha African Nation alCo ngres s(A NC)kilis ema katikasi kuhiyoy aMand elaDayhes himailit olewakwa m iaka 95ya"mais hayaliyo dumuvizuri", kwakujito lea katika ukomboz i wa wana nchiwaA frikaK usini nawatuwote duniani.

Wakatihu ohuo,nc hiya Ufaransa ja naili ungana nadu niakusherehekea"S ikuyaN elsonMandela, amba yeanat imiz amiaka 95yaku zaliwal eo(jana)," alisema La ure ntFabius ,Wa ziri waMamboya Nchi za Nje wa Ufaransa.

Kwa mujibu wa Xinhua katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake, Fabius alitoa heshima kwa Mandela kwa kutoa mchango mkubwa "kuleta uhuru na heshima kwa watu wa Afrika Kusini. "

"Ufaransa inatoa heshima za ukarimu na urafiki kwa Nelson Mandela," mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Ufaransa alisema.

Watoto walisherehekea siku hiyo ya kuzali waMandelak wa kufanya sherehemb alimbali nakuimbanyimbo .

Kwaupande wake, Rais Vladimir Putinwa Uru sijanaa limpo ngezaMand elak wamc hang owakekatika historia ya Afrika na kusema ni sehemu muhimu katika historia ya Afrika ya sasa.

"Jina lako halitenganishwi, bali linahusishwa muda wote wa historia ya sasa ya Afrika iliyojenga upya demokrasia katika Jamhuri ya Afrika Kusini," Putin alisema katika ujumbe wake akimpongeza Mzee













 

No comments:

Post a Comment