12 July 2013

MAJAJI WAPYA WAFANYA USAILI EBSS MBEYA


 Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MASHINDANO ya kumsaka nyota wa kuimba wa Epiq Bongo Star Search (EBSS), yamezoeleka kuwa na majaji watatu ambao ni Ritha Paulsen, Salama Jabir na Master Jay, lakini kwa mara ya kwanza, vijana waliojitokeza kwenye usaili mkoani Mbeya walipata fursa ya kusailiwa na majaji wapya wa kutokea mkoani hapa.
Majaji hao, Stanslaus Lambert na Fredy Mabula ambao waliongezwa ili kuleta ladha tofauti kwenye mashindano hayo, wamepongeza EBSS kwa kusaidia vipaji vilivyoko mikoani.
"Epiq Bongo Star Search ina mchango mkubwa mno kwenye tasnia ya muziki hapa nchini, hivyo ni heshima ya pekee kuwa jaji kwenye mashindano haya," alisema Mabula.

Wakizungumzia uwezo wa majaji wapya, Master Jay alisema wameonesha uwezo katika kuwashauri washiriki na kuchagua vipaji vinavyofaa.
Awali Jaji Mkuu wa EBSS, Ritha alisema kuingia kwa majaji hao wapya ni mwendelezo wa utaratibu walioanzisha sasa wa kushirikisha majaji kutoka mazingira, ambayo mchujo unafanyika.
"Lengo letu ni kuifanya EBSS imguse kila mtu, lakini pia ichague kila aina ya vipaji vilivyopo mikoani na iviendeleze," alisema Ritha.
Akizungumzia hali ilivyokuwa kwenye usaili wa mkoa huo, Ritha alisema washiriki wameonesha uwezo mkubwa katika kuimba na kujiamini.
Jaji huyo alisema Mkoa wa Mbeya ni mkoa ambao umewaridhisha majaji kati ya mikoa mitatu ya Dodoma na Zanzibar, ambako wameshafanya usaili hadi sasa.
Mbeya imetoa washiriki sita ambao wamepata tiketi ya kushiriki katika fainali zitakazofanyika Dar es Salaam, kwa sasa EBSS inakwenda mkoani Mwanza wiki h
.

No comments:

Post a Comment