24 July 2013

MADAKTARI BINGWA KUPELEKWA MIKOANI Na Fatuma Mshamu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za madaktari bingwa mikoani ili kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama pamoja na wadau wake. Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Afya na Utafiti wa mfuko huo, Raphael Mwamoto alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mpango huo.

Alisema, madaktari hao wanatoka Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa MOI ambao pia ni madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, watoto, upasuaji yakiwemo yale ya kawaida. Alisema, lengo la mpango huo ni kupeleka huduma katika mikoa yenye uhaba mkubwa wa madaktari bingwa pamoja na kupunguza gharama za usafiri kwa wagonjwa wanaofuata huduma hizo mijini na kuwapa watendaji waliopo fursa ya kujifunza katika mikoa hiyo wanayoitembelea.
"Ka t i k a k u t e k e l e z a mpango huu hadi sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshatumia sh. milioni 115.9 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na gharama za madaktari," alisema Mwamoto. Alisema, katika awamu ya kwanza ya mpango huo tayari mikoa minne ya Lindi, Kigoma, Katavi na Rukwa imeshapata huduma hizo na mikoa iliyosalia ni Mara, Tabora na Pwani huku akisisitiza maandalizi ya awali yanafanyika katika Mkoa wa Pwani.
Mwamoto aliongeza kuwa, hadi sasa wananchi 3,698 wamepata huduma na kati yao wagonjwa 98 walipata huduma ya upasuaji. Mb a l i n a h a y o p i a wanakabiliwa na changamoto ya idadi ndogo ya madaktari bingwa, uhaba wa vifaa tiba vya kisasa na uhaba wa vitendea kazi na dawa.
Pia aliongeza kuwa, wananchi wanaofanya kazi katika sekta binafsi wanaruhusiwa kujiunga na mfuko huo wa kufuata sheria zilizowekwa ila wao watatakiwa kulipia huduma hizo kwa mwaka

No comments:

Post a Comment