19 July 2013

MABONDIA 10 WAJIANDAA NA UBINGWA AFRIKANa Mosi Mrisho
MABONDIA 1 0 wa t imu y a Ta i f a y a ngumi, wanajiandaa na mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika, ambayo yanatarajia kufanyika kuanzia Septemba Mosi hadi 7 mwaka huu nchini Mauritius.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema mabondia hao wameshaanza mazoezi katika Uwanja wa Taifa wa ndani, Dar es Salaam.
"Mabondia watakaoshiriki mashindano hayo hivi sasa wapo katika mazoezi chini ya makocha watano na tunaamini kwa mazoezi hayo watafanya vizuri," alisema.Hata hivyo Mashaga alisema mabondia hao ni wachache kulingana na mashindano hayo. Aliwataja makocha hao kuwa ni Remmy Gambo, Edward Emmanuel, Mzonge Hassan, Benjamin Mwagata na Mussa Mwaisori.

No comments:

Post a Comment