17 July 2013

LWAKATARE CHINI YA UANGALIZI MAALUM


Ester Maongezi na Neema Malley
MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, amewekwa chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kwa muda wa siku nne ili kuimarisha afya yake.
Akizungumza na Majira alipolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dar es Salaam, juzi, Lwakatare, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya madaktari kukutana na kutoa tamko kuhusu matibabu yake
.
"Nipo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kwa muda wa siku nne, ambapo ndani ya siku hizo nne nitakuwa nafanya mazoezi kwa saa tatu kila siku kwa muda tofauti," alisema Lwakatare
Lwakatare alisema baada ya kumalizika kwa hizo siku nne alizopewa; madaktari watamfanyia kipimo cha X-ray ili kujua kama pingili zitaachana.
Akizungumzia hali yake kwa sasa, Lwakatare alisema anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa awali. Alisema maumivu aliyokuwa akisikia kwenye shingo ni madogo na anaendelea vizuri
Kwa upande wa Ofisa habari wa MOI, Patrick Mvungi, alisema bado wanaendelea na kumpatia huduma anayostahili Lwakatare.
Lwakatare alilazwa MOI J uma t a n o wi k i i l i y o p i t a akisumbuliwa na maumivu makali kwenye shingo ambayo yalitokana na kusagika kwa pingili za shingo

No comments:

Post a Comment