Na Daud Magesa, Mwanza
KochaMkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema
kikosi chake kimejiandaa kuikabili Uganda
kwenye mechi ya marudiano ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), itakayochezwa Jumamosi jijini Kampala. Akizungumza na waandishi wa habari
jijini hapa jana, Kim alisema tangu kikosi chake kimeingia kambini Julai 14
mwaka huu, wachezaji wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mazoezi na wako tayari
kwa ajili ya mechi hiyo
. "Uganda ni timu bora kwa ukanda huu
wa Afrika Mashariki na Kati. Mechi itakuwa ngumu, tunaamini tunakwenda kufanya
vizuri. Tayari tunayo mikakati kwa ajili ya mechi hiyo, tunakwenda kuikamilisha
Kampala,"
alisema Kim.Hata hivyo, Kim alisema licha ya
mwitikio mzuri wa wachezaji kwenye mazoezi, lakini wanakabiliwa na changamoto
ya wengi wa wachezaji kuwa wamefunga, wakati wachezaji wanapokuwa kambini
wanatakiwa kula, kunywa na kupumzika.
"Hiki ni kipindi kigumu kwa mpira
wa miguu na suala la kufunga ni la kiimani ambapo hatuwezi kuwazuia wachezaji
kufunga. Karibu nusu ya wachezaji wanafunga, hii ni changamoto ambayo
tunaiheshimu," alisema Kim. Aliongeza: “Ni wazi kikosi chake cha
kwanza kitakuwa na mabadiliko baada ya beki Shomari Kapombe kwenda kwenye
majaribio nchini Uholanzi.”
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager inaondoka Mwanza leo saa 7.25 mchana kwa ndege ya
PrecisionAir na kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8.15 mchana.
Wachezaji waliomo kwenye msafara huo ni
makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na Ali Mustafa ‘Barthez’. Mabeki ni Aggrey
Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Canavaro’ na
Vincent Barnabas.Viungo ni Amri Kiemba, Athuman
Idd ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis Mcha, Mudhathir Yahya, Salum
Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John Boko, Juma Luizio na Mrisho
Ngasa
No comments:
Post a Comment