Na Mwandishi Wetu
WATANZANIAwameshau riw ak utumiaki
faachakuchajiainaya Read ySetilikupungu zagharamayanish atipa mojanakujiingizi
akipato .Kifaah ichocha
kuchaji kilizinduliwan akampun iya mawasiliano y aV odacom,k wakushir ikianana
Fen ixInte rna tional Aprilimwak ah uuik iwanalengolakuwa pa tiaWatanzania
nishati pa mojanaaji ra .Akizungu mzah
ukuaki onyesha kifaa hichojijn iDar esSalaamwi kihii, Me nejawaKampuniyaVo
dacom,Nich olus Kizenga, alielezea kuwa Watanzania wamekuwa wakisubiria jambo
hili kwa muda mrefu.
“Chaja hizi
zimezinduliwa wakati mwafaka kabisa hapa nchini kwa sababu zitaleta msaada
mkubwa sana kwa Watanzania walio wengi kwa kuwa zitawasaidia kutunza mali kama
pesa na muda,” alisema Kizenga.Kizenga alisema
kuwa chaja za ReadySet zimeleta suluhisho la kupunguza gharama ya nishati
kwakuwa zinaweza kuchaji simu kumi kwa wakati mmoja, taa za ndani, redio na
kompyuta. Alisema kuwa
kifaa hicho kinagharimu sh.320,000 na kinaweza kikamuingizia mtu anayefanya
biashara ya kuchajisha simu sh.64,000 kwa mwezi.
Alisema kuwa kwa kutumia kifaa hicho
pia watumiaji wataweza kujiwekea takribani dola kumi za kimarekani kwa
kutokutumia mafuta ya taa.“Watanzania wasiogope kutumia kifaa
hicho kwasababu kinaendana na mazingira ya Kitanzania na kinapopata shida kuna
mafundi wa kuvitengeneza kwasababu kina uthibitisho,”alisema.
Maneno Mashaka, mmoja wa watu
waliokuwepo wakati wa maonyesho hayo, alisema ana matumaini kwamba kwa
maendeleo haya, Tanzania inakuwa kiuchumi bila kuwa na gharama kubwa kama za
kufungiwa umeme na kuingiza mafuta yatokanayo na petroli nchini.
“Huu ni uzinduzi mkubwa sana, na wengi
wetu ambao tulikuwa hatuna umeme majumbani mwetu tumelazimika kutumia mkaa na
mafuta ya taa. Haya yametuletea athari kubwa sana za kiafya. Kwa kutumia chaja
hizi tunaweza kuingiza kipato na wakati huo huo kupata nishati ya
umeme,”alisema Mashaka
Katika uzinduzi huo, ilifahamika kuwa takribani watumiaji milioni 600 wa
mitandao ya simu hutumia trilion 16 za Kitanzania kwa mwaka kusafiri kwenda
kuchaji simu zao na nishati ya umeme wa betri za magari.
No comments:
Post a Comment