23 July 2013

KESI YA RAIA WA UINGEREZA,WENZAKE YAAIHIRISHWA TENA Na Rehema Mohamed
UPANDE wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mwanafunzi, Ahsan Ali Iqbal au Ali Patel (19), raia wa Uingereza na wenzake sita, akiwemo msanii Chingwele Che Mundugwao, umeomba shauri hilo liahirishwe hadi kesho ili kuongeza washtakiwa wengine katika kesi hiyo

Mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya, alidai shauri hilo lilifikishwa kwa ajili ya kutajwa, hivyo aliomba liahirishwe kwa muda fupi hadi kesho ili kuunganisha washtakiwa hao na wengine.
Mbali ya Patel na Che Mundugwao, washtakiwa wengine ni ofisa ugavi wa Idara ya Uhamiaji, Shemweta Kiluwasha, Injinia Kenneth Pius wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, mfanyabiashara Ally Jabir, Rajabu Momba na Haji Mshamu.
Wa s h t a k iwa h a o amb a o wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, wizi wa hati 26 za kusafiria mali ya serikali, kughushi, kuwasilisha hati ya kughushi walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu shauri hilo lilipotajwa.
Komanya alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kwamba wanaomba liahirishwe hadi kesho.
Hakimu Sundi alikubali ombi hilo na hivyo aliahirisha kesi hiyo na washtakiwa hao kurudishwa rumande hadi kesho.

No comments:

Post a Comment