Na Rachel Balama
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana
imeahirisha kesi ya mauaji bila ya kukusudia inayowakabili washtakiwa 11
yaliyohusisha jengo la ghorofa 16 lililoanguka hivi karibuni katika Mtaa wa
Indragandi na kuhusisha vifo vya watu zaidi ya 30 kutokana na kutokamilika kwa
upelelezi.
Kesi hiyo
inamkabili mmiliki wa jengo hilo Bw. Raza Ladha na wenzake 10 ambao
wanakabiliwa na mashtaka 24 ya mauaji bila kukusudia.
Hakimu Devota
Kisoka liiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 15, mwaka huu itakapotajwa tena baada
ya Wakili wa serikali Genes Tesha kuieleza mahakama kwamba upelelezi
haujakamilika.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Bw. Goodluck Mbanga, Bw. Wilbroad Mugyabaso, Bw.
Ibrahimu Mohammed, Bw. Mohamed Abdulkarim ambaye ni injinia na Bw. Charles
Ogore pia ni injinia.
Wengine ni
mhandisi mshauri Bw. Zonazea Mashudada, msanifu majengo Bw.Vedasto Fednand, Bw.
Michael Hema, ofisa mtekelezaji Bw.Joseph Ringo na msajili msaidizi Bw. Halbert
Munuo.
Ilidaiwa kuwa
washtakiwa hao walitenda kosa hilo Machi 29, mwaka huu maeneo ya Mtaa wa
Indragandi wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao
wanadaiwa kuua bila kukusudia ambapo watu wanaodaiwa kuwaua kuwa ni Yusufu
Sharifu, Kulwa Khalfani, Hamad Musa, Kessy Ally, Hamisi Mkomwa, Boniface
Benard, Suhail Karim, Salma Akbar, Selemani Haji, Selemani Mtego na Sikudhani
Mohammen.
Wengine ni Ahmed
Mirambo, Salum Mapunda, Selemani Mnyoni, John Majewa, Mussa Munyamani, David
Helman, Willium Joackim, Abdulrahman Othman, Emanuel Christion, Mmanyi Ngadula,
Advai Desiki, Emanuel Watiani na Augustino chuma.
No comments:
Post a Comment