Na Fatuma Rashid
BEKI wa timu ya Simba, Shomari Kapombe
anatarajia kuondoka nchini leo jioni kwenda nchini Uholanzi kwa ajili ya
kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi, Kapombe alisema anaamini kwa jitihada zake na
kumuomba Mungu atafanikiwa kufuzu majaribio hayo.
Kapombe alisema
amejiandaa vya kutosha na anaamini Watanzania wengi wanamuombea na anajua licha
ya soka kuwa na changamoto nyingi, hususan kwa soka la kulipwa, lakini anaamini
atazishinda.Safari ya
mchezaji huyo, imepewa baraka na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).Akizungumzia
safari ya Kapombe, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema mchezaji huyo
amekubaliwa baada ya klabu yake ya Simba kuwasilisha barua rasmi ya kumuombea
ruhusa
"TFF tumempa ruhusa kwani mara
baada ya kupata barua kutoka Simba, tuliamua kuwasiliana na Kocha wa Taifa
Stars, Kim Poulsen kwa kuwa mchezaji yupo na timu ya taifa Mwanza ambaye naye
alikubaliana na suala hili," alisema.Kutokana na safari hiyo, Kapombe
hatakuwepo katika mechi ya marudiano ya kutafuta nafasi ya kucheza Fainali za
Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN), dhidi ya Uganda.Katika
mechi ya awali iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars ilinyukwa bao 1-0 hivyo
ili isonge mbele katika michuano hiyo itatakiwa kushinda mabao 2-0 au zaidi.
Kila la heri Kapombe,umeanza vizuri na inshallah Mungu akujalie umalize vizuri ili balozi wetu huko.
ReplyDelete