Na Rehema Mohamed
HALI ya askari
wanne wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kati ya 14
waliojeruhiwa katika shambulio la waasi mjini Darfur nchini Sudan ni mbaya na
wapo chini ya uangalizi wa madaktari.
Akizungumza na gazeti hili jana
Msemaji wa JWTZ, Kanali
Kapambala Mgawe,
alisema majeruhi 10 hali zao zinaendelea vizuri na kwamba wanaweza kujihudumia
wenyewe mambo madogo madogo, kwamba wanaweza kutembea na kuzungumza
.
A l i s ema ma j
e r u h i h a o wanaendelea na matibabu eneo la Nyara kwenye Hospitali Kuu
iliyopo eneo la operesheni.
Akizungumzia
hatua iliyofikiwa kurudisha miili ya wanajeshi saba waliouawa katika shambulio
hilo, alisema taratibu hizo zipo chini ya Umoja wa Mataifa (UN) hivyo bado
wanalifuatilia.
“Suala la kuwarudisha askari saba
waliouawa lipo chini ya UN na tunafuatilia,”alisema Kanali Mgawe. Mapema wiki
hii JWTZ ilitoa taarifa kuhusu askari wake hao kuuawa na wengine kujeruhiwa
katika shambulio la kushtukiza ambalo lilifanywa na waasi wa Sudan Julai 13,
mwaka huu.
A s k a r i h a o w a l i k u w a
wakiwasindikiza waangalizi wa amani kutoka Khor Abeche kwenda mjini Darfur.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shambulio
hilo lilitokea umbali wa kilomita 20 kutoka Makao Makuu ya kikosi hicho ambapo
miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na maofisa na askari kutoka mataifa
mengine.
Wakati kikosi cha askari jeshi wa
Tanzania kikishambuliwa, kilikuwa na askari 36 ambao ni miongoni mwa askari
wanaolinda amani kwenye Kikosi cha UN mjini Darfur nchini Sudan.
No comments:
Post a Comment