Na Mwandishi Wetu
MIILI ya askari saba
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla,
itawasili kesho kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere Terminal one jijini Dar
es Salaam. Taarifa iliyotolewa
na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi, Upanga jana ilieleza
kuwa shughuli ya kupokea miili ya wanajeshi hao itaanza saa nne asubuhi.
Taarifa hiyo ilieleza
kuwa mara baada ya kuwasili miili hiyo itapelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Jeshi, Lugalo, baada ya maandalizi ya miili hiyo, tarehe na utaratibu wa kuaga
kwa heshima zote zitafuata.Askari hao waliuawa
wakiwa wanawasindikiza waangalizi wa amani kutoka Khor Abeche kwenda mjini Darfur. Katika shambulio hilo
askari wengine wa Tanzania
14 walijeruhiwa. Shambulio hilo lilitokea umbali wa
kilometa 20 kutoka Makao Makuu ya kikosi hicho ambapo miongoni mwa
waliojeruhiwa ni pamoja na maofisa na askari kutoka mataifa mengine.
Wakati
kikosi cha askari jeshi wa Tanzania
kikishambuliwa, kilikuwa na askari 36 ambao ni miongoni mwa askari wanaolinda
amani kwenye Kikosi cha UN mjini Darfur nchini Sudan.
No comments:
Post a Comment