12 July 2013

JKT INAHITAJI WATENDAJI WAADILIFU WENYE DHAMIRA YA KWELI


 Na Juma Kiyenze
TANZANIA imeadhimisha miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwaka huu, tangu lilipoanzishwa kisheria Julai 10 mwaka 1963 chini ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na washirika wake.
Lengo la kuanzishwa kwake kulilenga kujenga umoja wa kitaifa, kuwapatia mafunzo ya kijeshi na stadi za kazi vijana
 ukakamavu na uzalendo katika nyanja mbalimbali za uchumi, jamii, kilimo, ulinzi na usalama wa taifa.
Malengo mengine ilikuwa ni kujenga mshikamano, udugu, kujitegemea, kuongeza ufanisi wa kazi, nidhamu, kujituma na kuwaandaa kulitumikia taifa kupitia vyombo vza ulinzi na usalama, sanjari na sekta binafsi kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

JKT ilifanikiwa kutimiza malengo yake kitaifa na kimataifa kuwakomboa wananchi kiitikadi, kielimu, kisaikolojia, kiutamaduni, kiutendaji na kwamba hakukuwa na ubaguzi ulioruhusiwa kuota mizizi miongoni mwa jamii.
Kufanikiwa kwake kulitokana na uadilifu wa viongozi waliopewa dhamana kuongoza JKT kwa nyakati mbalimbali, ambao walishirikiana na watendaji wake kutimiza wajibu wao kulingana na dhamana walizokabidhiwa kwa uaminifu, uadilifu, ubunifu, uvumilivu, kujituma, ujasiri na nidhamu.
Wananchi walijenga imani kubwa kwa jeshi lao kulingana na jinsi lilivyokuwa limejipanga katika nyanja mbalimbali kutekeleza majukumu ya Serikali katika suala zima la malezi ya vijana na uzalishaji mali.
Historia ya JKT
Watanzania watakumbuka kwamba, miongoni mwa taasisi zilizoanzishwa na Serikali ya Tanganyika, baada ya uhuru Desemba 9, 1961 ni JKT, ili kuepusha athari zilizoachwa na Wakoloni zisilete madhara miongoni mwa jamii.
Athari hizo ni ubaguzi, udini, ukabila, rangi na tofauti ya kipato, hatua ambayo ilifanikiwa kutokana na taifa kuwaelimisha na kuwaandaa vijana kupitia vikosi na makambi mbalimbali za malezi na mafunzo chini ya jeshi hilo.
Taasisi hiyo ina wajibu kuhakikisha maendeleo ya nchi yanafikiwa katika sekta ya uzalishaji mali kupitia sekta ya kilimo, ili kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa kutoa mafunzo zaidi ya ujasiriamali vikosini.
Kuanzishwa kwake kulitokana na mawazo ya Hayati Mwalimu Nyerere na Mzee Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita), ambao kwa pamoja waliona ipo haja ya kuanzisha taasisi itakayokuwa na jukumu la kuwapatia vijana malezi na kuwaandaa kiutendaji makambini.
Walipoafikiana mawazo yao yalipelekwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU Youth League), Hayati Joseph Nyerere, ambaye naye aliyafikisha katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika mkoani Tabora Agosti 25, mwaka 1962.
Mkutano huo uliafiki mawazo ya viongozi hao na Aprili 19 mwaka 1963, Baraza la Mawaziri la Tanganyika chini ya Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Mwalimu Nyerere, lilipitisha azimio la umoja huo.
Mnamo Julai 10 mwaka 1963 JKT ilianza kutekeleza majukumu yake kwa kuwachukua vijana kutoka mikoa mbalimbali ya nchi kujiunga na jeshi hilo na kundi la awali la vijana 11 kutoka wilaya 11 walipata mafunzo Kambi ya JKT Mgulani Dar es Salaam.
Vi j a n a h a o wa l i k uwa n i Makatibu wa Umoja wa Vijana wa TANU, ambao walipelekwa nchini Yugoslavia mwaka 1962 kwa mafunzo ya uongozi wa vijana, Bi. Z. Kiango, Bw. S. Chale, Bw. P. Lwegarulira, Bw. R. Kamba, Bw. H. Ngalason na Bw. J. Ndimugango (wote sasa hawapo jeshini).
Wengine ni pamoja na Bi. M. Mhando (Senior Guide), Bw. DS. Msilu (Master), Bw. ES. Mwakyambiki (Senior Master), AI. Msonge (Master) na Bw. LM Mitande (hawa wangali katika Jeshi la Kujenga Taifa.)
Mnamo Agosti 1963 kikundi kingine cha watu watano kilijiunga JKT na kupatiwa mafunzo ya uongozi wa vijana jeshini ni Bw. S. Desai, Bw. E. Simkone, Bw. J. Mwanimlele (Asst Master) na Bw. A A Moyo (Asst Master).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa JKT, Mwalimu Nyerere aliwaambia wananchi kuwa, umuhimu wa jeshi hilo unatokana na Taifa kuhitaji huduma ya vijana kulitumikia Taifa lao katika majukumu mbalimbali yatakayotolewa ama kujitokeza kijamii, kiuchumi, kielimu na kiitikadi.
Pamoja na hayo, mwaka 1964, ilitungwa Sheria ya JKT (National Service Act), ambayo ilianzisha mafunzo kwa Mujibu wa Sheria na mwaka 1966 na 1967 sheria ilifanyiwa marekebisho kuwawezesha vijana waliokuwa wanahitimu elimu ya upili kidato cha nne na sita kujiunga katika mafunzo yake.
Kufuatia marekebisho hayo, yalitoa fursa kwa kundi la kwanza la vijana 11 kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria
Operesheni Azimio la Arusha
Kundi la viongozi mbalimbali wa kitaifa lilijiunga mwaka 1968 kwa mafunzo maalum ya uongozi wa JKT, ambao walikuwamo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu Hayati Rashid Mfaume Kawawa na Spika wa Bunge la Jamhuri Hayati Chifu Adamu Sapi Mkwawa, ambalo lilikuwa Operesheni Kazi “A“.
Mwaka 1975, JKT iliunganishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ingawa majukumu ya msingi yalibaki ndani ya jeshi hilo, ikiwa ni Brigedi ya uzalishaji ya Jeshi.
Athari za mtikisiko wa uchumi duniani
Kutokana na kuyumba kwa uchumi duniani wa nchi zilizoendelea kwa viwanda barani Ulaya na Marekani katika miaka ya 1980 – 1995, nchi nyingi changa zilizokuwa zinaendelea, ikiwamo Tanzania ziliathirika kiuchumi.
Serikali ililazimika kusitisha shughuli za JKT mwaka 1994 hadi 2001 kwa vijana kwa mujibu wa sheria na kupunguza shughuli zake.
Kusitishwa kwa mafunzo ya JKT, athari nyingi zilijitokeza miongoni mwa jamii, ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili kwa viongozi, watendaji mbalimbali, nidhamu, kuongezeka kwa vitendo viovu mitaani, wizi, uvutaji bangi, ubwiaji wa dawa za kulevya, ubakaji, ujambazi na ubaguzi uliongozeka na kuleta fedheha kwa nchi.
Kulingana na kuwepo kwa hali hiyo, viongozi wa JKT walikabiliana na mazingira hayo na changamoto mbalimbali zilizojitokeza, sanjari na kufutwa kwa jeshi hilo.
Hali hiyo ilitokana na ushawishi wa mataifa yaliyokuwa yanatoa misaada katika nyanja mbalimbali za jamii kwa viongozi wa kitaifa waliokuwa na dhamana ya madaraka, ambayo walitaka JKT ifutwe ama ishushwe hadhi.
Serikali ilikataa mawazo hayo yaliyolenga kuparaganisha taifa, ili kutoa mwanya wa kujipenyeza kuotesha upya mimea ya ubaguzi, udini, ukabila na vitendo vingine kwa jamii.
Tume maalumu ya wataalam iliyoteuliwa na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Makame Rashid wakati huo ilifanya kazi yake vyema na kuishauri serikali kutofanya ajizi kufuta jeshi hilo, kwani athari zake zingekuwa kubwa na hatari zaidi.
Kufungwa kwa makambi
Mtikisiko wa uchumi duniani uliathiri shughuli mbalimbali, hivyo ulichangia kambi za JKT za kilimo na ufugaji kufungwa, ikiwa ni pamoja na Luwa mkoani Rukwa, Msange- Tabora, Mpwapwa-Dodoma na Makuyuni-Arusha.
Kambi hizo zilitumika kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji kwa nadharia na vitendo vijana waliokuwa wanajiunga na JKT kila mwaka kwa mkataba maalum, hivyo ziliathiri majukumu yake na miundombinu yake iliharibika.
Kuzinduliwa kwa mafunzo
ya JKT
Machi 26 mwaka huu mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria, yalizinduliwa upya, baada ya kusimamishwa kwa zaidi ya miaka 19 na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
Mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya wiki tatu kwa Kundi Maalum la wabunge 22 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na miaka miwili ya kujitolea Operesheni Miaka 50 ya JKT Kambi ya JKT Ruvu mkoani Pwani.
Rais Kikwete ni miongoni mwa viongozi wa kitaifa waliowahi kupitia mafunzo ya jeshi hilo katika kambi hiyo kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Tumaini mwaka 1972, ambaye alikuwa Kombania ‚A‘ akipatiwa namba ya JKT 9983.
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga alimwambia Amiri Jeshi Mkuu kwamba, mafunzo ya miezi mitatu yalianza Machi 4, mwaka huu Kambi za JKT Bulombora- Kigoma, Msange-Tabora, Ruvu- Pwani na Mgamboa-Tanga, ambayo yaliwashirikisha vijana 5,000 kati ya 41,000 waliohitimu elimu ya upili kidato cha sita mwaka huu na yaligharimu Shs 7.5 bilioni.
Akizungumzia wabunge anasema walioomba kujiunga JKT ni 47, jumla ya 24 walikwenda katika kambi walizopangiwa na 22 walihitimu, wawili hawakufaulu kutokana na sababu mbalimbali za kiafya.
Dira ya JKT
Dira ya JKT inataka Tanzania iwe nchi ya watu waliolelewa vyema kitaifa na kujengwa katika misingi ya nidhamu, kujiamini, moyo wa uzalendo, umoja na udugu, kupenda kazi na kutekeleza wajibu, tayari kuitumikia nchi yao katika suala zima la uchumi, elimu, ulinzi na usama.
JKT inaendeshwa kwa kufuata misingi, maadili ya kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa, ambayo ni uadilifu, kujitolea, mshikamano, umoja, uzalendo, nidhamu na kufanyakazi.
Mafanikio yake kwa taifa
JKT ilifanikiwa kuimarisha umoja wa kitaifa, ambapo vijana mbalimbali waliohitimu mafunzo hayo walijituma kufanyakazi za mikono kwa kujiheshimu, walikuwa viongozi mahiri, wavumilivu, wabunifu na walithamini kuhifadhi utamaduni wa taifa.
Jeshi hilo limechangia kuimarisha michezo mbalimbali na kuiletea sifa Tanzania kitaifa na kimataifa, pia vijana walikuwa mstari wa mbele kuokoa jamii katika majanga ya asili yaliyotokea kwa vipindi tofauti hapa nchini.
Taasisi hiyo ni mfano wa kuigwa kutokana na mataifa mbalimbali duniani kufika nchini kujifunza shughuli zake na wao kuanzisha JKT katika nchi zao, ikiwamo JKU Zanzibar, Zambia na Guyana.
Hifadhi ya mazingira imepewa kipaumbele kwa kutambua umuhimu wake kwa maisha ya jamii na wanyama, hivyo JKT hugawa miche bure kwa wananchi waishio jirani na kambi, sanjari na kubadilishana uzoefu na utaalamu wa suala zima la utunzaji na uhifadhi wake.
Naishauri Serikali itoe fedha zinazokidhi mahitaji ya JKT na kutembelea mara kwa mara kuona utekelezaji wa majukumu yake vikosini, pia kuwabaini watendaji wasiowaadilifu kiutendaji, ambao hufanya kazi kwa masilahi yao na sio kwa jeshi hilo na taifa kwa ujumla.
Watendaji wengi wanaichukulia JKT kuwa ni sehemu ya kujilimbikizia mali na kusahau majukumu yake, hivyo kusababisha jeshi hilo kuonekana halifai, kumbe baadhi ya viongozi wanaoteuliwa ni butu kiutendaji.
Kuundwa kwa JKT Staff SACCOS ni sehemu muhimu ya mafanikio ya JKT, ambayo ililenga kuwawezesha watendaji wake kuimarika kiuchumi na kuepuka kukopa katika taasisi za fedha ambazo hutoza riba kuba.
Mwitikio ulikuwa ni mzuri kwa maofisa, askari na watumishi wa umma, ingawa ushirika huo haujakomaa kutokana na uchanga na ubovu wa baadhi ya watendaji na wanachama kutokuwa waaminifu kiutendaji, hivyo kusimama na kuwa sehemu ya changamoto zilizopo JKT, tangu kuundwa kwake miaka 50 iliyopita.
Naamini viongozi hili wameliona na litafanyiwa kazi, ili ushirika huo uweze kuendelea kuwahudumia wanachama wake, kuwakomboa katika dimbwi la umaskini uliokithiri na wengine kujiunga zaidi, ili kuleta ushindani wa kibiashara na kuaminiwa na jamii.
JKT Staff Saccosni kimbilio la wanyonge walio wengi, uboreshaji na utendaji wake unahitaji watu walio makini kiutendaji, ili iweze kutekeleza agizo la Serikali kuwapatia wanachama mikopo ya kilimo kufanikisha mapinduzi ya kijani.
Operesheni za Vijana JKT
JKT mpaka sasa imekwishaendesha zaidi ya operesheni 102, kwa takwimu ya wakati huo ni Ujenzi 1980, Tija 1980, Juhudi 1981, Imarisha 1981, Tekeleza “B” 1982, Kujihami 1982, Safisha1983, Nguvu Kazi 1983 na Mshikano 1984.
Zingine zilikuwa ni wajibu 1984, Vijana 1985, Okoa 1985, Awamu ya Pili 1986, Nidhamu 1986, CCM Miaka 10 1987, Miaka 20 ya Azimio la Arusha 1987, Kizota 1988, Miaka 25 ya JKT 25 YA JKT 1988, Mpito 1989, Program ya Chama 1989 na Kambarage 1990/91.
Julai 10 mwaka huu ni kilele cha maadhimisho ya JKT kutimiza miaka 50 tangu liundwe mwaka 1963 na shamrashamra mbalimbali zimefanyika katika makambi na vikosi hapa nchini.
JKT kutimiza umri wa nusu karne sio kazi rahisi, hivyo muda umefika kwa viongozi wasiowajibika kujivua magamba kabla ya kusubiri kuvuliwa, ili kupisha wachapa kazi watakaowezesha jeshi hilo kusimama imara miaka 50 ijayo.
Muda huu utumike kuona changamoto zilizopita, zilizopo na zijazo na jinsi ya kupambana nazo kijeshi, ambayo huchangia kustawisha tija na ufanisi endelevu JKT na maamuzi ya siasa yaepukwe, kwani hudumaza maendeleo.
Hata hivyo Taifa la Israel lilisaidia uanzishwaji wa JKT miaka 50 hapa nchini ambapo ilitoa wataalamu mbalimbali na walipokamilisha majukumu yao walirejea nchini mwao.
JKT ilifuata mfumo wa uongozi wa Israel na Tanzania ilipeleka watu nchini humo kujifunza taaluma mbalimbali za malezi ya vijana,uendeshaji uongozi na

No comments:

Post a Comment