22 July 2013

EAC KUWA JUMUIYA YENYE MSISIMKO Na Mwandishi wa EANA
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt. Richard Sezibera, ameelezea umuhimu wa kuifanya jumuiya hiyo kuwa yenye msisimko zaidi na ya kuvutia." J umu i y a y e t u ( EAC) inatakiwa kuwa ya manufaa, yenye ufanisi, msisimko na ya kuvutia kuwawezesha wana Afrika Mashariki kupata kilicho bora kutoka kwake." Dkt. Sezibera alitoa kauli hiyo wakati akizindua utafiti juu ya uelewa wa raia wa Afrika Mashariki kuhusu mtangamano wa Jumuiya hiyo, unaofanywa kwa ushirikiano baina ya EAC na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (GIZ) katika nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na timu ya watafiti na maofisa waandamizi wa GIZ. Utafiti huo utakaofanywa katika nchi wanachama ambazo ni Burundi,Kenya,Rwanda, Tanzania na Uganda utachukua mwezi mmoja na unatarajiwa kumalizika Agosti 24.
Utafiti huo utafanyika kwa njia ya madodoso ya kwenye mtandao na kwa mahojiano ya moja kwa moja katika maeneo maalum yatakayochaguliwa kwenye majiji na miji ya mipakani."Utafiti huo unatarajiwa kutupatia mwanga juu ya namna ya watu wanavyoiona EAC, wanavyoifahamu vizuri, jinsi wanavyozifahamu nembo za EAC na jinsi wanavyotathmini utendaji wake," alisema.
Kwa mujibu wa taarifa ya EAC, kubwa zaidi katika utafiti huo ni kutathmini jinsi taarifa zinavyowafikia walengwa na jinsi inavyoeleweka na raia wa Afrika Mashariki na namna gani ya kuweza kusonga mbele.
Dkt. Sezibera alipongeza juhudi za utafiti, akisema zipo katika uhalisia wa kutaka kuileta jumuiya hiyo karibu zaidi na walengwa.Mkuu wa Mawasiliano na Masuala ya Umma wa EAC, Owora Othieno, alisema mradi huo unalenga kubaini kama ndoto za mtangamano za wana Afrika Mashariki zinaendana na matakwa ya Mkataba wa EAC.

No comments:

Post a Comment