22 July 2013

DARCOBOA YAJIPANGA KWA MRADI DART Na Heri Shaaban
WAMILIKI wa Daladala Mk o a wa Da r e s Salaam (DARCOBOA) wameanzisha Kampuni mbili zitakazoagiza magari kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Mwendo Kasi (DART) kwa ajili ya kutoa huduma jijini Dar es Salaam.Wamiliki hao wa DARCOBOA walifikia hatua hiyo ya kuunda kampuni zao Dar es Salaam jana, baada ya Serikali kuwapa waraka wa kusimamia mradi huo kwa sharti la kuwa wameanzisha kampuni inayotambulika. Akizungumza katika kikao cha wamiliki wa daladala jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa DARCOBOA, Sabri Mabouk, alisema lengo la kuunda kampuni hizo mbili ni kuwawezesha kutambulika ili kuweza kuagiza magari kutoka nje ya nchi yasiozidi 300.

"Kampuni zetu mbili moja itakuwa ofisi zake Ubungo katika kituo cha mabasi ya mikoani kwa sasa nyingine Jangwani. Alisema kila mmiliki wa daladala anatakiwa kujiunga katika kampuni hii ili aweze kuchangia hisa zitakazofanikisha mradi huo.Sabri alisema hatua ya kuanzisha kampuni hiyo ni dhamana waliyopewa na Rais Jakaya Kikwete, akitaka huduma hiyo isimamiwe na wamiliki wa DARCOBOA na sio uvumi wa maneno ya mitaani kuwa kampuni za wafanyabiashara wakubwa wamechukua tenda hiyo.
Alisema ifikapo Desemba mwaka huu kampuni hizo zitakuwa zimetambulika pamoja na usajili wake ili waweze kuagiza magari kutoka nje kazi itakayochuka mwaka mmoja ili magari yaweze kufika nchini."Wamiliki wa daladala Dar es Salaam tupo 5,000 hadi 6,000 kama DARCOBOA tumeweka kiwango cha kuchangia hisa ya sh. milioni 1.5 kila mmiliki ili tuweze kupata sh. bilioni 5 zitakazokuwa mtaji wa kuagiza mabasi hayo jambo ambalo linawezekana,"alisema.
Alisema katika barabara ya Morogoro mabasi 300 yatatoa huduma hiyo na mabasi 150 ofisi zake zitakuwa Jangwani na mengine 150 ofisi zake zitakuwa Ubungo.Aliwataka wamiliki wa daladala ambao bado hawajajiunga kwenye umoja huo kufanya haraka ili waweze kupata fursa hiyo. Alisema watakaoshindwa kujiunga katika kampuni hiyo watashindwa kusafirisha abiria katika Barabara ya Morogoro, kwani mradi huo ukianza katika njia hiyo unatarajia kuondoa wastani wa daladala 1,200 hadi 1,500 hivyo kulazimika kusubiri awamu ya pili katika Barabara ya Kilwa. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa DARCOBOA, Mashaka Karume, aliwataka wamiliki wa daladala kuwa kitu kimoja na kujenga tabia ya kuaminiana ili waweze kupata kiasi hicho cha fedha wanachokusudia

No comments:

Post a Comment