15 July 2013

CHADEMA SPIDI 120


  • YADAIWA KUONGOZA KATA ZOTE ZA UCHAGUZI
  • CCM, CUF UTATA, POLISI WATIA FORA VITUONI
Na Pamela Mollel, Arusha
UCHAGUZI mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha, umefanyika jana ambapo matokeo ya awali katika vituo vingi kati ya 136, yanaonesha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepata ushindi wa kishindo.
Kata zilizohusika na uchaguzi huo ni Themi, Kimandolu, Elerai pamoja na Kaloleni ambapo Jeshi la Polisi jijini humo, liliimarisha ulinzi kwa kuweka askari wenye silaha nzito
.
Upigaji kura katika vituo ulianza saa moja asubuhi wengi wao wakiwa vijana ambao ni mashabiki wakubwa wa CHADEMA.
Taarifa za awali ambazo hazijathibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zinasema katika Kata ya Kimandolu chama hicho kimepata ushindi katika vituo vyote 30.
Wagombea katika kata hiyo alikuwa Edna Saul (CCM), na Rayson Ngowe kwa tiketi ya CHADEMA.
Katika Kata ya Themi, upinzani ulikuwa mkali ambapo CHADEMA walimsimamisha Malance Kinabo ambapo mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), alikuwa Bw. Petro Ndaproi.
Ilipofika saa 11 jioni, matokeo katika vituo yalisomeka A 1, CCM 24, CHADEMA 97, A2-CCM 29, CHADEMA 85, A3-CCM 31, CHADEMA 81, A6-CCM 28, CHADEMA 87, A7-CCM 35, CHADEMA 70.
Katika kituo cha B1-CCM 27, CHADEMA 82, B2-CHADEMA 84, CCM 27, B3-CCM 21, CHADEMA 103, B4-CHADEMA 87, CCM 36, ambapo katika Kituo cha Shule Suye, A1-CCM 15, CHADEMA 47, A2- CHADEMA 39, CCM 24, A3-CCM 14, CHADEMA 35.
Kata ya Themi ambapo kulikuwa na vituo 15, upinzani ulikuwa kati ya CUF na CHADEMA ambapo Kituo cha Zahanati A1-CCM 29, CUF 35 na CHADEMA 62.
Kituo cha A2-CCM 20, CUF 26, CHADEMA 65, A3-CCM 19, CUF 40 na CHADEMA 40, A5-CCM 29, CUF 32, CHADEMA 58, Kituo cha Themi Mtendaji A2-CHADEMA 33, CCM 16 na CUF 02.
Hadi tunakwenda mtamboni saa 2:30 usiku, matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa katika kata ya Themi pekee ambapo mshindi ni Melance Kinabo aliyepata kura 674, Bw. Victor Mkolwe (CCM-324) Lobora Ndavirou (CUF-303).
Wafuasi wa chama hicho walikuwa wakishangilia ushindi huo katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo

No comments:

Post a Comment