22 July 2013

CCM WAFARIJIANA KWA KUSHINDWA NA CHADEMA



Na Jamillah Daffo, babati
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sophia Simba, amewataka wanachama wa chama hicho wasivunjike moyo kwa kupoteza viti vya udiwani katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni.Simba ambaye pia Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, aliyasema hayo juzi katika ziara yake wilayani Babati ambapo ameambatana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Amina Makilag

Katika uchaguzi huo, ambapo aliongea na viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya katika ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara na baadaye aliongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Old-Majengo mjini Babati.Katika uchaguzi huo CCM ilishindwa katika kata mbili za Bashnet iliyopo Babati Vijijini na Dongobeshi Wilaya Mbulu, ambapo CHADEMA iliibuka mshindi.
"Poleni kwa kushindwa kwani ilituuma sana, kwa kushindwa kule tunapigiwa kengele tusicheze kabisa ingawa sote tunajua chaguzi ndogo watu hawaendi kupiga kura sisi hilo linaweza likatuathiri pia na hali iliyotokea mkoani Arusha," alisema na kuongeza;"Ndugu zangu tusifanye mambo yetu gizani tutakuwa hatukitetei chama chetu, tutakwenda na maji."
Alisema pamoja na kujitahidi kufanya kampeni nyingi lakini walishindwa katika uchaguzi huo mdogo na badala yake kata kuangukia CHADEMA.Alisema hiyo ni dalili mbaya, hivyo wana-CCM wanatakiwa kujipanga upya ili kuondoa hali hiyo.
"Lazima tuwe na watu wetu ndani mwao ikiwezekana tuwalipe kwani wao wana watu wao ndio maana wanajua mbinu zetu,"alisemaAliwataka viongozi kuhakikisha wanakuwa karibu na wanachama ili ule unyonge uliosababishwa na vuguvugu la chaguzi ndogo uondoke, kwani wana-CCM hawajui kujibu mapigo bali hujipanga kuhakikisha pale walipokosea wanajirekebisha.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Makilagi, alisema mara nyingi wanawake wamekuwa wakishindwa kujiamani na uwoga unachangia kushindwa kutekeleza wajibu wao katika nafasi zao za uongozi.Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Manyara, Salome Luhinguranya, alisema ziara ya waziri inawezekana ikaleta mabadiliko na chachu katika mkoa huo ambao unaendelea kutekwa na wimbi la upinzani. Alisema ni wazi wapinzani wame j i a n d a a k u h a k i k i s h a wanashinda kwa nguvu

No comments:

Post a Comment