Na Halfan Diyu, Morogoro
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka 'SMG' anatarajia kuweka
kambi ya wiki nne nchini Kenya kwa ajili ya kujiandaa na pambano lake la
ubingwa wa Dunia, uzito wa kati.
Pambano hilo
linalosimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (WBF) litafanyika Agosti 30,
mwaka huu Katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Best Art
Promotion inayomsimamia bondia huyo, Makame Zumo alisema wameamua kumpeleka
Cheka nje ya nchi, ili aweze kupata mazoezi ya kutosha na kujiweka sawa kwa
ajili ya pambano hilo muhimu.
Zumo alisema
kwa kushirikiana na kocha wa Cheka, Saleh Abdallah wameamua kuweka kambi nchini
Kenya kutokana na nchi hiyo kuwa na Gym zenye kiwango cha hali ya juu na kuwa
na walimu wazuri wa mchezo wa ngumi.
Al i s ema wa n a u h a k i k a
watamsaidia bondia huyo kufanya vyema katika pambano lake dhidi ya mpinzani
wake Derick Findley kutoka nchini Marekani.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kabla ya
kupambana na bondia huyo kutoka Marekani, Cheka atapanda ulingoni Agosti 10,
mwaka huu mjini Morogoro kucheza mechi ya kirafiki na bondia Chimwemwe kutoka
nchini Malawi katika pambano la kirafiki la raundi kumi litakalosimamiwa na
PST.
Naye Cheka, amewaomba mashabiki wa ngumi
kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono katika mapambano yote mawili, ambayo
amesema ni magumu kwake, ingawa ana uhakika ataibuka na ushindi.
Kwa upande wake Kocha, Abdallah 'Komando' alisema
ameshamwandaa kikamilifu bondia wake kiufundi na kisaikolojia, ili kuhakikisha
anaibuka na ushindi katika mapambano yote mawili.
No comments:
Post a Comment