Na Shufaa Lyimo
UONGOZI wa klabu ya Azam FC umesema kwa
sasa timu yao inaendelea na mazoezi ya viungo 'gym' na ya uwanjani kwa ajili ya
kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza Dar
es Salaam jana Msemaji wa klabu hiyo, Jaffari Idd alisema lengo la kuanza mazoezi
mapema ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa huo safari hii na si kuishia nafasi ya
pili tena.
"Timu yetu
inaendelea vizuri na mazoezi vijana wapo katika hali nzuri na wameahidi kurudi
kivingine baada ya ligi kuanza," alisema Jafari.
Alisema upungufu
ambao ulijitokeza msimu uliopita, benchi la ufundi linaendelea kuyafanyia kazi
ili yasiweze kujirudia tena.
"Upungufu ambao ulijitokeza
msimu uliopita naamini hauwezi kujitokeza tena kutokana na mazoezi wanayoyafanya,"
alisema
No comments:
Post a Comment