23 July 2013

AIRTEL,UNESCO KUWEZESHA REDIO JAMIINa Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Airtel T a n z a n i a k w a kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamezindua mradi wa kuwezesha redio za kijamii kwa kuwapatia vifaa vya redio na kuwaunganisha na mitambo ya mawasiliano ili kuwafikia wananchi wa pembezoni kwa urahisi zaidi.

Mradi huo wa kipekee ulizinduliwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Masawe ambaye aliwatia moyo Airtel na UNESCO kuendelea na moyo huo wa kusaidia jamii kupitia redio zao za kijamii ambazo ndiyo zipo karibu na wananchi wa vijijini.
Aidha, aliwataka wananchi wa Karagwe kuitumia Redio Karagwe kwa maendeleo ya jamii na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi kwani zaidi ya watu takriban milioni mbili sasa watafikiwa na mawasiliano ya Redio Fadeco na Redio Karagwe.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa mradi katika Redio ya Fadeco Karagwe, Meneja Mahusiano ya Kijamii, Hawa Bayumi alisema kwamba mradi huo kwa kushirikiana na UNESCO utawanufaisha wa t u wa p emb e z o n i ambao radio za kijammii (Community Radios) ndio kimbilio lao la karibu katika kupata habari na taarifa mbalimbali.
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin alisema wana ushirikiano na radio za jamii kama nane na leo tumeanza na radio ya Fadeco ambapo maeneo mengine pia yatanufaika na mradi huo.
Kwa u p a n d e wa k e Mkurugenzi wa radio FADECO Bw.Joseph Sekiku alisema aliwashukuru Airtel na UNESCO kwa kuboresha ufanisi wa huduma za radio Karagwe sasa takribani watu wapatao zaidi ya milioni 2 wanapata mawasiliano ya radio tofauti na ilivyokuwa awali.
Kupitia mradi huo kampuni ya Airtel imeweza kuwapatia modem na simcard radio za kijamii ili kuwawezesha waandishi wao wa Habari kufanyakazi kwa ufanisi na kuinua mawasiliano katika maeneo ya vijiini nchini

No comments:

Post a Comment