05 February 2013

Viongozi VUKA-Tanzania wapatikana na kesi ya kujibu-Hakimu



Na Rehema Mohamed

VIONGIZI wa Shirika la VUKA-Tanzania wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa zaidi ya sh.milioni 100 fedha za mradi wa UKIMWI, wamepatikana na kesi ya kujibu.

Washtakiwa hao ni Bw.Adolf Mrema mwenyekiti wa shirika hilo,Bi.Hilda Urassa Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala na Bw.Straton Simon ambaye ni mshauri ambao wanakabiliwa na kesi hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao walipatikana na kesi ya kujibu baada ya upende wa mashtaka ukiwakilishwa na wakili Leonald Swai alidai kuwa wamemaliza kuleta mashahidi wao na kufunga ushahidi.

Baada ya kusema hivyo,Hakimu Fimbo aliwaeleza washtakiwa hao kuwa wana kesi ya kujibu na kuwapangia leo waje kuanza kujitetea.

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 37 likiwemo la kugushi,wizi,matumizi mabaya ya fedha.

Inadaiwa kuwa washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Juni11,2006 hadi Desemba 2007 jijini De se Salaam Wilaya ya Temeke.

Ilidaiwakuwawashtakiwa hao waliumia vibaya na kuiba zaidi ya sh.milioni 133 walizopewa na Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA na shirika la SAT-Tanzania kwa ajili ya kuendesha miradi ya UKIMWI.

No comments:

Post a Comment